AL-USTADH
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 406
- 226
- Thread starter
- #121
Shukrani kwa majibu yako,
Pamoja na maelezo yako, bado hujanambia majini hasa ni kitu gani?
nimeshakwambia kuwa kuna threads humu zimewaelezea vizuri tu tafuta uzisome utaelewa vizuri au kwa jibu unalotaka kujua kuwa majini ni kitu gani majini ni viumbe walioumbwa na muumba wetu.
Hujasema kwanini wanatumia Quran ambayo imeteremshwa kwa binadamu wakati wao ni majinni? Kwanini wasiwe na kitabu chao sawa na maumbile yao na wakakifuata hicho?
Ndio maana nikakwambia tafuta hizo threads utaelewa coz wameeleza vyote hivi kuwa majini pia wana dini wapo waislam, wakristo n.k.
Sasa kwa waislam lazma wafate kitabu hiko coz ni kitabu cha dini yao ya kiosks wakiwa kama viumbe.
Nakwambia elimu yako ndogo sababu ya maelezo yako hapo kwenye nyekundu nani kakwambia QURAN imeteremshwa kwa binadam tu...?. Kabla ya kubisha usichokijua jaribu kwanza kukifaham ndio uandike ikiwa unaelewa unachokiandika sio unaandika tu kitu usichokijua wala kukielewa wala kuwa na ufaham nacho.
Kwa upande wa Ibilisi, je ni kweli ni jini kwa kuwa alikuwa miongoni mwa majinn? Hivi, mbwa au chui akiwa miongoni mwa maji naye ataitwa jinni?
Ndio Iblis ni miongoni mwa majini kwa sababu imeshaandikwa kuwa fafasaqa min amri rabby.
Ukiwa na elimu pana juu ya majinni maana yake unaelewa kila kitu? Elimu yako inafananaje kiasi cha kusema wengine wana elimu ndogo? Yako ukubwa wake kiasi gani?
Elimu huzidiana kwa kiwango na elimu haina mwisho ni sawa na alive na Bachelor hawezi kuwa sawa na mwenye Master's pia hawezi kufanana na mwenye PhD.
Elimu yangu ukishaijua itakuhusu kitu gani hasa...?. Elimu ndogo hujidhihirisha kwa uelewa na upeo wa kile kinachotolewa na mhusika hasa juu ya ufaham wake, kwa sababu ujinga wa mtu hujidhihirisha kutokana na matendo yake.
AHSANTA.