View attachment 1436743
Hii tabia ya huyu dereva wetu inatia hasira sana. Mara ya kwanza ilikuwa Septemba 2016 gari ilikula mzinga ajali haina kinga. Dereva alikimbia abiria akaishia kupiga simu kutoa pole.
Hakuna hatua zozote zilizochukulia na mwajiri wala mamlaka. Aendelea kuendesha gari.
Mwaka huu pia gari imekula mzinga mkubwa na watu kupoteza maisha. Dereva amekimbia ametelekeza gari kawaachia msala makondakta na tingo.
Kwa tabia hii ya kukimbia gari inapopata ajali nashauri leseni yake ikiisha muda asipewe leseni nyingine. Akafanye kazi nyingine