Kikwete, Serikali ichunguzwe suala la Absalom Kibanda!

Kweli magamba hamnazo; kwani mlivyo mteka na kumtesa Dk. Ulimboka ilikuwa ni faida kwa nani? Mkuu usitufanye wote ni UAMUSHO.

......

Tatizo lenu ni uvivu wa kufikiri.na mvivu wa kufikiri huwa ni mtumwa wa mawazo ya wengine na hii ni silka ya mva mwagwanda yeyote.hutegemea aliye juu yake na ndio maana huitana kamnda.
 
thank you very much, its a good analytical piece of work. Kwa kweli nchi yangu pendwa ya Tanzania iko na ombwe kubwa la uongozi this time more ever.

Kwa kifupi udhaifu wa JK.

......

I am crying for my beloved country that it has gone to the dogs!!
 
Umefunguka poa KAMANDA,mipini sio mipini,misumari sio misumari,imesimama vyema na ukipita inachoma panapostahil.OLE WAO HAWA WANAKUSOMA HAPA NA KUJIFANYA HAWAELEWI YA KWAMBA WATU WANATESEKA NA KUDHALILISHWA NA UTAWALA HUU HARAM,DHALIM NA WA KIDIKTETA WAJA NA VIHOJA VYAO DHAIFU VISIVYOJAA KIGANJA KWA DHAMIRA YA KUWALAMBA MIGUU WATAWALA WALIOJAWA DAMU HADI KWENYE VIGANJA VYAO VYA SALAM NA KULIA CHAKULA CHA DHULMA KWANI SIKU ZAO ZAHESABIKA***Watalia na kusaga meno huku watu wakishangilia bila huruma.

Hasira au?
 
@Lubua Mkuu umeongea vizuri, lakini pia ukweli utabaki pale pale kuwa Mazingira ya matukio yote uliyoyataja yamekuwa yakigubikwa na hisia mbalimbali. Nikianza na tukio la MWANGOSI, ikumbukwe kwamba huyu alikuwa ni rafiki wa karibu sana na mwanahabari ambaye ni mnazi mkubwa wa chama cha CHADEMA, sina sababu ya kutomtaja huyu si mwingine bali ni TUMAINI MAKENE, kama utaliangalia tukio hili kwa undani utapata picha kuwa mbali na kuaminishwa kuwa Mwangozi alikuwa katika shughuli za habari, lakini mazingira yanaonesha kuwa yawezekana alikuwa akitekeleza shughuli za chama chake cha CHADEMA, nasema hivyo kwa sababu hakuwepo yeye peke yake mwanahabari, kwa nini yeye tu ndo akumbwe na mkasa huo?

Katika tukio la kutekwa, kuteswa na hatimaye kutelekezwa kwa ULIMBOKA, wewe unaangalia upande mmoja kuwa ni serikali ndiyo iliyolaumiwa, unasahau kuwa mengi yalisemwa katika tukio hili, wapo waliosema alitekwa na ndugu wa wagonjwa waliokuwa wakiathirika kutokana na mgomo ule, wengine wakasema aliwasaliti wenzake ambao alikuwa akifuatana nao kutafuta suluhu dhidi ya serikali, kuna waliokwenda mbali na kusema alikuwa na mahusiano na mke wa kigogo mmoja, mazingira yote haya huwezi kkuyabeza na kuusuta upande mmoja ambao ni serikali eti kwa sababu tu mnatetea chama fulani, wananchi wanaona na wanaujua ukweli. Katika tukio la ABSOM KIBANDA, hata mtoto mdogo anajua kuwa huyu bwana hakutoka Tanzania DAIMA kwa amani, na kwa maana hiyo lazima aliondoka huku akiwa anajua siri nyingi hasa ukizingatia kuwa alikuwa akiandikia gazeti la chama, unafikiri wanaimani naye na uwezo wake wa kutotoa siri zao?

Tuache kuchonganisha serikali na wananchi katika mambo ya kudhania, wanahabari ni watu wanaoheshimika duniani kote , kuanza kukurupuka na maneno ambayo yanaweza kulitumbukiza taifa katika korongo kama ambavyo umesema siyo vizuri hata kidogo. Tuache Polisi wafanye kazi zao, Suala la kusema majambazi gani hawachukui kitu ni mawazo potofu, utambue ujambazi siyo lazima utumie nguvu hata mhanga mwenyewe anaweza kuwa jambazi na kuzulumu wenzake hata kwa njia ya kalamu na hivyo wenzake wakahitaji roho yake tu na siyo pesa kama tunavyodhania.

siji unatenga vipi mateso ya ulimboka na ushiriki wa serikali, tumia akili, hakunaasiyejua kilicho kuwa kina endelea ukitaka muume kova sikio atakupasha
 
Watanzania wenzangu,

Tumeshashughudia utekwaji wa watu kadhaa mara kwa mara. Tumeshashuhudia matukio mbalimbali ya ajabu, ambayo hata hivyo yalifanywa kwa namna ya kuwasingizia majambazi.

Leo, tunamwona tena Mwanahabari mahiri, Absalom Kibanda, akipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, si ya ugonjwa, bali ya kipigo kutoka kwa watu wasiofahamika, watu waitwao majambazi.

Hili linatokea muda wa miezi takribani minne baada ya Mnaku Mbani, Mhariri wa gazeti la Business Times kupigwa risasi mdomoni na kupoteza meno matatu.

Hili linakuja baada ya Mwandishi mwingine wa Tanzania Daima, Shaaban Mtutu kupigwa risasi na Polisi eti akidhaniwa ni jambazi. Huyu alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake mnamo tarehe 4 Disemba, 2012, eti polisi walimdhania ni jambazi, AKIWA NYUMBANI KWAKE.

Tukio la Kibanda, linatokea ikiwa ni miezi michache tangu Mwangosi Daudi, mwandishi wa Channel Ten kuuawa na jeshi la polisi tarehe 2 Septemba 2012.

Hili linakuja miaka michache baada ya mapema mwaka 2008 Saed Kubenea, Mkurugenzi wa kampuni ichapayo gazeti la Mwanahalisi (ambalo nalo limefungiwa), kumwagiwa tindikali machoni pamoja na Mhariri Mshauri wa gazeti hilo Ndimara Tegambwage kucharangwa kwa mapanga.

Linatokea miezi michache baada ya Dk. Ulimboka kutekwa na kupigwa nusu kifo, na kutupiwa msitu wa Mabwepande. Haya yote yanatokea Tanzania, na asilimia kubwa ya haya yote yamehusishwa na ujambazi.

Huwa najiuliza, ujambazi ni nini? Kwa nini hao majambazi hawaibi chochote zaidi ya kuwajeruhi na kunuia kuwaua hawa makamanda? Kwa nini wawavamie tu watu wenye kuikosoa serikali?

Hao majambazi kwa nini hawapatikani? Ikiwa juzi tu ameuawa kwa risasi Padre kule Zanzibar, na serikali imewaleta FBI kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo, kwa nini serikali isione haja ya kuwatumia FBI na taasisi nyingine za ukachero kutoka mataifa yaliyoendelea ili tuwapate hawa wahalifu wawavamiao wanahabari na wanaharakati wetu? Watanzania, tutanyamaza hadi lini ikiwa sauti zetu zinanyamazishwa?

Bwana Kibanda, hadi sasa, ana kesi mahakamani. Kesi ya uchochezi baada ya gazeti la Tanzania Daima (Wakati Kibanda akiwa Mhariri) kuchapa makala iliyoandikwa na Mwandishi na Mwanaharakati Samson Mwigamba. Kesi hii ingali ikisikilizwa, leo tunasikia kuwa amevamiwa na majambazi! Kweli? Latuingia akilini kweli? Latushawishi hili kweli?

Tanzania, serikali imetengeneza mtandao wa Kimafia (kama alivyoeleza Mh. Joseph Mbilinyi Bungeni Mwaka jana). Kumekuwa na mtandao wa kimafia unaowawinda makamanda, wanaharakati.

Habari/tetesi zilishawekwa wazi kuwa kuna kundi la watu limeundwa, linalojishughulisha na utekaji, utesaji, na uuaji wa watu wenye ushawishi katika jamii, wanaoikosoa serikali kwa uwazi. Yamkini kundi hili ndilo lililoripotiwa kuwafuatilia Mh. John Myinka, Mh. Godbless Lema, na Mh. Dk. Wilbroad Slaa.

Yamkini hilo ndilo kundi lililomwekea sumu Mwanaharakati mwingine Dk. Harryson Mwakyembe. Hili ndilo kundi lililoripotiwa kufuatilia maisha ya Mh. Samwel Sitta. Hili ndilo kundi, ndilo hasa!

Kundi hili la kimafia limeamua kuwanyamazisha Watanzania, na kuiacha serikali iendelee kutuibia, kutunyonya na kutufanya mafukara.

Kundi hili limenuia kuifanya serikali iendelee kutawala na kujinawirisha. Vigogo wa serikali na watoto wao waendelee kufurahia nchi, kwa kodi zetu wananchi.

Kundi hili limenuia kuhakikisha viongozi waovu na wabadhirifu wa mali za umma wanaendelea kututawala kwa mabavu, kwa matisho na kwa dhuluma.

Kwa mtindo huu, lazima tuhoji waziwazi kuwa kwa nini watu hawa hawakamatwi na kutiwa nguvuni, iwapo kweli serikali haina uhusiano nao?

Si ndio hawa wafanyao kazi kama Ramadhani Ighondu? Hapa tusidanganyane, serikali inawafahamu watu wote wa kundi hili... Serikali inafahamu A hadi Z ya kundi hili, na yamkini serikali ndiyo iliyowapa kazi hii maalum.

Kufunika kombe ili mwanaharamu apite, tunaiona serikali ikienda kuwajulia hali wahanga wa uonevu huu. Serikali inamtuma Makamu wa Rais kwenda kumtazama Kibanda hospitalini, Rais Kikwete pia alikwenda kumjulia hali Saed Kubenea... Yote haya ni kujaribu kutudanganya (elude) kuwa hawajui kiendeleacho..

Serikali inafahamu kundi lake hili la kimafia. Kundi la uovu, inalifahamu vyema..

Sasa, kwa nini serikali ifanye hivi? Kwa nini wanaharakati wateswe, wakamatwe, wauawe? Ukweli wenyewe ndio huu:

Lengo kuu la serikali, ni kunyamazisha sauti zote zinazoikosoa bila kujali sauti hizo zinatokea wapi. Serikali inahitaji kunyamazisha sauti za watu binafsi, inahitaji kunyamazisha sauti za vikundi, vyama au jumuiya zinazoikosoa.

Sasa kwa sababu tasnia ya habari huwafikia wengi, na kwa sababu watu wengi huamini habari za vyombo vya habari, serikali imenuia kuinyamazisha kabisa tasnia ya habari kwa kushughulika na wakosoaji wakubwa katika vyombo vya habari.

Ndio maana hata waandishi wa makala kama hizi wanatafutiwa visa hata vya kufungwa gerezani. Mfano mzuri wa hili ni kesi ambayo inaendelea mahakamani dhidi ya Kibanda mwenyewe, na Samson Mwigamba, eti kwa sababu ya makala iliyochapwa kwenye gazeti la Tanzania Daima.

Pengine wengi wetu mnamkumbuka Sam Shollei. Huyu alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, kabla ya Tido Mhando wa sasa.

Huyu si Mtanzania bali ni Mkenya. Shollei aliibadilisha taswira ya gaeti la Mwananchi na kulifikisha katika taswira lililokuwa nayo sasa.

Alifanya kazi kubwa sana. Lakini, mwisho wake alinyimwa kibali cha kuendelea kufanya kazi nchini Tanzania baada ya kibali chake cha awali kwisha muda.

Serikali, kupitia uhamiaji, ilimnyima Shollei kibali bila kuweka bayana sababu za kufanya hivyo. Zitto Kabwe alipiga kelele kidogo kuikosoa serikali kwa swala hilo lakini kelele zake hazikufua dafu.

Shollei, aliyelipa gazeti la Mwananchi umaarufu mkubwa na maendeleo makubwa akalazimika kuacha kazi.

Baada ya Shollei kulazimika kuondoka Tanzania, nafasi yake ikachukuliwa na Tido Mhando. Hapa tukumbuke kuwa, Tido Mhando alifuatwa na Rais Kikwete London mwaka 2007, akiwa Mkurugenzi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, na Kikwete akamwomba aje aiongoze TBC.

Hata hivyo naye alipoiongoza TBC na kuwa chombo cha uwazi na ukweli, na pale aliporuhusu kuonyeshwa kwa mikutano ya kampezi ya vyama vyote vya siasa katika uchaguzi Mkuu wa 2010, bila upendeleo, Tido alinyimwa mkataba mpya mwaka 2011.

Tido, akiwa amebadilisha taswira ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), akanyimwa mkataba wa kuendelea kuiongoza. Sasa ni nani asiyejua kuwa TBC imeshapoteza ule umahiri wake ambao Tido aliisaidia kuwa nao? TBC sasa imerejea ilipotoka, imeanza kulichungulia kaburi tena...

Baada ya Tido kunyimwa mkataba na serikali, licha ya kwamba watu wengi walilaumu sana, Tido akachukuliwa na Mwananchi, kuziba nafasi ya Shollei.

Sasa, pengine kwa weledi wa Absalom Kibanda, kwa kazi ambayo ameifanya tangu akiwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, naye ameanza kutafutwa roho yake na hao wanaoitwa "majambazi". Majambazi wasioiba chochote, majambazi watafutao roho za wanahabari mahiri na wanaharakati.

Nirudie tena, lengo la serikali ni kuifunga mdomo tasnia ya habari Tanzania. Lengo lake ni kuwa na vyombo vya habari kama Radio Uhuru na Gazeti la Mzalendo ambayo kazi yao ni kuitukuza serikali ya CCM hata pale pasipostahili.

Lengo la serikali, ni kuwanyamazisha makamanda wote waonekanao kuikosoa serikali kwa uwazi. Na hili linaonekana kufanikiwa kwa kiasi fulani.. Kwani gazeti la Mwanahalisi liko wapi leo? Mwangosi yuko wapi? Kubenea anasikika tena? Je ulimboka mmemsikia tena? Wote hawa wameshanyamazishwa kwa kiasi fualani, sauti zao zimefifia.

Watanzania wenzangu, Tanzania ya sasa si mahala salama kwa Wanahabari makini, na wanaharakati. Nawaomba na kuwasihi tuwe macho na tuamke tuungane na wenzetu hawa waliojitoa mhanga.

Tusimameni imara kuitetea nchi yetu, haijalishi watuue sote. Kwa hakika, tusiposimama imara, nchi hii tutaitumbukiza korongoni.

Tupazeni sauti zetu pale tuwapo na nafasi. Kwa wale tusioweza kuchapa makala kwenye magazeti mbalimbali, mitandao ya kijamii ndio silaha yetu iliyosalia.

Tusiandike jumbe za mapenzi kwenye kuta zetu za Facebook, Tiwitter, blogu zetu. Tuandikeni jumbe za kutafuta haki na usawa nchini.

Tuandikeni jumbe za kuikosoa serikali na kuilalamikia kila uchwao uchao. Tusiishie hapo; tuwaamsheni Watanzia wenzetu; tuwaamsheni waliolala... Tuwaelezeni kumepambazuka.... Tusipofanya hivyo, tutakapoacha kazi hii mikononi mwa wenzetu wachache, kwa hakika tutashiriki kiliangamiza taifa letu. Mwisho tutalia na kusaga meno.

View attachment 85800View attachment 85801View attachment 85807View attachment 85803View attachment 85804

View attachment 85805View attachment 85812

Mimi napingana na wewe. Dawa ni moja tu. ACTION! Kama ni kelele zilishapigwa sana. Bila watanzania kuingia mitaani kwa umoja bila kujali dini, kazi, siasa au jinsia serikali haitasikia. Tuingie mitaani tudai haki kwani serikali imeshindwa kutulinda. Maalbino wanauawa, Waandishi wanauawa, wananchi wa kawaida wanauawa tena bila sababu. Na wako wanaopokea mshahara na wamepewa magari mazuri, majumba makubwa na kila kitu ili kutimiza jukumu la kutulinda lakini hawataki. Sasa unataka kuniambiwa mtu kama huyu waziri wa mambo ya ndani ana faida gani kwa Tanzania. Mkuu wa polisi ana faida gani. Usalama wa taifa una faida gani. Kama mnafikiri maneno yatasaidia basi endeleeni!
 
@Lubua Mkuu umeongea vizuri, lakini pia ukweli utabaki pale pale kuwa Mazingira ya matukio yote uliyoyataja yamekuwa yakigubikwa na hisia mbalimbali. Nikianza na tukio la MWANGOSI, ikumbukwe kwamba huyu alikuwa ni rafiki wa karibu sana na mwanahabari ambaye ni mnazi mkubwa wa chama cha CHADEMA, sina sababu ya kutomtaja huyu si mwingine bali ni TUMAINI MAKENE, kama utaliangalia tukio hili kwa undani utapata picha kuwa mbali na kuaminishwa kuwa Mwangozi alikuwa katika shughuli za habari, lakini mazingira yanaonesha kuwa yawezekana alikuwa akitekeleza shughuli za chama chake cha CHADEMA, nasema hivyo kwa sababu hakuwepo yeye peke yake mwanahabari, kwa nini yeye tu ndo akumbwe na mkasa huo?

Katika tukio la kutekwa, kuteswa na hatimaye kutelekezwa kwa ULIMBOKA, wewe unaangalia upande mmoja kuwa ni serikali ndiyo iliyolaumiwa, unasahau kuwa mengi yalisemwa katika tukio hili, wapo waliosema alitekwa na ndugu wa wagonjwa waliokuwa wakiathirika kutokana na mgomo ule, wengine wakasema aliwasaliti wenzake ambao alikuwa akifuatana nao kutafuta suluhu dhidi ya serikali, kuna waliokwenda mbali na kusema alikuwa na mahusiano na mke wa kigogo mmoja, mazingira yote haya huwezi kkuyabeza na kuusuta upande mmoja ambao ni serikali eti kwa sababu tu mnatetea chama fulani, wananchi wanaona na wanaujua ukweli. Katika tukio la ABSOM KIBANDA, hata mtoto mdogo anajua kuwa huyu bwana hakutoka Tanzania DAIMA kwa amani, na kwa maana hiyo lazima aliondoka huku akiwa anajua siri nyingi hasa ukizingatia kuwa alikuwa akiandikia gazeti la chama, unafikiri wanaimani naye na uwezo wake wa kutotoa siri zao?

Tuache kuchonganisha serikali na wananchi katika mambo ya kudhania, wanahabari ni watu wanaoheshimika duniani kote , kuanza kukurupuka na maneno ambayo yanaweza kulitumbukiza taifa katika korongo kama ambavyo umesema siyo vizuri hata kidogo. Tuache Polisi wafanye kazi zao, Suala la kusema majambazi gani hawachukui kitu ni mawazo potofu, utambue ujambazi siyo lazima utumie nguvu hata mhanga mwenyewe anaweza kuwa jambazi na kuzulumu wenzake hata kwa njia ya kalamu na hivyo wenzake wakahitaji roho yake tu na siyo pesa kama tunavyodhania.

wewe ni kilaza mwingine TUKIO la MWANGOSI na Dr ULIMBOKA serikali imechukua hatua gani ........! kusema taarifa za kifo cha mwangosi NI SIRI,Na ISSUE ya Dr ULIMBOKA kushikwa MKENYA hayo yoote huja yaona? mbona serikali imekataa kuuunda tume huru kuchunguza issue ya ulimboka? gwaride la utambuzi,ighondu katajwa na mjeruhiwa kashikwa?, ACHA U-KILALAVI,utatumwa na magamba mpaka lini? upo sawa lakini KICHWANI au una tundu mahali?
 
mengi tutasema lakini ukweli unabaki pale pale kwamba kibanda na wengine waliotendwa kama yeye ni ujambazi mpya ulioibuka kwa wanahabari na wanaharakati na bila kuwa na mshikamano ipo siku makamanda wapambanaji wote wataumizwa sana,
 
Unashangaa Kibanda kuhusishwa na cdm? unakaa wapi ww? Alipoondoka gazeti la Tanzania Daima ambalo hata ukitoa POVU Lubua ni la cdm indirect na unajua hivyo pamoja na Cdm wenzio, alishambuliwa na wana-cdm humu ndani kwamba kanunuliwa na magamba , tatizo kaamia gazeti la Azizi ambye ni CCM.

Sasa hivi unangaka ukisema TZ-Daima si cdm au isemwe kuwa New Hbari alikoamia Kibanda ni CCM? Kweli ukweli unauma.

Kubali tu kwani hata ww ulikuwa ni mmoja wa cdm aliyemshambulia Kibanda alipoama TD. Hivi Kibanda alikuwa na kadi ys Cdm?

Kama hakuwa nayo kwanini mmfuate kihivi. Na hata kama alikuwa nayo hivi cdm ni mama yake? Je ww cdm ni mama yako? Punguza povu hilo basi napumua taratibu
 
One of the best and well written,well done Mr Lubua...i must confess ni miaka mingi imepita sijawahi kuona analysis nzuri kama hii kwa lugha ya Kiswahili!
 
Unashangaa Kibanda kuhusishwa na cdm? unakaa wapi ww? Alipoondoka gazeti la Tanzania Daima ambalo hata ukitoa POVU Lubua ni la cdm indirect na unajua hivyo pamoja na Cdm wenzio, alishambuliwa na wana-cdm humu ndani kwamba kanunuliwa na magamba , tatizo kaamia gazeti la Azizi ambye ni CCM.

Sasa hivi unangaka ukisema TZ-Daima si cdm au isemwe kuwa New Hbari alikoamia Kibanda ni CCM? Kweli ukweli unauma.

Kubali tu kwani hata ww ulikuwa ni mmoja wa cdm aliyemshambulia Kibanda alipoama TD. Hivi Kibanda alikuwa na kadi ys Cdm?

Kama hakuwa nayo kwanini mmfuate kihivi. Na hata kama alikuwa nayo hivi cdm ni mama yake? Je ww cdm ni mama yako? Punguza povu hilo basi napumua taratibu

Tatizo sio Kibanda tuu ni wengi wameshakufa na kujeruhiwa,na wanaoumizwa wengi wao ni wanaharakati au waandishi wa habari na mbaya zaidi hao majambazi or sijui mafia mbona hawakamatwi na kila siku ni usanii tuu na sababu kibao kutoka kwa polisi na serikali....wewe endelea kutetea huu upuuzi lakini kumbuka siku na wewe au ndugu yako ukionekana threat kwao watatumia the same style kukunyamazisha.
 
mengi tutasema lakini ukweli unabaki pale pale kwamba kibanda na wengine waliotendwa kama yeye ni ujambazi mpya ulioibuka kwa wanahabari na wanaharakati na bila kuwa na mshikamano ipo siku makamanda wapambanaji wote wataumizwa sana,

Very well said! Nafikiri kwa wengi mpaka ipige "close to home ndio wataamka usingizini". Ni afadhali tulishughulikiea kwa vitendo hili swala sasa kabla haijawa too late!
 
Mimi napingana na wewe. Dawa ni moja tu. ACTION! Kama ni kelele zilishapigwa sana. Bila watanzania kuingia mitaani kwa umoja bila kujali dini, kazi, siasa au jinsia serikali haitasikia. Tuingie mitaani tudai haki kwani serikali imeshindwa kutulinda. Maalbino wanauawa, Waandishi wanauawa, wananchi wa kawaida wanauawa tena bila sababu. Na wako wanaopokea mshahara na wamepewa magari mazuri, majumba makubwa na kila kitu ili kutimiza jukumu la kutulinda lakini hawataki. Sasa unataka kuniambiwa mtu kama huyu waziri wa mambo ya ndani ana faida gani kwa Tanzania. Mkuu wa polisi ana faida gani. Usalama wa taifa una faida gani. Kama mnafikiri maneno yatasaidia basi endeleeni!

Nduguye hao wote uliowataja, wana faida, si kwetu wananchi bali kwa serikali. Kwa ujumla, hao ndio watekelezaji wakuu wa wa utekaji, utesaji, na uuaji? Hiyo ndiyo kazi yao, hayo ndiyo majukumu yao waliyopewa na bosi wao.
 
Unashangaa Kibanda kuhusishwa na cdm? unakaa wapi ww? Alipoondoka gazeti la Tanzania Daima ambalo hata ukitoa POVU Lubua ni la cdm indirect na unajua hivyo pamoja na Cdm wenzio, alishambuliwa na wana-cdm humu ndani kwamba kanunuliwa na magamba , tatizo kaamia gazeti la Azizi ambye ni CCM.

Sasa hivi unangaka ukisema TZ-Daima si cdm au isemwe kuwa New Hbari alikoamia Kibanda ni CCM? Kweli ukweli unauma.

Kubali tu kwani hata ww ulikuwa ni mmoja wa cdm aliyemshambulia Kibanda alipoama TD. Hivi Kibanda alikuwa na kadi ys Cdm?

Kama hakuwa nayo kwanini mmfuate kihivi. Na hata kama alikuwa nayo hivi cdm ni mama yake? Je ww cdm ni mama yako? Punguza povu hilo basi napumua taratibu

Hivi kuna kitu gani nimeongea kwenye makala yangu hiyo kinachohusiana na Chadema? Kwa nini unadhani mimi ni Chadema kwa kuandika ukweli? Yawezekana wanaotetea ukweli wote utawaita Chadema. Gazeti la Tanzania Daima si la Chadema, japokuwa linamilikiwa na mtu mwenye uhusiano na Chadema. Magazeti ya Rai, Mtanzania si ya CCM, japokuwa yanamilikiwa na mtu mwenye uhusiano na CCM.

Unaposema mimi niliwahi kumshambulia Kibanda alipohamia New Habari Corporation, je waweza kutoa ushahidi wa komenti moja tu ambayo niliandika katika uzi wowote kuhusiana na kuhama kwa Kibanda? Je wewe walifahamu tamko la Kibanda, alilolitoa hapa JF baada ya kuhamia New Habari? Tamko hilo alilitoa tarehe 18 Disemba 2012, saa 2:49 (saa mbili) usiku. Hili tamko umewahi kulisoma au unakurupuka tu? Je umesikia mahojiano yake na vyombo vya habari baada ya kupigwa kwake na kuteswa? Aliwataja watesi wake kama walisemaje?

Hata hivyo, ni vyema ujue kuwa, Absalom Kibanda ana kesi ya kujibu Mahakamani mpaka leo, kama nilivyoainisha katika makala yangu. Kesi hiyo si kwa kazi aliyoifanya akiwa na hilo gazeti uliitalo la CCM, bali kazi aliyoifanya akiwa bado yu Tanzania Daima. Je Chadema ndio waliomfungulia kesi ile?

Jifunze kuwa mchunguzi ndugu yangu, usikurupuke katika kutoa hoja. Ulimwengu wa sasa ni wa watu wawezao kuchambua hoja na kuchambua pumba na mchele. Wewe pia nakufananisha na wale wengine wanaotumia miamvuli ya wavu kujikinga na mvua, au wapandao kwenye mti kumkimbia chui... Mtaloweshwa tu na mvua, mtaliwa na chui!!
 
Back
Top Bottom