Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Nilionesha kushangaa kwangu mapema kwa kuwana vijana wa green guard kwenye mkutano wa hadhara wa Kikwete kama rais.

Huyu mama wa green guard alikuwa akisaidiana na mapolisi katika kuwapanga watu ili msafara mh.Kikwete apate njia ya kuingilia uwanjani. Hivi CCM wanashindwa kuliamini jeshi la polisi na kamati ya maandaliz ya ziara ya rais?

Hawa nao mabarobaro wa green guard walikuwepo wakiendelea kufanya kazi za kiulinzi kama vile hatuna jeshi au vyombo rasmi vya kumlinda rais na mikutano ya hadhara au makusanyiko.

Pia kulikuwa na mapokezi yasiyo rasmi ya vijana wa CCM walikuwa na pikipiki zilizofungwa bendera,,, kwa ujumla ziara ya rais ilipoteza sura hali na kupata sura nyingine, naam, sura ya ziara ya mwenyekiti wa CCM taifa akikagua uhai wa chama Mwanza.

Wakati nikiwa mshangao bado niko nao katika fikra zangu, nikashikwa na bumbuazi pale viongoz wa CCM wa mkoa wa mwanza walipotumia hadhara ya kiserikali kupokea vijana waliorudisha kadi,,, kuna kitu nimejifunza.
Si kingine,,CCM haina ubavu wa kuitisha mkutano wa hadhara Mwanza na kujaza watu kias kam kile, hivyo uongoz wa CCM JIJI la mwanza wakatumia mwanya huo kufanya siasa na huku wakijua kuwa mkutano ule umegharamikiwa na fedha za umma.
Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma na kitu hichi lazima tukikemee. Katiba ijayo isitoe nafasi kwa rais wa nchi kuwa kiongoz wa chama cha siasa.
[video=youtube_share;5aDQMDjNKLY]http://youtu.be/5aDQMDjNKLY[/video]
NISEME JAMBO HILI.
Kiukweli Ziara ya mh rais Kikwete jijini Mwanza iliishia na mkutano wa hadhara katika viwanja vya Furahisha, pamoja na mambo mengine Mh rais alipokea kadi zilizorudushwa na vijana wa vyama vingine kama kipande cha video niliyoichukua uwanjani kinavyoonesha. Kwakuwa Mh rais alifika uwanjani kwenye saa 12:15 jioni, hivyo wakati zoezi la urudishaji kadi likifanyika tayari usiku ulishangia na hii ilipelekea video hii iwe na kiza kwa kiasi fulani.
Yawezekana kutokutenganisha kofia ya urais na uenyekiti wa chama si tatizo, tatizo ni kwa mvaa hiyo kofia hutokea wakati mwingine kushindwa kutafautisha kazi za hiyo kofia na umma wakati mwingine hushindwa kumtofautisha mtu aliyevaa kofia ya uenyekiti na urais.
Kitendo kilichotokea leo ni kutumia vibaya fedha za umma na kwa vyovyote vile CCM ya mwanza haina ubavu wa kuitisha umati mkubwa watu kama ilivyokuwa leo, hivyo wakatumia mgongo wa ziara za kiserikali kufanya siasa. Jambo hili lazima tulikemee.
Ndio naondoka furahisha.
Njano5.
0784845394.