MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,297
Unawaambia wananchi yale ambayo unajua wanataka kusikia (maisha bora kwa kila mbongo, ambulance za bajaj kwa akina mama wajawazito huko maeneo ya milimani) kisha unajiendea Ikulu na kupiga usingizi mnono (yaani mzigo mzito).
Kesho yake wanakuuliza vipi baba yale uliyotuahidi, unasema siyo kila ahadi lazima itekelezwe na papo hapo unamwaga ahadi nyingine mpya kabisaaa (kilimo kwanza, maji kwanza, flyovers ubungo, nk), na wananchi wa kusadikika wanakupigia makofi. Unarejea Ikulu unajichapia usingizi mnono. Baada ya miaka yako kumi Ikulu unajiondokea mlaini na matrilioni yako!
Basi angaa kwa miaka yako miwili iliyobakia watoe watoto wa shule sakafuni na uwaweke kwenye madawati - utakuwa na kitu cha kukumbukwa katika historia ya nchi hii ya Kusadikika!
Maisha bora kwa kila mtanzania