Kikwete na watanzania

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Waheshimiwa wachangiaji!
Salaam;
Mnakumbuka mwaka 2005 mlivyojitokeza kwa wingi usio mfano kunshangilia na kumpamba Jakaya Mrisho mwana wa Kikwete? Mnakumbuka watu walivyojipanga barabarani, walivyo kanyagana kwenda kwenye mikutano ya hadhara ya kunsikiliza huyu mgombea akitoa sera na mikakati yake? Mnakumbuka kuna baadhi yetu tulitaka kukong'otwa kwa kuuliza tu ''jamani hivi mgombea huyu tunayempamba kama mkombozi tumempima lini na kujiridhisha kuwa ndiye anayefaa kweli?'' Tuliambiwa hebu kaeni pembeni hakuna wa kumlinganisha na huyu! Nyombo zikaimbwa mpaka sauti zikawakaukeni, ngoma zikapigwa mpaka kupasuka, na sherehe zikashamiri kwa kwenda mbele, vinywaji vikakmiminwa kwa nguvu mpya alimradi huyu bwana achukue kile kiti!
Ajabu lakini kweli , leo hali ilivyo ni tofauti kabisa na ilivyokuwa wakati ule! Wa Tanzania tunajifunza lipi hapa? Je haya malumbano yanayoendelea kuhusu udhaifu, ufisadi, kukumbatiana, ukosefu wa mwelekeo, maisha magumu, mifumuko ya bei n.k. tuna yafikiriaje kwa wakati huu na siku zijazo? Tukiitwa wanafiki tutasemaje?
Asalaam aleikum:angry: !
 
Hawa wooooote unaowaona wapiga kelele wote hao walikuwa mashabiki wakubwa wa CCM kabla ya waraka wa kanisa haujatoka! Hawa walitetea mpaka mauaji ya watu kule Mwembechai na Zanzibar... UNAFIKI at its best!
 
Back
Top Bottom