Kila Binadam amezaliwa na Jinn

Kila Binadam amezaliwa na Jinn

Mkuu mtoa mada nina vijiswali vichache.
1, kwa nn Mungu aruhusu wewe kutawaliwa na huyu jini??
2.hebu tupe taarifa kuhusu hao majini wa mitume na Manabii wengine tofauti na mtume Muhamad (S.A.W)
3.huoni kama Mukulu atakua anatuonea kutupa majini watutawale.. Tena majini wenye nguvu sana kama unavyomuelezea wewe...

Au labda cjaelewa mada yako...
Msaada pliz
 
Mtoa maada naomba uniambia ufafanuzi wa aya 51 ya suwratul Swaaffaaat
Hakika nilikuwa na rafiki (Qaala qaailun minhum in-niy kaanali Qariynun).
Umeitoa katika kitabu gani ambacho kinasema kuhusu qariynun na haya maelezo uliyotuma.

Nimetumia muda wangu zaidi ya masaa 12 kusoma tafsiri ya wanavyuoni mbali mbali kuhusu maelezo yako ya qariynun.
Nimeangalia tafsiri ya wanavyuoni kupitia www.altafsir.com
Ni wanavyuoni wa ulimwenguni waliopasishwa 86 na vitabu vyao, sikuona haya maelezo uliyoyaandika wewe.
Sasa naomba unipatie kitabu gani, mtunzi nani, anaeleZea hizi habari za qariyn ili nipate ufafanuzi zaidi.
Tukimalizana hapo ndio tutakuja kuelezana mengine zaidi,
Kwa wanajf kwanza tusibiri hili jibu
Ahsanteni
Hapo ndipo ninapoipendea JF, akijibu naomba uni-tag mkuu.

Kaka ...
 
aliyezaliwa na majini ni wewe na watoto wako..ninachojua mimi na familia yangu na taifa langu tumefunikwa kwa damu ya Yesu kristo aliye hai na roho mtakatifu akiniongoza ktk kila jema nifanyalo hapa duniani..
 
Hapo ndipo ninapoipendea JF, akijibu naomba uni-tag mkuu.

Kaka ...
Huyu mtoa mada ni maandazi kichizi yan.. Kaleta mada ila tukimuuliza maswali kwa ajili ya ufafanuzi anasepa au atakuja na aya zake za kukariri alaf anaandika kwa matamshi ya kiarabu.. Mpuuzi sana huyu
 
tupe vitu ustaadh hizi mada zinakuja chache sana wengine tunapenda hio elimu aisee shusha vyombo kaka

Shukran shukran sana ndugu yangu.

Kama mada inavyosema kuwa huyu Jinn hupenda mambo ya kipuuzi tu na negative things na ndio amewakamata walio wengi sana na kuwa-control na ndio maana unaona wengi wao huchukia kuskia vitu vyenye faida kwao na hupenda kuskia upuuzi na habari zisizo na maana yoyote.

Shukran sana akhiy kwa kuwa pamoja.
 
Hii
Shalom/Salaam.

images


Kila Binadam amezaliwa na Jinn/Jinni. Ndio KILA BINADAM AMEZALIWA NA DJINN/JINN/JINNI. Simaanishi kuwa wazazi wetu waliotuzaa ni MAJINI hapana, ila nnachomaanisha ni kuwa kila mmoja wetu amezaliwa akiwa na JINN. Jinn huyu yuko pale kwa ajili ya kumuamrisha mtu kufanya mambo maovu, machafu, mabaya, shari kwa kifupi humuamrisha binadam kutenda DHAMBI tu muda wote. Jinn huyu anajulikana kwa jina la QAREEN/QARIYN/QARIN kwa lugha nyepesi jina hili ukilitafsiri maana yake ni RAFIKI. Hapa ningependa ninukuu baadhi ya aya toka kwenye QUR’AN ikizungumzia Qariyn kuwa ni Rafiki. (Surat Swaffaat aya ya 50-57)

”Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe (humo motoni). Hakika nilikuwa na rafiki (Qaala qaailun minhum in-niy kaanali Qariynun). Aliyekuwa akiniambia “ Ah! Wewe ni katika wale wanaosadiki (hivi unaamini kweli) ?. Ya kuwa tutakapokufa na kuwa udongo na mifupa (eti tufufuliwe tena) na tulipwe (kwa tuliyoyafanya kama anavyosema Muhammad) ?”. Atasema “Je, mtamchungulia (muone anavyoadhibiwa) ?”. Basi atachungulia na atamuona katikati ya JAHANNAM (huyo rafiki yake anavyoadhibiwa, Qariyn). Kisha amwambie “Wallahi ulikaribia kunipoteza wewe”. “Kama isingekuwa NEEMA ya MOLA wangu, bila shaka ningekuwa miongoni mwa waliohudhurishwa (humo motoni kama wewe)”.

Kwa kifungu hiko cha aya unaweza kuona kuwa huyu ni mmoja kati ya JINN wabaya sana ambapo humfanya mtu kutenda maovu na machafu tu muda wote. Na kadri unavyofanya maovu na machafu anazidi kupata nguvu na kadri unavyofanya mema na mazuri basi anazidi kuishiwa nguvu.

Jinn huyu unaweza ukamuita na akaja, yaani akatoka ndani ya mwili wako na ukamuona LIVE, YES. Anaweza akaja na ukamuona kama wanavyoitwa Jinn wa aina nyingine na wakaja nae huyu pia vivyohivyo yawezekana kufanya hivyo na akaja. Kwa lugha nyingine anaweza akawa mtumishi wako ukammiliki na akakutumikia kama watu wanavyowatumikisha Jinn wengine, NDIO. Ila zoezi hilo ni gumu sana kulifanya na linaweza kuchukua miaka kwa miaka kulifanikisha. Qariyn wa Mtume Muhammad (S.A.W) aligeuzwa akawa MWEMA kabisa, sasa basi kwa kufanywa hivyo, kwa kuwa QARIYN kazi yao ni kumuamrisha na kumsukuma mtu kufanya mambo maovu, mabaya na machafu basi QARIYN wa MTUME aligeuzwa akawa mwema akawa kinyume na hivyo ikawa anamuamrisha na kumsukuma MTUME kufanya mambo yaliyo mazuri na mema muda wote. Sisi binadam wa kawaida hatuna nguvu za kutosha kuweza kufanya hili jambo, isipokuwa watu walio safi kabisa na wenye kufanya mambo mema muda mwingi na kwa miaka mingi pia sio kitendo cha muda mfupi kuweza kukifanikisha, HAPANA.

Mambo Gani Anayoweza Kukufanyia Qariyn Ukishamkamata/Kumdhibiti ?.

1.) Anaweza kukupa taarifa za mtu yoyote duniani. Kumbuka kuwa kila mtu ana Qariyn wake, hivyo utakapomkamata Qariyn wako utakuwa na uwezo wa kumpeleka/kumtuma kwa Qariyn wa mtu mwengine popote alipo duniani na akakuletea taarifa za mtu huyo popote pale alipo. Qariyn, yuko pale tangu siku ambayo tunazaliwa kwa hiyo wanajua habari zote kuhusu sisi tangu tunazaliwa mpaka hapa tulipofkia na mpaka kufa kwetu.

2.) Wana uwezo wa kutibu maradhi na magonjwa tofauti tofauti kutegemea na ugonjwa uliopo na dawa au tiba itakayotumika. Si dawa unayotumia wewe kupona ugonjwa fulani ndio atakayotumia Mhindi au Mchina kupona, ugonjwa mmoja unaweza unaware na Dawson zaidi ya Kimi na sio zote tunazifaham, hivyo wanajua vitu vingi na hupeana information juu ya mambo mengi ambayo sisi binadam hatuyajui.

3.) Wana uwezo wa kupata vitu vilivyoibwa au kupotea kama ilivyosemwa mwanzo kuwa huwasiliana wao kwa wao kuweza kujua kitu flani hata kama kimefichwa na nani na wapi, wana uwezo wa kujua na kufaham wapi kilipo/vilipo vitu hivyo.

4.) Wana uwezo wa kumshawishi Qariyn wa mtu mwengine kumfanya huyo mtu kufanya kitu chochote unachokitaka wewe akifanye.

5.) Wana uwezo wa kukujulisha nani anakuja muda gani kukuona kabla hata hajaja huyo anayekuja kukuona. Yupo bwana mmoja ambaye hana Jinn wa kupandisha wala wa kumpasha habari ila amefanikiwa kumkamata/kumdhibiti Qariyn wake, basi kila muda apatapo mgeni humueleza mgeni huyo nini kilichomleta na kwa nini amekuja/shida gani iliyomleta, mwaka gani aliozaliwa, muda na hata taarifa za wazazi wake kwa ujumla. Hali hii hupelekea kwa asilimia kubwa kama si zote kufanya mgeni aliyekuja kukuona kuweka IMANI juu yako kwa kiwango kikubwa kabisa, hii ni kwa sababu huyu bwana humtumia Qariyn wake kupata information toka kwa Qariyn wa mgeni husika aliyekuja, hii hupelekea watu kumuamini sana.

Hatari Inayotokana na Huyu Jinn :

Kumkamata au kumdhibiti Jinn huyu sio kazi rahisi hata kidogo. Kiuhalisia hawa ni Jinn waovu sana na pia ni very powerful Jinn, wana nguvu sana. Wanajua kila kitu kuhusu wewe, kitu gani unachoogopa au kinachokutia hofu na kukuogopesha, kitu gani kinachokufanya uwe na huzuni, madhaifu yako yote wanayajua na vingine vingi kuhusu wewe. Kwa hiyo kumdhiti kiumbe wa aina hii ni kazi ngumu kiasi.

Kuna njia KUU mbili zinazoweza kutumika kumkamata/kumdhibiti Jinn huyu na njia hizo ni NJIA YA GIZA na NJIA YA NURU (NJIA YA RUHANI). Njia ya GIZA inajumuisha kufanya mambo maovu, machafu, mabaya na dhambi ndani yake kukiwemo ushirikina pia, na ndio njia iliyo rahisi kabisa kutumia kumdhibiti QARIYN (NJIA YA GIZA). Kwa sababu mtu anapoamua kumdhibiti/kumkamata Qariyn wake kwa njia hii ya GIZA ni kwa sababu ya kumtumia kwa ajili ya mambo maovu na ya kishetani, uchawi, ubaya n.k. Hivyo Qariyn anakuwa wazi kabisa juu ya mambo haya na anafurahia kwa sababu ndio njia yake tangu umezaliwa, yeye ni mwenye kuelekea kwenye njia hii tu ya maovu na uovu muda wote, hivyo huwa rahisi kuwa nae karibu.

images


Ila mtu anapotaka kumkamata/kumdhibiti Qariyn wake kwa njia ya NURU au NJIA YA KIROHO (ROOHAN WAY), kitu cha kwanza kitachomlazimu kufanya ni kutumia muda mref kutenda yaliyo mema na kujiepusha na madhambi, kufanya ibada, kuswali na vitu vingi vitakavyokuweka na kukufanya kuwa safi kabisa (PURE & GOOD). Kwa sababu mtu anapokuwa amezama katika masuala ya KIDINI na kuwa karibu na MUNGU humfanya Qariyn kuwa dhaifu na huishiwa nguvu kwa kiasi kikubwa sana, hivyo inakuwa rahisi sana kumkamata/kumdhibiti, kinyume chake anakuwa hana nguvu za kuweza kuku-control badala yake wewe ndiye unayem-control yeye. Hii si kazi ndogo kwa sababu ni ngumu sana kwa binadam kuwa mtakatifu/msafi kwa kipindi/muda mfupi, humlazimu kufanya ibada kwa muda mref kuweza kujitengeneza KIIMANI na KIROHO zaidi na kuwa karibu zaidi na MUNGU.

Watu nnaowafaham ambao wameweza kuwakamata/kuwadhibiti Qariyn wao kwa haraka haraka ni watu wenye umri kama kati ya 47 na 62 hivi. Kusema ukweli ni watu watakatifu, watu wasiokosa kuswali swala zao, wamekuwa mbali na dhambi na hata na matamanio ya hapa na pale ya nafsi zao, they are pure & good.

Unapofanya zoezi la kumuita/kumdhibiti Qariyn haitakiwi kukosea hata nukta, kiukweli hata Qariyn atajaribu kukutisha kama vile KUKUUA ili uache zoezi lako, sasa ukionekana kuogopa na ukakosea kwa bahati mbaya ukatoka nje ya duara ambalo ndilo litakuwa limekuzunguka ikiwa ndio ULINZI WAKO ukaogopa then ghafla ukatoka nje ya mstari kitakachofata kwako ni KIFO. Kuna jamaa mmoja alikuwa amefanya zoezi hilo kwa muda wa siku 30, sasa katika siku zake 5 za mwisho amalize zoezi lake, Qariyn alijitokeza katika taswira ya kimvuli na ndivyo wanavyokuja kwanza, au huja katika taswira ya mfano wako, mithili ya wewe jinsi ulivyo nae huja kama hivyo ulivyo. Atazunguka chumba kizima akitoa sauti za ajabu ajabu za kukutisha na vitisho vingine vingi n.k

Katikati ya zoezi lake huyo jamaa kulikuwa na moto ndani ya chumba ukaanza kuwaka, akiwa amekaa kwenye duara lake moto ukaanza kumsogelea, yote ni vitisho ili atoke nje ya mstari, moto ulizidi kuongezeka uvumilivu ukamshinda akatoka nje ya duara ambalo ndilo lilikuwa ni ULINZI wake. Alivyotoka tu hakuona moto wala majivu na wala hakukuwa na kitu chochote kilichoungua na Qariyn hapohapo akayayuka na kupotea. Siku iliyofuata akaanza kutokwa na damu kwenye kila tundu ya mwili wake, akaanza kuumwa na ndani ya wiki moja akaiaga dunia. Nimeshaskia habari nyingi tu za mfano wa hii. Qariyn sio mchezo wa kucheza nao hata kidogo. Anakujua vizuri sana zaidi ya wewe unavyojijua binafsi. Ni ngumu sana kum-control.

images


Nimeshaskia mara nyingi na hata wewe utakuwa umeskia kuwa kuna nyumba au sehemu huwa ikiandamwa na mtu ambaye alikuwa akiishi eneo hilo au kwenye nyumba hiyo au mtoto au mtu yoyote labda ambaye ameuliwa kwenye eneo au nyumba husika. Sasa kiuhalisia yule anakuwa sio huyo mtu kwa sababu QUR’AN na BIBLE vinatufundisha kuwa mtu anapokufa ROHO hupaa na kwenda MBINGUNI KWA MUNGU na wala ROHO zetu hazibakii huku duniani na kutangatanga pasina kuzingatia umekufa kifo cha aina gani ROHO itaenda tu mbinguni. Ile sio roho ya huyo mtu anayeonekana kiuhalisia katika eneo au nyumba hiyo ila huyo anakuwa ni QARIYN wa huyo mtu aliyekuwa akiwa anaishi katika eneo hilo. Kwa sababu tunapokufa Qariyn wetu hawafi kwa sababu wao wana maisha yao wao kama wao na sisi tuna maisha yetu sisi kama sisi, hivyo tunapokufa Qariyn huendelea kuwepo tu na wanakuwa wako huru kufanya chochote kile wanachojiskia kufanya.

Mtu anapokufa na kumuacha Qariyn wake, wengine huchagua kujitokeza kama roho ya mtu aliyekufa na kutokea kwenye eneo au nyumba aliyokuwa akiishi au wengine huwatokea hata jamaa zao wa karibu pia kwa sura zilezile za wapendwa wao marehem. Kama nilivyosema kuwa, kwa kuwa wanakuwa na sisi tangu mtu unazaliwa mpaka unapokufa na kuamua kujitokeza kama kimvuli au picha/taswira halisi ya mtu husika aliyekufa, wengi hupelekea kuamini kuwa aliyetokea ni ndugu yake kweli. Na kwa kuwa wanajua taarifa zote kuhusu sisi tangu tulipozaliwa na tutakapokufa, hivyo hata akikwambia jambo lolote lile linalohusiana na maiti/marehem wako hupelekea wewe binafsi kuamini kwa asilimia zote kuwa ni kweli yule aliyetokea ni mtu wako wa karibu aidha BIBI au BABU au MAMA au BABA lakini kiuhalisia HAPANA. Sio yeye. Huyo hujulikana kwa jina la Djinn/Jinn aina ya QARIYN.

AHSANTA.
Hii ni kwa mujibu wa kitabu na maandiko ya majini?
 
Kila mtu ana nafsi huru anapanga na kuchagua afanye nini. Hizo habari za kuwa na director ni uzushi tu
 
Mtoa maada naomba uniambia ufafanuzi wa aya 51 ya suwratul Swaaffaaat
Hakika nilikuwa na rafiki (Qaala qaailun minhum in-niy kaanali Qariynun).
Umeitoa katika kitabu gani ambacho kinasema kuhusu qariynun na haya maelezo uliyotuma.

Nimetumia muda wangu zaidi ya masaa 12 kusoma tafsiri ya wanavyuoni mbali mbali kuhusu maelezo yako ya qariynun.
Nimeangalia tafsiri ya wanavyuoni kupitia www.altafsir.com
Ni wanavyuoni wa ulimwenguni waliopasishwa 86 na vitabu vyao, sikuona haya maelezo uliyoyaandika wewe.
Sasa naomba unipatie kitabu gani, mtunzi nani, anaeleZea hizi habari za qariyn ili nipate ufafanuzi zaidi.
Tukimalizana hapo ndio tutakuja kuelezana mengine zaidi,
Kwa wanajf kwanza tusibiri hili jibu
Ahsanteni

Nashkuru sana mkuu kwa kutumia muda wako kujifunza na kujua mambo. Kitabu nilichotoa hili jina QAREEN ni Kitabu Kitakatifu cha ALLAH (QUR'AN) na wala sikutoa kwenye Kitabu chochote coz ni Kitabu ambacho hakina shaka ndani yake.

Ni sura ya 37 aya ya 51 imeeleza hili jina na pia kuna aya zaidi ya hiyo imeongelea kuhusu QAREEN ukiacha hiyo aya. Maana halisi ya hii aya utaipata juu hapo kwenye mada kuu/husika coz kuna aya ambazo zinasmama zenyewe kama zenyewe kwenye QURAN ukiisoma tu unaielewa moja kwa moja. Na kuna aya nyingine huwezi kuzielewa kwa kuisoma yenyewe kama yenyewe mpaka uwe na upeo wa hali ya juu, ila utaweza kuielewa kwa kusoma kifungu cha aya aidha za mbele au nyuma yake.

Ila kwa aya hii ya 51 Surat Swaafat inajieleza tu yenyewe kama upeo wako ni mpana utaweza kuelewa bila ya kusoma aya za mbele ya aya hiyo.

Aidha kwa maana halisi ya neno QAREEN aliyeeleza maana yake ni MTUME MUHAMMAD (S.A.W) ambaye hata hao wanazuoni/wasomi uliosema umewatazama wanamfata yeye na hakuna hata mmoja anayeweza kumzidi kwa ilmu aliyokuwa nayo MTUME MUHAMMAD (S.A.W) ndiye aliyeelezea maana halisi ya neno hilo QAREEN.

Aidha kwa maelezo ya ziada kwa kukusaidia tu ili kuweza kuongeza ufaham unaweza ukapitia maelezo kwenye hii site hapa chini


Qaree - Wikipedia The free Encyclopedia

AHSANTA.
 
Back
Top Bottom