safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,164
- 15,848
Kama akili zako zinang'amua mambo sawa sawa basi utajua tu kwamba huu ulimwengu wetu umeumbwa na Mungu wala hauja exist tu kwaanbahati mbaya au nature.
Kama mtu hakubali kwamba yale maghorofa ya kariakoo hayajaja yenyewe basi lazima asikubali pia kwamba dunia hii ipo ipo tu kwamba eti hakuna msababishi.
Kila unachokiona kina msababishi wake tena ana akili na malengo ya kufanya.
Simu unayotumia haikuibuka tu lazima kuna aliyesababisha na alikuwa na Malengo yake ambayo ndio wewe unatumia sasa hivi hayo ndio malengo
Hiyo nguo unayovaa sio nature kwamba ati imejitengeza yenyewe tu hapana,kuna mtu alibuni na akasababisha tena kwa malengo maalumu ya watu kujisitiri na kujihifadhi na lengo hilo limeetimia
Kiatu chako nacho hakikuja tu paap kwamba kimeibuka yakhee,lazima kuna aliyesababisha akatumia akili zake akabuni na akatengeneza na malengo yake yakatimia.
Sasa ikiwa vitu hivi vidogo vidogo katika dunia vina msababishi wake tena mwenye akili na ufahamu wa kufikiria mambo sawa sawa je dunia vipi isiwe nna msababishi aliyeiumba tena mwenye akili na ufahamu na akatuumba sisi tuje duniani hapa kwa malengo Maalumu...?
Akili salama lazima ikubali kwamba ulimwengu umeumbwa na Mwenye akili na fikra sawa sawa tena kwa malengo maalumu.
Haiwezekani kwamba kitu kisichokuwa na akili wala fikra kizalishe kitu ambacho kina akili na fikra na malengo
Vijana mnaomkataa mungu mkifa mkamkuta mtakuwa mumepoteza sana,vijana tunaomkubali Mungu tukifa alafu tusimkute tutakuwa hatujapoteza kitu chochote zaidi ya kupata faida.
Wanaoamini Mungu wana dhamana ya kuishi kwa raha hapa duniani na huko akhera kwa sababu wakimkuta walishajiandaa tayari,na kama hawakumkuta (wadaivyo kina Kiranga ) basi hawana cha kupoteza.
.
Mkubali Mungu uishi kwa amani isiyo na wasiwasa kabisa.
Mungu awabariki nyote..