Kikwete ni rais bora zaidi ya wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ni rais bora zaidi ya wote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MTENDAHAKI, Jun 1, 2011.

 1. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,993
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Sina shaka kuwa kuna watu wasiopenda kukubali ukweli watakanipinga kwa kejeli na mbwembwe lakini hilo lakini ni bora kilicho gizani kikamulikwa ili kionekane!

  Ni ukweli usiopingika kuwa serikali ya ya JK imechafuliwa na kashfa nyingi mbaya ambazo sina malengo ya kuzirudia na wala sitomjibia hizo. Lakini kama mwananchi mwema na msema kweli nakiri kuwa NIMEIONA NDANI YA JK DHAMIRA YA DHATI YA KUMSAIDIA MWANANCHI WA HALI YA CHINI NA HASA MKULIMA!

  Pamoja na ushabiki wangu kwa CHADEMA,nimesikitishwa na vipaumbele vyao katika bajeti mbadala kwani ''KILIMO SIO KIPAUMBELE CHAO''.

  Kwa hili nimeona na nimetambua kwanini CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu,chakusikitisha hata AFYA za wananchi nazo sio muhimu kwa kwa waandaji wa bajeti mbadala. Hili limenifanya niamini kuwa kambi ya upinzani ilyopita ilyokuwa na mchanganyiko wa vyama vyote vya upinzani ilitufaa sana kuliko hii ya chama kimoja.

  Kitendo cha JK kuongeza bajeti ya umwagiliaji mpaka kufikia bilioni 40 kimeonyesha dhamira yake ya kumhakikishia mkulima anavuna na kuondokana na njaa halafu umaskini. Kwa nchi ambayo asilimia 80 ya wananchi wake ni wakulima huwezi kuondoa kilimo kama kipaumbele, huu kwangu ni ujuha!

  Ninawataka waliondaa bajeti hii mbadala warudi wakazingatie maslahi ya wachache na kuweka maslahi ya ya walio wengi mbele. Kwa ujumla nimekereka nayo na kama wakulima hatutoanza kujaaliwa kwenye bajeti mbadala ni vipi tukiwapa nchi?

  Nampongeza JK na serikali yake kwa hili ila hizo pesa zilizotengwa zitolewe mapema ili wananchi wanufaike nazo!

  UPDATES
  Enzi hizi nilikuwa shabiki wa CHADEMA, kabla sijabadili namimi gia angani!Naamini JPM atatufikisha tunapotaka kwenda. Msilie sasa BAVICHA Raisi tuliyemtaka aje atikise system ndio yuko madarakani tumuunge mkono
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa style hii hata mtoto mdogo humdanagnyi, fikiria upya!! Mkitumwa msiwe mnakurupuka, unasema hela za umwagiliaji zimeongezwa hebu taja hiyo miradi mipya aloanzisha kwa hizo hela kama sio hela zote kuingia mifukoni mwenu!! Je bwawa la Manchira Serengeti mradi mloanza mwaka 1980 mshakamilisha, na je miradi ya umwagiliaji ya miwa mtibwa na mpunga kilombero bado inafanya kazi!! Acheni kuwatukana wananchi, wanaona na wanajua nini mnachokifanya!!
   
 3. n

  nmiku Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kaka kama miaka hiyo 11 iliyopita ahadi zimekuwa ni hizo na hatujaona maisha bora kwa Mtanzania yeyote tulivyoahidiwa bali kudidimia, hiyo miaka 4 iliyobaki tutaona nini? Ni yale yale ya Buhemba Gold Mines kudanganya wananchi wa eneo husika wataletewa maendeleo badala yake wameambulia mahandaki everywhere na walioahidi wakachuma chao wakatokomea! Na ya JK yatakuwa hayo hayo. Hatudanganyiki!
   
 4. K

  Kasanga Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hebu kaka mtoa mada kaangalie ule usanii wa matrekta ya kichina yaliyojazana pale Mwenge kuingia eneo la LUGALO! pesa ilyozama na thamani halisi ya hayo matrekta hailingani! watu tayari wameishaanza kulalamika kuwa niafadhali ukanunua yale ya mtumba kama MASSEY FERGASON! Maana hayo ya mjoma wako ukiingiza shambani jembe ndio linalokatika nasio udongo!
   
 5. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mhhh! Sekta ya Uzalishaji ni too broad! Jaribu kujifahamisha nini kimo kwenye sekta hiyo. Dhamira ya kweli ya JK inaweza kuwepo, lakini angalia kilichoko nyuma ya pazia. Hela za KK (Kilimo Kwanza) zinamfaidisha nani? Mikopo kwenye benki kama TIB zinapatikana kwa wakulima wa jinsi gani?

  Ulisha wahi kusikia kuwa Tanzania ime-ban uuzwaji wa tumbaku, sukari na chai nje? Haya mazao yanazalishwa kwa wingi na makampuni makubwa. Mbona mazao ya mkulima mdogo kama mahindi yanapigwa ban (export ban)? Utasema ili watz wengine wasife kwa njaa!

  Hizo traktor na power tiller na exemptions zake anafaidika nani? Umewahi kufanya utafiti kuona endapo bei ya hayo mapembejeo imepungua kutokana na exemptions?
   
 6. Kimbojo

  Kimbojo JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu mtoa mada. Sina uhakika kama unaelewa kwa kina unachokisifia. Unafaham kilimo kwanza kwa mapana yake?. Ebu nikuulize benki ya wakulima mliosema itaanzishwa iko wapi na kama ipo wewe mkulima umekopa hapa sh. ngapi. Je pesa ya epa iliyorudishwa na mkasema imerudishwa na itaanzisha benki ya wakulima je ni sh. ngapi zimerudishwa? unayafahamu haya yote? hata BOT wenyewe hawajui zilko wapi. jjjjjjjjjjje Kikwete wa kwanza kwa hayaa!!!:A S 103:
   
 7. m

  moma2k JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Naomba niliweke wazi hili kuwa Rais Kikwete ni rais bora kuliko marais wote waliomtangulia hapa Tanzania. Nathibitisha hoja yangu kwa ushahidi ufuatao(conclusive evidence):

  1. J.Kikwete siyo dikteta, wakati JK Nyerere alikuwa dikteta mkubwa sana, akifuatiwa na Mkapa.Nyerere alitaka mambo yote ktk nchi yaende kama anavyotaka yeye. Hakuwa tayari kukosolewa.Mkapa naye hivyohivyo.

  2.J.Kikwete ni mtu mwenye utu, ubinadamu. Nyerere, mwinyi, Mkapa hawa jamaa walikuwa hawana utu, ni unyama tuu.

  3.J.Kikwete ni mtu muungwana ambaye yuko tayari muda wote kusikiliza na kufanyia kazi maoni hata ya vyama vya upinzani.Anaheshimu mawazo ya watu bila kujali itikadi za vyama husika. Nyerere alifuta vyama vyote vya upinzani miaka ya sitini, akaleta dhana ya chama kushika hatamu ili imulinde yeye na madaraka yake. Mkapa daima aliporomosha matusi kwa vyama vya upinzani.

  4.J.Kikwete anaheshimu sana utawala wa sheria(Rule of Law). Hapendi kuingilia UHURU WA MAHAKAMA. Wakati waliomtangulia wote walikuwa tayari hata kuingilia uhuru wa mahakama kwa masilahi yao.

  5.J.Kikwete ni mtu ambaye hana mawaa na mtu yeyote.

  6.J.Kikwete amekuwa tayari kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya. Kitu ambacho watangulizi wake wote hawakuwa tayarisha licha ya misukumo ya kimahakama na wanaharakati.Nyerere ndiye alikuwa kinara wa kuvuruga katiba ya nchi kwa masilahi yake. Mwaka 1977 kwa makusudi kabisa akiwa anajua, alitengeneza mkakati wa kuhakikisha katiba ya nchi inatengenezwa na kamati ya chama, siyo wananchi.Ukisoma historia ya constitutional development ktk nchi hii kuanzia katiba ya 1961 hadi 1977 utajua who is Nyerere. Vinginevyo hutamjua Nyerere.

  7.J.Kikwete ni mtu wa Mungu na Changuo la Mungu, ni zawadi ya Mungu kwa watanzania kwani kweli anaheshimu uhuru wa kuabudu, haki za binadamu, hana ubaguzi wa aina yoyote ile.

  Take note: Kama mtazamo wangu huu si wa kweli basi mtakuja kunikumbuka mwaka 2015 atakapopatikana raisi mwingine. Kumpata Raisi mwenye fadhiri za kiutu, kibinadamu, kizalendo, kidemokrasia, kihaki, kama Kikwete ni ngumu sana!

  God Bless you!
   
 8. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mawaaaaaaaaaaa!!!!!!
   
 9. B

  BMT JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  we una matatizo,tena makubwa,kapimwe akili,hata jk mwenyewe sifa hzi ulizompa amekushangaa,kwa great thinker kama wewe unaleta hoja mfuu kama hz kwl?sema rais jk kafanya maendeleo haya kwa watu wake(we need perfomance)hvi unajua tanzania ni ya tatu kwa kuombaomba?tena hii rekodi ni ya kipindi chake,we mtupu na mweupe sana kichwani
   
 10. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Dah watanzania kwa kulalamika, hebu elezeni mipango mizuri mliyonayo kichwani basi, maana mkilalamika bila ku-present your own good idea ili tuseme dah, unacholalamika ni kweli na una option au opinion nzuri, amasivyo huna tofauti na wale tulikuwa tunawaita "watoto wa mama, au kula kulala" maana pamoja na kuwa na umri na uwezo wa kuzalisha mali, chakula hawajakitafuta wao, ila kikiwa na kasoro duh, hilo varangati lake hapo mezani usipime? Hebu tutoeni aibu Wa-Tanzania, anzeni kufikiri positively, na muamue hapo mlipo mnataka kufanya nini kuibadili hii Tanzania, hata Raisi akiwa strong or weak, at the end of the day Tanzania stands high in terms of the developments adn in terms of inter-country politics and image.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  kabisa inflation iko double figures 30%
   
 12. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Jk ni dhaifu, fisadi soma scandal ya IPTL, EPA, WANYAMA PORI walioibwa Kirimanjaro,
   
 13. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ni kiongozi dhaifu kuliko wote? Mifano: kusamehe wezi (EPA), kuteuwa watu dhaifu, kuruhusu wanyama wetu kuibwa, ku engineer kampuni hewa (richmond), kuchekacheka hata kwenye mambo mazito, kushindwa kusimamia kujifua gamba na mengineyo mengi.
   
 14. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Jk..a.k.a kiranja wa la kwanza ei,Danganyika primari sku!
  Yes,he is a human being,never perfect, ndio ana mazuri yake, but hiyo misifa mnayomshushia,akiisoma tu mwenyewe anaweza kuzimia ghafla..!
   
 15. J

  JOE58 Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa vipaumbele vilivyoanishwa ndani ya bajeti kuhusu kilimo ni dhahiri kuwa kilimo kitachukua muda kukua hata kama kikiongezewa mamilioni hayo na mengine! kuhusu miundo mbinu kama chachu ya maendeleo natoa tick,lakini kwa kilimo? sidhani!

  Sababu ni kubwa ni kuwa, msingi mkubwa wa ukuaji wa biashara yoyote ni soko, kama kuna uhakika wa masoko yenye bei za kuvutia uzalishaji, basi binadamu atahangaika tu ,atapata hizo pembeje, huduma za ugani hata kama asipo saidiwa na serikali! sasa soko la mazao ya kilimo nini?

  Ni viwanda vya usindikikaji, ambavyo vinaweza kuanzishwa kwa juhudi za kuunganisha Veta, SIDO, USHIRIKA, na huduma za kibenki! kila pazalishwapo zao pawe na kiwanda cha kusindika na kuongeza thamani! serikali ikisimamia vyema juhudi hizi za wadau hawa, amabao watamobilise, vijana, watapatiwa ujuzi,na vtendea kazi pamoja na mikopo katioka kuanzisha viwanda hivyo, ambavyo vitakuza ajira na kuimarisha soko la mazao hivyo kuleta msukumo (stimulant) katika ukuaji wa kilimo,ufugaji, uvuvi,na hata madini!
   
 16. J

  JOE58 Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hizo sifa ulizoainisha hazipo kabisa katika miongoni mwa kiongozi bora wa nchi, labda labda angekuwa imamu sawa! kiongozi bora ameainishwa katika sifa alizowahi kutaja mwanafalsafa wa zamani wa kiyunani aristotal,alisema " kiongozi bora huotoka katika kundi la watu wenye busara, kwa bahati mbaya watu wakundi hili hawapendi uongozi, na hata wakipata uongozi hukaa kwa ajili ya kutimiza lengo liliwaweka katika uongozi na kuachia ngazi, ni watu wanaoweza kujitoa kwa ajili ya imani waliyonayo katika jambo hata kama ni la hatari" mfano wa viongozi hawa weza kuuona kwa akina Mahtama Ghandi,Nelson Mandela,na hata julius Nyerere! kiongozi ambaye anasita kuchukua maamuzi magumu( to take risk for the sake of good course) sio kiongozi anayefaa hata kidogo! great risk takers ndio walioleta maendeleo ya dunia hii! kama ni wema , ubinadamu nk akahubiri injili sio kuleta maendeleo ya watu! maendeleo ni mapinduzi na mapinduzi huletwa na wenye kujitoa na ku risk kwa ajili ya watu!
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Jk ni rais dhaifu kuliko wote waliopita. Hata ukimwekea kidole kwenye jicho yeye aka! Hana shida. Kama Nyerere alikuwa dikteta basi tunataka madikteta kama Nyerere kuongoza tanzania
   
 18. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuongezea, Kikwete ni very HONEST. Hata alipoulizwa kwa nini nchi yake ni maskini, hakudanganya, alisema tu simply HAJUI.

  Ni mkarimu pia. Chini ya uongozi wake, rafiki zetu wazungu wamefaidika sana kwa kuchukua madini na uwekezaji kama wa RICHMOND. Kama haitoshi, wamezawadiwa TWIGA (lkn kwa mdomo wa baadhi ya watu itabidi warudishwe)

  Ni mwadilifu na mwenye huruma. Kwa huruma yake Babu Seya amebahatika kifungo cha maisha, ilikuwa anyongwe yule.

  Ni mchapa kazi wa kimataifa. Wazungu wanamsifia sana, kipindi cha uongozi wake amesafiri kikazi zaidi ya mara 300 ili kutuombea chakula.

  Ana HURUMA. Hata watu walipoiba EPA alisema warudishe tu, kwa kuwa alijua wana shida ndio maana waliiba.
  -Mkapa alipojiuzia mgodi na kumpa mkewe kiwanda cha korosho kule Mtwara, aliwakataza watu wasimsakame. Namnukuhu 'mwacheni mzee wa watu apumzike'
  -Mawaziri wasioweza kuwajibika pia aliwaonea huruma. Ni kelele tu za Zitto na wenzake

  Hatutapata rais kama huyu asilani
   
 19. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  huna lolote, sema tu unamtamani Miraji akuoe ila unashindwa kuwa straight
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Udhaifu wa kikwete ni udhaifu serikali- Tanzania daima

  jk ni rais dhaifu kuliko wote waliopata kutawala nchi hii.

  Nyerere angekuwa hai asinge kubali jk atawale.
   
Loading...