Kikwete: Uvumilivu sasa basi...

Kikwete: Uvumilivu sasa basi...

kutoka ktk gazeti la nipashe nimeona Rais jk akijiuliza maswali yafuatayo.

"Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba," jk

sasa nimeamua kuyageuza maswali yake anayojiuliza na kuuliza unawezaje kuimarisha umoja wa nchi kwa kuamisha rasilimali za mkoa mmoja kupeleka mkoa mwingine?? kama ni kodi kwa ajili ya taifa kwani huwezi kuwatoza kodi ya rasilimali hapo walipo na kuzitumia kwingineko??

swali lake la pili sikuweza kufuatilia logic yake ni nini kwani anaonekana kama vile anajijibu yeye mwenyewe offcourse kahawa ya kilimanjaro inawafaidisha watu wa kilimanjaro. ndizi ya bukoba watu wa bukoba ndio waliolima ulitegemea watu wengine wanufaike na jasho la watu wengine so as ziwa victoria linavyowanufaisha waliolizingira huo ndio ukweli wenyewe. swali langu la msingi unapoamisha rasilimali moja kupeleka sehemu nyingine ya nchi unaimarisha umoja gani ?? umoja ndio limegeuka jawabu la maswali magumu ya wanakusini. its ridiculous

sera za majimbo ya chadema hiyo ndio inataka kugawanya nchi. nassari anataka kipande chake cha nchi, sugu nae, lema nae yaani hadi balaa
 
Mwaka 2013 umeanza kama mwendelezo wa matukio ya mwaka jana2012 yani kila siku tukio laajabu chakushangaza serikali nikiziwi feki na yuko na mponyaji anaulizwa unataka kusia kiwizi anajibu ndio, kwni husikii anajibu ndio, yaani jk hana washauri bali anashauri tumbo tu, kwn kuhusu gesi jibu liko wazi wamtwara wanadai wapewe nafasi yakujengewa viwanda kuwe na maendeleo, ajira nahuduma za kijamii zitapatikana kupitia wawekezaji hapa jk ni jazba ndio zinamfanya asijue point na hata hiyo jojo the fighter blog walitoa siri kwanini wachina watadumu tz has mtwara.......yani makubalionamyakifamilia na nchi ya china mmh tanzagiza hiii.

Sio jazba mkuu akiwaza 10% aliyokula ya wachina anachanganyikiwa kabisa mbaaba wa watu ,huku wanamtwara wanataka kumvua nguo
 
SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.



Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.

Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.

"Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha," alisema Rais Kikwete.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi waJamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.

"Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa inashughulikia mambo yakevizuri. Tunaomba mwendelee kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa Makuu," alisema Balozi Mpango.

Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.

Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo jana, habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende kwenye kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo akizomewa.

Hata hivyo, polisi walikiri wananchi kuweka magogo barabarani kwa lengo lakumzuia waziri huyo, lakini ikaeleza kuwa gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.

Akizungumza na Balozi Corner, Rais Kikwete alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kuwapotosha wananchi.

"Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa kutumia rasilimali zataifa," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

"Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

"Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala."

Source: Mwananchi
Anatoa maneno haya kisa ni Gas anataka aipeleke pwani ! Kwa nini hakusema haya Uamsho kule Zanibar walipokuwa wanachoma makanisa na wafuasi wa Shekh Ponde pale Mbagala .!!!?
 
Tatizo ni pale ambapo rasilimali zinapotoweka bila kumfaidisha yeyote..si kule zilikotoka wa taifa kwa ujumla...bali ni watu wachache tena ni walewale kila siku....
 
Katika kipindi cha uongozi wa Jk 90% ya nafasi za watumishi wakuu wa serikali ni Waislamu kwa Tanzania bara,100% Tanzania Zanzibar= Maaskofu.
 
Alipoingia madarakani mwaka 2005 alisema mwenyewe kuwa atamaliza kero zote za Muungano lakini jinsi muda unavyokwenda naona kero za Muungano zinazidi, taifa linazidi kuparaganyika na sasa zimeanza kero za Tanganyika. Mpaka 2015 tutaona kero nyingi sana zikiibuka na yote hayo yanasababishwa na aina ya uongozi uliopo aidha kwa kutojua ama kwa makusudi ili waendelee kujineemesha zaidi.
 
Tatizo ni pale ambapo rasilimali zinapotoweka bila kumfaidisha yeyote..si kule zilikotoka wa taifa kwa ujumla...bali ni watu wachache tena ni walewale kila siku....

... mkuu umenena.., asante kwa mchango wako mzuri.., hasa hilo ndilo tatizo kubwa kwa TZ. "ni walewale... Wana JK na familia yake"
 
Mleta mada umekaririshwa kukosoa,Jk yuko very right, kama ishu ni maendeleo wangezungumzia kupewa mrahaba wa gesi itayovunwa badala ya kulazimisha eti gesi ikichimbwa Mtwara watapata Ajira, kwan pamoja na wingi wa Viwanda vilivypo Dsm unaweza kuthubutu kusema vimewanufaisha wazaramo kiajira? Mnajua kuwa Mama Anna Abdala alipokuwa waziri wa Afya alijitahidi kupeleka NGO nyingi mtwara kuliko sehem nyingine yoyote hapa nchini lakini bado waliopata ajira ni watu wa maeneo mengine wenye sifa za ajira, Nani kakwambia gesi ikichimbwa mtwara Chale za usoni ndo itakuwa Qualification ya Ajira? Madini yanachimbwa shinyanga je kuna kitu cha kujivunia kwa wasukuma?. Kitu cha msingi ni uwepo wa uadilifu wa pesa itokanayo na gesi.
 
Kikwete huwa mara nyingi hajui anachosema. Kama kuna watu wenye hadhi tofauti kisheria kama akina Lowassa, Chenge na Rostam kwanini majimbo yasiwepo yenye turufu na yasiyo na turufu?
 
sera za majimbo ya chadema hiyo ndio inataka kugawanya nchi. nassari anataka kipande chake cha nchi, sugu nae, lema nae yaani hadi balaa

nchi imeshagawanyika mkuu unataka igawanyike mara ngapi ? kati ya walio nacho na wasio nacho ikiongozwa na jk mwenyewe jiulize kwanini ulipokuja mradi wa Bil. Bill Gates wa USA alimpeleka Bagamoyo na siyo Mtwara?? angalia
familia yake ni mabilionea lakini wewe anakupigia gitaa lake utaifa wakati anakula na familia yake. usisikilize maneno yao angalia vitendo vyao kama vinaashiria utaifa please let me know.
 
Miaka miwili iliyobaki inahitaji commanding/order nzito kama hii vinginevyo tutaendelea kulaumiana huko mambo yanaharibika.Binafsi nilitegemea kauli kama hii kutoka kwa mh. Rais,hii inadhihilisha jinsi gani raisi wetu anavyoweza kufanya maamuzi magumu yasiyo na chembe ya unafiki wala uoga kwa taiga.Nitoe rai kwa wale wote ambao wao suala la Gesi wanaona ni dili lao kisiasa,hili sio dili ni balaa kubwa wanatafuta maana kuna mambo mengi ya msingi wamesahau kuyafanya ikiwa ni pamoja na,1.Kujenga vyama vyao kimkakati kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.2.Kujenga uwezo wa ndani wa vyama vyao kukabiliana na mamluki wanaovivuruga vyama vyao.3.Kutanua wigo wa uongozi na matumizi ya fedha ndani ya vyama vyao.4.Kutafuta njia iliyo bora kuona jinsi gani vyama hivyo vinakuja na nguvu mpya ya kuungana na kupata chama kimoja chenye nguvu na ushawishi kwa wananchi tofauti ilivyo sasa.5.Kuacha kuwasumbua wananchi ambao maisha kwao bado yataendelea kuwa magumu tu hata kama Gesi hiyo itabaki kwao.6.Kuwatumia wataalamu walionao/ama kuwatumia wale waliopo katika masuala muhimu kama haya kwani kwa kufanya hivyo kutawapatia wataalamu wetu nafasi ya kutumia vibaji vyao kuwaeleza wananchi ukweli.7.Vyama kuondoa dhana potofu kwamba eti siasa ni kwa wanasiasa na si wataalamu,vyama vijenge tabia ya kufanya consultation kwa wataalamu kabla ya kutafuta nguvu ya umma.Vyama kwa kutokufanya hivyo navyo vitaonekana kama ni sehemu mojawapo ya dili la mtu/watu na si kwa maslai ya taifa.Chama bora ni kile tu amabacho msingi wake uko katika kujenga nchi hata kama ni polepole maana haraka haraka haina baraka.Napenda kuviomba vyama vya siasa na wadau wengine kuwa msingi mkuu wa Rasilimali za Taifa ni AMANI.AMANI Ikitoweka sidhani kama kuna yeyote kati yetu atakayethubutu kuzungumzia Rasilimali hizo akiwa Ukimbizini,mifano tunayo sema tu tunajisahaulisha kwa makusudi.La mwisho ni kuwaomba ndugu zangu tupende kumheshimu Rais wetu hata kama hatumpendi,lakini heshima ni kitu kikubwa sana na kama alikwisha kukosea msamehe tu na umuachie mwenyezi Mungu.Tofauti za vyama zisitufanye kukosa adabu kwa Mkuu kama huyu na kwa wale ambao wana tabia ya kumkebehi,kimdharau na kumsema hovyo bila sababu waache tabia hizo kila mtu na atimize wajibu wake.Asanteni.
Hivi kwa nini mnakazana kuona kuwa ili ni suala la vyama vya siasa badala ya suala la kitaifa lisilokuwa na usiasa. Hivi kweli hatuoni huu uwekezaji wa jinsi hii na Menejimenti ya jinsi hii ya raslimali zetu itatupa tabu baadaye.
Hatujajifunza yanayotokea kwingine duniani - mfano wa rahisi ni Nigeria, tumekuwa tunayasikia haya tangu miaka ya 70! Kwa nini tusishauriane na kupata sera nzuri zaidi badala ya hizo command/order nzito?
 
nchi imeshagawanyika mkuu unataka igawanyike mara ngapi ? kati ya walio nacho na wasio nacho ikiongozwa na jk mwenyewe jiulize kwanini ulipokuja mradi wa Bil. Bill Gates wa USA alimpeleka Bagamoyo na siyo Mtwara?? angalia
familia yake ni mabilionea lakini wewe anakupigia gitaa lake utaifa wakati anakula na familia yake. usisikilize maneno yao angalia vitendo vyao kama vinaashiria utaifa please let me know.
Urais ni suala la kifamilia.
 
Mleta mada umekaririshwa kukosoa,Jk yuko very right, kama ishu ni maendeleo wangezungumzia kupewa mrahaba wa gesi itayovunwa badala ya kulazimisha eti gesi ikichimbwa Mtwara watapata Ajira, kwan pamoja na wingi wa Viwanda vilivypo Dsm unaweza kuthubutu kusema vimewanufaisha wazaramo kiajira? Mnajua kuwa Mama Anna Abdala alipokuwa waziri wa Afya alijitahidi kupeleka NGO nyingi mtwara kuliko sehem nyingine yoyote hapa nchini lakini bado waliopata ajira ni watu wa maeneo mengine wenye sifa za ajira, Nani kakwambia gesi ikichimbwa mtwara Chale za usoni ndo itakuwa Qualification ya Ajira? Madini yanachimbwa shinyanga je kuna kitu cha kujivunia kwa wasukuma?. Kitu cha msingi ni uwepo wa uadilifu wa pesa itokanayo na gesi.

jawabu ni moja nalo ni sera mbaya za ccm ambazo zimetufikisha hapa tulipo kwa kuweka maslahi ya wawekezaji mbele kuliko watanzania wenyewe. kabla ya utekelezaji wa jambo lolote andaa kwanza mazingira yatakayowafanya watu wa eneo usika kufaidika na mradi kwa mfano ktk suala la gesi. toka gesi ivumbuliwe songosongo ni miaka 20 sasa kwanini mpaka hivi hatuna chuo cha oil and gas huko kusini ili kuandaa mafundi mchundo wa kuja kufanya kazi kwenye miradi hiyo. Lindi na Mtwara yako masekondari mengi andaa special program ya gas and oil kwy hizo sekondari za kuandaa vijana mazingira mazuri ya kuingia kwenye vyuo hivyo baadaye. unaposikia jk anawaambia watu wa mtwara wajiandae kufaidika na gesi bila kusema how ?? its a joke.
 
onyesha huo uoga na unafiki.
Mbona unaogopa sana suala la mjimbo kwani Tanzania ndo nchi pekee ambayo itakuwa inaendeshwa kimajimbo? kwani hakuna nchi zingine zenye majimbo? wapi ulisikia kuwa Lema anataka Arusha kama nchi? au wapi ulisikia Sugu anataka Mbeya kama nchi na hata kuyo Nassari aliwahi kutamka kuwa ikiwa hawajali watu wa meru basi tujue hatuna raisi na ijitenge hayo aliyazungumza kwa hasira baada ya kuona police ccm wanatumika kuua watu bila hatua kuchukuliwa. halafu hata vifo vingine vilivyo tokea vya utata hakuna ufuatiliaji! sas unaposema Oh sijui wanagawa nchi huo ni uafiki mkubwa
 
Aliyeanza kuigawa Nchi ni JK mwenyewe kwa kuendekeza uswahiba! Sasa hivi kila mtanzania anatamani kuandamana ili kutetea kilicho chake,Si ajabu kuona siku moja watu wa Chunya wakiandamana dhahabu ibaki kwao mpaka pale serikali itakapopeleka maji na barabara

Kwa hiyo JK aache kujiuliza maswali ya ajabu bali ajiulize,why uprising now? Kwa nini isiwe wakati wa Mwinyi au Mkapa? Why now? Majibu ni kwamba watanzania wamejitambua na wanataka haki zao! Ndio maana kuna mabango waliyokuwa waandamanaji yanasomeka Tanzania(Tanganyika) kwanza Mengine baadaye!
Pole sana Rais wangu,hiyo ndio hali halisi,.........!
 
Back
Top Bottom