Kikwete tutakukumbuka kwa BVR

Kikwete tutakukumbuka kwa BVR

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,521
JK alifanya uamuzi sahihi wa kuruhusu uboreshaji wa daftari kwa mfumo wa BVR. Kuna wakati Kinana na Nape walisema hicho siyo kipaumbele lakini ulisimama kidete.

Uboreshaji huu umeleta mwamko na hamasa mpya ya kisiasa Tanzania, hili ni jambo kubwa hakika tutakukumbuka!!

Umehuisha fikra za kisiasa kwa watanzania japo wahafidhina ndani ya chama hawakupenda,

HONGERA!!
 
Mkuu sina uhakika kama hamasa ya watu ni kwa ajili ya kura au
kupata kitambulisho kwa ajili ya kurinyuu laini.

Yote kwa yote zoezi ni zuri
 
Mie nalaumu zoezi halikuanza mapema make kuna idadi kubwa ya watanzania wenye sifa hawakuandikishwa.
 
JK siku zote anakuwa kwenye ubora wa hali ya juu sana. Kila anachofanya anatengeneza historia. Kuanzia vitambulisho vya taifa, BVR, nk
 
Sema utamkumbuka jk usitusemee wengine BVR zenyewe hakuna maandalizi zoezi linaendeshwa kwa pupa hakuna wataalam na vifaa vya kutosha watu tumehangaika ktk foleni siku tatu ndo tuandikishwe
 
Hoja yako ya msingi sana. Ila JK kaweka historia

Ni kweli,historia ya kutuletea outdated BVR kits kwa bei kama mpya vile kumbe used kits.Kweli lazima tumkumbuke kwa ufisadi huu uliofanywa na watu wake wa karibu.
 
Najiuliza maswali ambayo sipati majibu kweli bvr ni historia lakini kwanini zilisubiri hadi miezi mitatu kabla ya uchaguzi?pili kwanini muda ulowekwa kujiandikisha ni siku saba?
 
Ukumbuke na zile fuso za mtumba toka kwa mwenyekiti zilizonunuliwa kwa bei kubwa zaidi ya mpya!!
 
JK siku zote anakuwa kwenye ubora wa hali ya juu sana. Kila anachofanya anatengeneza historia. Kuanzia vitambulisho vya taifa, BVR, nk

Lizabon hivyo vitambulisho mie ninavisikia tu.Hivi safari wako mkoa gani vile.Maana hata kuviona sijawahi kuviona.Labda viko kwa ajili ya wanaCCM tu.
 
Utanisamehe sijui ni Fuso zipi lakini ninachoongelea ni kile kinachomgusa mtanzania bila kujali Itikadi,dini,kabila au ukanda.

Pole kama nimekudissapoint.
 
Sema utamkumbuka jk usitusemee wengine BVR zenyewe hakuna maandalizi zoezi linaendeshwa kwa pupa hakuna wataalam na vifaa vya kutosha watu tumehangaika ktk foleni siku tatu ndo tuandikishwe

Wewe hata ukipiga kelele kiasi gani watu wote lazima waandikishwe licha ya mikwara! Vitambulisho ndo mpango mzima!
 
Lizabon hivyo vitambulisho mie ninavisikia tu.Hivi safari wako mkoa gani vile.Maana hata kuviona sijawahi kuviona.Labda viko kwa ajili ya wanaCCM tu.

Na matangazo yote yaliyokuwa yanavuma kwenye media na hapa JF!!Kweli ua not serious!
 
Najiuliza maswali ambayo sipati majibu kweli bvr ni historia lakini kwanini zilisubiri hadi miezi mitatu kabla ya uchaguzi?pili kwanini muda ulowekwa kujiandikisha ni siku saba?

Ili msijiandikishe kwa wingi.Na pili nia na lengo lilikuwa kwa wanaCCM nyie wengine hamkuwepo kwenye list ya wapigaji kura kwa mafisadi.
 
JK siku zote anakuwa kwenye ubora wa hali ya juu sana. Kila anachofanya anatengeneza historia. Kuanzia vitambulisho vya taifa, BVR, nk

Kuna vitambulisho vya taifa? Liziboni we unacho?

Hata katiba mpya kaleta jk
 
Last edited by a moderator:
mpaka.dakikahii ndotoya kupiga kura imetoweka daily natoka 12 kasor asubuhi narudi KUANZIA saa 1.30 KASORO WEEKEND NA HAPO NDOKILA MFANYAKAZ ATAKUWEPO KITUONI
 
JK siku zote anakuwa kwenye ubora wa hali ya juu sana. Kila anachofanya anatengeneza historia. Kuanzia vitambulisho vya taifa, BVR, nk
JK kila anachofanya anatengeneza historia, kuanzia kwenye bvr ya watu kuamuka saa sita usiku kwenda kwenye mkesha wa bvr, hadi rais aliyekaa angani kwa mda mrefu zaid Duniani.
 
Na matangazo yote yaliyokuwa yanavuma kwenye media na hapa JF!!Kweli ua not serious!

Rafiki mkoani kwetu havijafika.Mie naona hadithi tu.Mpaka sasa wameshaenda mikoa mingapi?Kijini kwetu bado havijafika
 
Back
Top Bottom