Kikwete ni Masiha

hata HITLA kuna watu watu walikuwa wana muona vivyohivyo inategemea uko upande gani.kwahiyo sishangai kuona watu wa aina yako wakikesha wakiomba abaki milele ili na wao wafaidi milele.kuna watanzania maelfu kwa maelfu wanakula mlo mmoja tena wa kubahatisha chini ya utawala huu halafu wewe unaleta masihara? iko siku.
 
Kuna masiha wa kweli wa kuteuliwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe;na kuna masiha wa Uongo wasioteuliwa na Bwana Mungu wa wote wenye mwili ! Tafakari mwenyewe, kwamba Kikwete yupo kundi gani la masiha ?
 
Hivi hamjaanza kuamini tu maandiko yangu?
 
This is Jf, bwaaaah! Watu wakielemewa na mastress yao wanakuja kuanzisha thread hapa kuwaongezea wengine stress zao matokeo yake wote mnabaki pale pale na kumtafuta mtu wa kumtwisha uvivu wenu. Mtu huyo anaweza kuwa mungu, kikwete, nyerere and what ever lakini ukweli unabaki pale pale wamatumbi nyie fanyeni kazi kwa ubunifu na juhudi kubwa mtatoka tu, mkitegemea raisi aje awaondolee ugumu wa maisha yenu bado sana hata raisi awe nani hawezi mko wengi mno na kila kukicha mnaongezeka jifunzeni kutoka China, India na Brazil.

Ubunifu huu wa thread bora mngeweka katika uzalishaji mali hatua ingepigwa.
 
mzee wa miba na songambele na wengine, msilolijua ni kama usiku wa kiza. Au msome tena ujumbe kwa uzuri
 
ni masiha kwa upeo wako mdogo,mimi namwona ni kilaza fulani tu,labda kama ni masiha wa mafisadi kwani aliwapa kila watakacho baada ya wao kumpisha kwa mtandao wa kishetani hapo chimwaga hall 2005.

its been a long time but upeo wangu mdogo utadhihirika
 
Usilinganishe mifano ya kwenye bible holela holela,
 

Huyu kweli ni masiha wa familia ya Mwangosi. Ni masiha Mkubwa sana kwa wagonjwa na madaktari hasa tukikumbuka Dr. Ulimboka. Ni masiha wa wamama wanaojifungulia kule Mananyamala na mhimbili tena chini huku wenzao wakichekiwa afya zao India. Ebu muone yule binti wa miaka 65 anapopiga ile suti na masiha wakienda India kuchekiwa meno wanavyopendeza huku watoto wetu wakifia maleria pale Mhimbili, Bugando, na KCMC? Ni masiha wa tembo waliomalizika porini pamoja na simba. Sasa tunaambiwa hata punda haoo China. Ni masiha wa watu wa Mtwara na gesi yao si unakumbuka jeshi lilivyowadhibiti? Uzuri ni kuwa walishasahau siku nyingi wala hawakumbuki kitu maana masiha akipita hao wamejipanga kama kwamba hakuna mkataba mbovu hata mmoja uliokwisha signiwa kuihujumu nchi hii. Tumshukuru huyu masiha kwa dhati kwani ametuamsha toka usingizini na sasa upepo unageuka haraka kuliko alivyotegemea. Ukiona Darisalaaama wenyeji wamejikakamua ujue masiha yuko bandarini na ukombozi waja. Usisahau yale mabomu kule Arusha maana wale hata ukiuwa hapo nusu waliosalia bado wanaendelea na safari. Hata kifo hakiwazuii wale kabisaaa. Ni unawalenga risasi, mabomu, wapi masiha wanamwona na wala hawamwogopi kamwe. Ni masiha wa Wamasai. Ukiona Mmasai amechoma kadi ya chama chake jua masiah yuko karibu ya hakuna rangi ya ukombozi hutana.
 
Tuko pamoja sana. Heri wanaosoma wakaelewa maana si lazima kuwaandikia kama taarifa ya habari. JK anakwenda kudhihirisha kuwa yeye ni mjumbe wa mabadiliko. Ni 'masiha' wa maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma has a tena inapokuja mada ndefu au iliyoandikwa kwenye muundo wa Sana'a(usanii). Mwandishi ametumia ulumbi ufundi wa maneno kufikisha ujumbe hivyo kama Somo la kuchambua vitabu kidato cha tatu limekushinda shuleni huwezi kumuelewa hivyo usimulaumu
 
Daaaa ni message ya 2011 lakini imetimia sasa, kweli kupitia JK ndio LOWASA. ametuwa ukawa na maisha bora yanakwenda kupatikana sasa. ...Ahsante mh Dr Kikwete
 


Mkuu Raia Fulani, wewe unaweza kuwa Nabii ndani ya JF big up kwa kuona mbali
 
Katumia nguvu ndogo kufikiri ameangalia njia zamafanikio zilizokwisha wekwa na team CCM na baada ya kujua maendeleo hayawezi kuja kama upepo.
 
Daaaa ni message ya 2011 lakini imetimia sasa, kweli kupitia JK ndio LOWASA. ametuwa ukawa na maisha bora yanakwenda kupatikana sasa. ...Ahsante mh Dr Kikwete
Yeah nimeelewa hivyo pia!!!,!Kama sio judi zako Kikwete na lowassa tungepata wapi?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…