Kikwete Usituletee Siasa za Kagame na Vitorie Ingabire

The Prophet

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
682
94
umeshindwa kuongoza. umefeli. umefulia. huna vision. unaongoza nchi kwa mtindo wa bora liende. Rais hujui hata unatakiwa ufanye nini na usifanye nini wakati gani na wapi. kwa kutokujua yote haya, sasa umeanza siasa chafu za jirani yako Kagame. siasa za kukandamiza wanaokupinga.

its too late bro. ndege isha paa hiyo.

jiulize upya. na kama ni ushauri wa kagame au museveni, nenda tena kawaambie 'dawa waliyokupa ni sumu'.

kaa. hesabu siku zako za kupanga magogoni kwa wema na amani. nchi hii siyo ya kikwete na mwema. nchi hii ni ya watanzania. na wala wewe na mwema wako hamuna ubavu wa kutuamulia chama, serikali au viongozi tunaowataka.

viongozi wetu wa upinzani tunawathamini na kuwaheshimu kuliko wewe. laiti kama ungejua hili bila shaka usingethubutu kuruhusu dola ya polisi kujiingiza kwenye siasa. maana mwisho wa siku wewe na shemeji yako mwenma mtaishia kwa Ocampo.

dunia inaona.

majira yanatika.

majira na nyakati havizuiliki mkuu. utafika wakati utakapojuta kuwahi kuwa rais wa tanzania.
 
No!acha kumkosoa utaambiwa wewe unamchukia kwa sababu ya uislam wake.
Nchi kwa mujibu wa waislam inasonga vizuri na kwa kasi kwa hiyo rais anaandamwa na wasio wa dini yake kwa sababu za kidini.
 
Unajua shida ya mkulu wa kaya ni moja.ana lack self confidence kitu kinachompa highly inferiority complex ukilinganisha na waliomtangulia.hali hii basi humfanya kuwa na aina flani ya ubabe na kutoshaurika.anyway tuone kama tutafika.
 
Kikwete ameshindwa kuingoza nchi anatumia mabavu kuiongoza bora hata Kagame nchini kwake amejitahidi kuzuia Ufisadi na anaijenga nchi, Huyu Kikwete anaihribu nchi yetu na kuitokomeza :madgrin:
 
Kikwete kwanini Tanzania unaitendea hivi?
Hivi unadhani utabaki hapo magogoni milele?
Umesha yapanda mengi mioyoni mwetu Udini ,Ukanda,Ukabila,Hadi umetudhairishia wapendwa wetu wenye ugonjwa hatari kua ni kiherehe chao ukaona haitoshi sasa umekuja na njia ya kutaka hata kutuulia watetezi wetu walio jitoa kwa moyo kututetea hivi unadhani utabaki salama?

Hivi ni kweli umeishiwa kabisa mbinu za kutukwamua na ugumu huu wa maisha unaotukabili waja wa mwenyezi Mungu?
kama ndivyo kwa nini usiwaachie wanaoweza na wewe ukaendelea kuheshimika kama mtu unaeitakia mema inji yako?
Na kama unaweza kutupatia tunayo yapigia kelele mbona unazidi kutumaliza tu huku mtaani?
Hivi mtanzania huyu aliyekuchagua na ukamuhaidi kua utampatia dawa,maji,barabara na kuilinda heshima yake leo unapo kuja kumletea mabomu,maji ya kuwasha na risasi za moto unadhani unapanda nioni ndani ya moyo wake?
Wanainji tumechoka na tunaona tayari kifo ni heshima kwetu na itafika wakati kina Ocampo watakuta tushachukua hatua inayo stahili kwako.
 
kashindwa kuongoza amejawa na chuki na ubinafsi wa hali ya juu..ni sawa sawa na mwananfunzi aliyeko kwenye mtihani maswali magumu hakuna anachoaandika na muda unakaribia kuisha ....hahaaaa JK urais sio kuchekacheka na kukutana na wageni ikulu
 
Back
Top Bottom