Kila baraka ina laana ndani yake



Lakini akaja kumtamani mke wa mjakazi wake.... LAANA! na ili apate kummiliki kikamilifu nadhani alimfanyia mjakazi wake figisu mbaya

nilikuwa nataka nijue... hiyo HEKIMA aliyopewa.. ni ipi
 
Lakini akaja kumtamani mke wa mjakazi wake.... LAANA! na ili apate kummiliki kikamilifu nadhani alimfanyia mjakazi wake figisu mbaya

nilikuwa nataka nijue... hiyo HEKIMA aliyopewa.. ni ipi
Kwa muktadha wa mada na uhalisia wake (binadamu) chini ya mbingu hakuna mwanadamu mkamilifu la hata mmoja na kila mmoja wetu ana udhaifu wake.... Hivyo pamoja na hekima kuu aliyojaaliwa bado udhaifu wa kibinadamu haukumwepuka
 
For sure, Mungu atujaalie hekima kwakweli hata tupatapo tusimsahau.
 
Kaka mkubwa kwanza hongera kwa mada nzuri. Hapa nataka niseme kitu.

Ukisema laana hapa naona umeipa uwanja mkubwa sana kuliko uhalisia wake.

Laana hawawezi kuizungumzia wakanamungu sababu hawana elimu nayo,laana ikizungumziwa na watu wa dini ndio mahala pake.

Nini maana ya laana ?

Kwa ufupi laana ni kufukuzwa nje ya rehma za muumba au kutolewa nje ya rehma za muumba. Laana hutokea baada ya mtu kuchupa mipaka katika kukosea,na si kila laana inamfikia mja. Hapa nitatoa mifano au mfano.

Tukimzungumzia Ibilisi laana za Mola zimfikie,huyu ametolewa nje ya rehma za Mloa wetu muumba muumba.

Huwa tunasema wamelaaniwa wale wanao kula mali za ma yatima,na wamelaaniwa wale wenye kubadili maumbile,na wame laaniwa wale wenye kudanganya kwenye mizani yaani vipimo.


Tukija katika suala la mali na vizazi na mengine kama uliyoyasema huko juu,hayo yote yanaingia katika mtihani au kutahiniwa na Mola.

Huwa tunaambiwa mali,wanawake na watoto ni mtihani kwetu. Kwa maana tukivitumia vibaya neema hizo lazima tutaangukia katika madhambi,madhambi kivipi ?

Endapo ukizitumia mali ulizo pewa kwa kufanya maovu hiyo sio laana bali ni mtihani unaokupelekea katika kufanya madhambi.

Ukiwa mzinifu hali kadhalika,ukipewa kizazi usipokilea na kukipa mafunzo mazuri ujue huo ni mtihani na utakuja kuulizwa juu ya wale au vile unavyovisimamia.

Swali ni wa kina nani wana laani ?

Laana ina laaniwa na viumbe mpaka wa baharini wanatoa laana.

Ama kuhusu suala la mtume Suleyman,yeye aliruhusiwa kuoa mpaka vijakazi na haikuwa kosa wala hatusemi alikosea.

Ila hili la kuhusu kumtamani na kumfanyia figisu msaidizi kisa mwanamke,hapa unatakiwa utupe ushahidi.
 
Hujawahi kuniangusha pamoja na tofauti zetu kiimani, ndani ya intelligence tu wa moja... Ngoja nisake ushahidi nikiukosa nitasema nimeukosa
 
Kwa muktadha wa mada na uhalisia wake (binadamu) chini ya mbingu hakuna mwanadamu mkamilifu la hata mmoja na kila mmoja wetu ana udhaifu wake.... Hivyo pamoja na hekima kuu aliyojaaliwa bado udhaifu wa kibinadamu haukumwepuka
Mkuu ivi mwisho wake mfalme Suleiman ulikuwa ni upi alikufa na utajiri wake au ilikuwa namna gani
 
Kwa muktadha wa mada na uhalisia wake (binadamu) chini ya mbingu hakuna mwanadamu mkamilifu la hata mmoja na kila mmoja wetu ana udhaifu wake.... Hivyo pamoja na hekima kuu aliyojaaliwa bado udhaifu wa kibinadamu haukumwepuka
HEHEHE MBUNYE sio ya mchezo mchezo... haichagui... uwe tajir au nabii.. yenyewe inakuvuta tu...
 
Mfano : katika familia mmoja kafanikiwa sana lakini kuna mmoja anapata mateso ya ajabu na hawamjali ila familia inashangilia tu kama zuzu pasipo kujua aliyefanikiwa kafanya nini . Basi ujue ubaya na wema ni mapacha
 
Kama kumbukumbu zangu ziko poa aliyemtamani na kumchukua mke wa mtumishi wake kwa kumfanyia zengwe afe hakua Suleiman Bali alikua babake na Suleiman (Daudi ) ndo alifanya ivoo kwa askari wake aliitwa uria

Daudi Aliweka order jamaa (uria) awekwe Mbele sehemu ya vita vikali ili afe na kweli akafa

Then huyo mwanamke aliyechukuliwa na Daudi ndo baadae akamzaa Suleiman baada ya mtoto wake wa kwanza kufa

Anyway thanks for good lesson
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…