mshana mimi nitakuwa tofauti kidogo na wewe, iwe unayosema wewe baraka au jaha, lakini kuna vitu ambavyo mungu anampa mtu yoyote na kuna vitu ni kwa ajili ya watu maalumu aliowateuwa, hatuwezi kusema leo kwa sababu mungu alimpa yesu au mussa utume, tukafikiria mtu yeyote anaweza kuwa mtume, labda hawa mitume wetu wakufoji na manabii uchwara, kama mungu kampa nguvu mmasai ya kuuwa simba, ni kichekesho kilioje kwa wewe mpare au muhaya ukakute simba kauliwa na mmasai ukajipaka damu na kusema na wewe ni shujaa, hapo lazima wanaofahamu ishu ilivyo wakucheke sijui wewe mwenyewe unajionaje pale watu wanaofahamu mchezo mzima wakisimama mbele yako na kukupigia makofi utahisi wanakupongeza au wanakucheka?.
Pili mungu kumbariki mja wake jaha au baraka kama usemavyo kuna laana nyuma yake hii si sahihi, kwa sababu chochote anachokupa mungu kinaweza kuwa mtihani kwako, lakini pia ni kawaida ya roho za kibinaadamu kuonelea husda pale mungu anavyomfaidisha katika rehma zake mmoja wetu, lakini pia mungu siku zote akikupa kilema hukupa na mwendo, ni muhimu sana watu kuelewa mwenyezi mungu anapoamua kuleta rehma kwa waja wake na akamchagua mmoja wetu kuwa ndio rehma hiyo ipitie kwake, basi hata binaadamu ufanye vipi kama mungu kaamua rehma hiyo iwafikie waja wake itawafikia kwa sababu binaadamu hawezi kushindana na rehma na uwezo wa mungu, mwisho wa siku ukilaani laana itakufikia mwenyewe, kushindana na uwezo na utukufu wa mungu katika kuumba kwake na kuvitukuza vyengine dhidi ya vyengine ni sawa na kushindana na aliekuumba.