Jana usiku limetokea tukio baya la kuvamiwa na kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Ndugu Abdalom Kibanda.
Tukio hilo ambalo limesababisha sintofahamu kubwa miongoni mwa watanzania wanahabari, wapenda uwazi na ukweli na wale wenye kusimamia misingi ya Amani na utulivu katika nchi hii.
Aina ya tukio lenyewe na upekee wa utokeaji wake umegubikwa na utata mkubwa kiasi kwamba akili yangu ikanituma kutafakari kwa kina na kuyaandika haya, ikiwa ni miongoni mwa YAWEZEKANAYO kuwa ndiyo yaliyosababisha tukio ilo la kusikitisha kutokea kwa Mtanzania mwenzetu huyu kipenzi cha wanahabari.
a) 14th November 2012, Baada ya kuundwa kwa sekretarieti mpya ya chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Kibanda akiwa ni Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima ambalo linafahamika wazi kuwa ni chombo cha propaganda cha Chadema chini ya Mbowe, aliandika makala ambayo ilikuwa ikisifu safu hiyo mpya ya uongozi ya CCM,
huku akinukuu kauli mbalimbali za viongozi wa upinzani akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Znz, Mhe. Maalim Seif Sharif. Baada ya tukio hili wakuu wa gazeti hilo walimuita na kumuonya juu ya makala yake hiyo.
Lakini katibu Mkuu wa Chadema hakuishia na kuridhishwa kwa kuonywa kwa Kibanda bali alienda mbele zaidi na kumjibu
b) Lakini mara tu ya jibu hilo la Slaa kwa Kibanda, Mhariri huyo kwa ufundi mkubwa aliandika makala nyingine ambayo ilikuwa ikimsifu zaidi Katibu Mkuu mpya wa CCM, ndugu Abdulrahaman Kinana, ambae Slaa alimkosoa katika majibu yake dhidi ya Kibanda.
Baada ya Makala hiyo ya pili, ulizaliwa mgogoro wa haja ndani ya kampuni hiyo ya freemedia uliomuhusisha Kibanda na wamiliki wa kampuni na Chama kinacholitumia gazeti hilo. Mgogoro ambao ulipelekea Kibanda kuihama Freemedia na kuhamia katika New Habari Corporation ambayo kimsingi ni ya wadau wa Chama Cha Mapinduzi na kampuni ambayo kwa namna moja ama nyingine inaruhusu kuandikwa habari katika mandhari na tafsir ya HABARI bila propaganda wala upendeleo. Kwa maana nyingine ni kuwa Ndugu Kibanda alikuwa akihariri habari ambazo zinasema ukweli wa mazuri ya chama cha Mapinduzi na kuimwagia sifa kwa mipango yake ya kuiletea nchi Maendeleo lakini pia kwa kasi ya utekelezaji wa Ilani ya chama.
Baada ya Uamuzi huo wa Kibanda kuhamia New Habari Corporation na kuiandika habari zenye mlengwa wa Kati, wakuu wa Free media walimuita ili kufanya nae mazungumzo ya kumtaka kurejea katika kampuni yao, hasa baada ya Gazeti lao la Tanzania Daima kuanza kupoteza dira na kuandika habari ambazo hazina mvuto hivyo kulifanya kushuka kimauzo na kipropaganda dhidi ya Chama Cha Mapinduzi. Lakini Kibanda aliendelea kukataa kurudi na kuwa pamoja na viongozi hao wasiojua nini maana ya kuwa kiongozi, hawaheshimu taaluma wala hawataki kuruhusu fikra huru kuchukua nafasi katika chama na Kampuni zao. - with Sambala Ole Comrade and 16 others.
Wana jamvi
Yamesemwa mengi mema na mabaya kuhusu mimi Absalom Kibanda. Wengine tena wana habari na wakiwamo wahariri wenzangu, wakitumia kivuli cha majina bandia wakafikia hata hatua ya kutoa matusi ya wazi na kebehi juu yangu. Ni kweli nimeondoka Free Media Ltd na kujiunga na New Habari Corporation kwa mkataba mahususi. Wako waliosema ningeanza kazi Desemba Mosi na mwingine akazusha kwamba nilianza kazi Jumamosi iliyopita. Wote hao hawakuwa wakweli. Nimeanza kazi rasmi jana Jumatatu na nikatambulishwa leo Jumanne asubuhi.
Nimeondoka Tanzania Daima kwa heri na wala si kwa shari. Natambua na kuheshimu kwamba kila mmoja anao uhuru wake wa kutoa maoni kuhusu jambo lolote analoona linafaa. Namshukuru Mungu kwamba uamuzi wangu wa kuondoka Free Media umeibua hoja na mijadala mingi mikali. Sikujua kwamba naweza nikavuta hisia kwa wema au kwa ubaya kwa kiwango hicho. Sikupata kujua hata siku moja kwamba kupitia uhariri wangu, msimamo wangu katika baadhi ya mambo na pengine makala zangu niliweka alama katika maisha ya watu wengi ambao ama walikuwa wakiniunga mkono au walikuwa wakikerwa nami. Naamini nimetimiza wajibu wangu.
Nilijiunga Free Media Ltd si kwa sababu nilikuwa muumini, shabiki au mwana Chadema la hasha, bali nilifanya hivyo kwa sababu naamini katika mabadiliko ya kifikra na kimfumo. Nimekuja huku pia kwa sababu hizo hizo. Nilipokwenda Tanzania Daima mwaka 2006 nikitokea Mwananchi baadhi yenu mliniponda mkisema nimejiunga na kipeperushi cha Chadema. Nafurahi kwamba nimeondoka pale huku baadhi yenu mkiwa mashabiki wa kile mlichokiita kipepeushi. Zama hizo kwa wengi wenu Chadema ilionekana kuwa mwanasesere.
Leo Chadema kimekuwa chama makini cha upinzani na kwa kiwango kikubwa kazi hiyo ilichagizwa na maono ya Tanzania Daima nililokuwa nikiliongoza. Maono yetu ya kuchochea mabadiliko yaliijenga Chadema. Bado ningali ninayo maono yale yale ya mabadiliko. Ni wazi nina ajenda na maono binafsi katika mambo kadha wa kadha. Yote hayo yanapaswa kujengwa na kuaminiwa. Kazi hiyo nitaifanya nikiwa hapa New Habari Corp. Nikikwama nitaondoka kama nilivyoondoka Habari Corp (1999), Mwananchi (2006) na Tanzania Daima (2012).
Kama unataka kuwa MKWELI basi andika ukweli.Ni viongozi wangapi na muda kiasi gani wanutumia katika FB? Hivi operation Sangara,M4C zimefanyika mjini tu? Hivi Mwangosi aliuawa wapi,mjini au kijijini?Mitandao ya kijamii inaweza isisaidie sana, tunatakiwa tuende kuhamasisha wale watu waliopo vijiweni wasio na kazi na wale wananchi wa vijijini wasiokuwa na uhakika hata wa chakula. Hawa wa kwenye mitandao ya jamii wengi wao wanaandika humu wakiwa wameshiba na hata ukiwaambia kesho kuna maanandamano ni wachache sana watakaoshiriki, maana wengi wao wana kazi zao, au biashara zao ambazo zinawakeep busy.
Na hapa ndipo ambapo hata CHADEMA inakengeuka. Utakuta viongozi wao wamejaa tele kwenye facebook wakibadilisha status zao kila kuchapo, badala ya kwenda vijijini kuwaelewesha wale wananchi wenye njaa kwamba njaa yao inatokana na CCM, na kwamba njia ya kuiepuka ni kuikataa CCM. Vivyo hivyo, tunatakiwa tuchukue hatua kama hizo iwapo tunataka kuikataa serikali.
Binafsi naamini UWT wapo na wana uwezo kubwa wa kufanya kazi yao ila Uzalendo hawana na kwa kuwa system yote ni corrupt naamini wanaangalia zaidi maslahi yao na si UTAIFA tena.Wameingiliwa na wanasiasa na kama utakumbuka miaka ya nyuma katika uteuzi wa mkuu wao wa sasa kuna watu walilalamika kuwa kateuliwa ki ushkaji zaidi kuliko kiutendaji.Hivi kuna ushahidi gani thabiti zaidi ya ule anaotoa mhanga wa tukio? ww unatumia akili kuandika haya uliyoweka hapa? Dk Uli alitaja majina, simu za wahusika zinajulikana, hao mbwa unaowatetea nini walichofanya hadi leo, ni ajabu na kuudhi sana hawa washennzi wanaoishi kwa kodi zetu kazi yao imebaki moja tu kutetea upumbavu na kulinda chama cha siasa, tutaona mwisho wenu endelea kujidanganya na miwani yako ya mbao, hatuna usalama wa taifa nchi hii this is a dead weight organ we are carrying!
Nawalaumu sana Dr Mwakyembe na Dr ulimboka ,kwani hawa ni waathirika walituahidi kuwataja wahusika pindi watakapo toka kwenye matibabu.Ukimya wao ndio unatumaliza.
Ukila nyama ya mtu huachi.J.K.Nyerere.
Alivyohojiwa na BBC ni wazi walomvamia wanaweza kuwa ni maafande
Tukiendelea kumwita VAsco da Gama Dhaifu, tunamjengea kinga kwenye matukio kama haya.Hii ndiyo style yake ya utawala.kwa hili la kutesa wana harakati, ndiyo uhodari alionao, na sio dhaifu kwenye hili.thank you very much, its a good analytical piece of work. Kwa kweli nchi yangu pendwa ya Tanzania iko na ombwe kubwa la uongozi this time more ever.
Kwa kifupi udhaifu wa JK.
Tukiendelea kumwita VAsco da Gama Dhaifu, tunamjengea kinga kwenye matukio kama haya.Hii ndiyo style yake ya utawala.kwa hili la kutesa wana harakati, ndiyo uhodari alionao, na sio dhaifu kwenye hili.
good analysis
nakupongeza kwa mwono wako usi na shaka
nami nakutunuku uandishi bora unafaa kuwa mchambuzi wa habari katika media zetu
Wanaopaswa kuchunguzwa sikiliza maneno yao, wakishirikiana na kina Pasco wa JF.
Nape Nnauye
Hili la kutekwa na kupigwa na kuumizwa kiasi hichi kaka yangu Kibanda, kila nikilitafakari maneno ya waliosema hakutatawalika na makala za Kibanda mbili au tatu za mwisho kabla ya kuhama chombo cha habari kabla ya anachofanyia kazi sasa vinajirudia kichwani mwangu sana! Get well soon brother!