Kikwete VC mpya UDSM

kilichobaki sio kulalamika na kutoa maelezo ya jinsi ulivyoonewa bali tuanze kujipanga kupambana na serikali hii kandamizi. polisi hawana mbinu za kupambana bali wanatumia malalamishi yetu kuvimbisha vichwa vyao.
 
Kila mara ninapochangia humu nahimiza sana hasa vijana kufanya utafiti wa kina kabla ya kunena humu tusijelishana sumu kwaajili tu ya kufurahisha hisia au interest zetu.

Chuo kinaongozwa na kitu kinachoitwa CHARTER (Hati Idhini). Hii ndiyo kama katiba ya chuo na iko wazi kuwa haiko juu ya sheria za nchi. Ukihitaji nenda Kitivo cha sheria wakupe mistari ndugu. Student by-lwas ziko chini ya hii au zinatokana na hii nazo pia haziko juu ya sheria za nchi. Prospectus haizungumzii sheria za kuongoza chuo bali ni muongozo wa kitaaluma unaoonesha namna mitaala ilivyo, course contents and regulations na examination regulations.

Swala la Kikwete kuzomewa na swala la kufukuza wanafunzi nadhani hayaendani. Dr. Rwaitama ni mwalimu mzuri wa falsafa labda anaweza kutupa muongozo katika hili kutupa uhusiano kati ya matukio mawili.

Mukandala hachaguliwi na Ikulu ila na chuo tena senate. Hapa lazima tujue utaratibu unaopitiwa mpaka senate imkubali mtu. Acha kabisa. Ni sawa na mtu kuwa Prof au kupandishwa cheo katika ualimu wa chuo ni kazi wandugu.
 
Back
Top Bottom