Losomich
JF-Expert Member
- Nov 9, 2011
- 371
- 71
Sitakubali. That is not an issue here.
Umeleta hoja kuwa Rwanda haitegemei misaada kama Tanzania.
Naomba ulete data hapa. According to WB, Tanzania ina Poverty head count ratio of 34% right now.
Na Rwanda ina 44.9%.
Misaada kwa tanzania tangu 2007 ni asilimia 13.7 ya total GDP.
Misaada kwa Rwanda ni asilimia 17.9 ya total GDP.
Kaka~Issue hapa ni kwamba pamoja na Rwanda kupokea misaadi kwa kiwango kinachozidi inayopokea Tz, kuna gap kubwa kwenye matumizi ya misaada kwao na matumizi ya misaada hiyo kwa Tz. Rwanda wametumia na wanaendelea kutumia misaada hiyo kuboresha kilimo cha kahawa, wakati huku Tz asilimia kubwa ya misaada inatumika kwenye shughuli za kiutawala, na kuwekeza zaidi kwenye mizingi ya chama tawala kuwekeza matumizi makubwa fedha za misaada kuhakikisha kwamba wanaendelea kubakia madarakani. Hilo ni wasi kila Mwuungwana hapa Tz anajua hilo. P. Kagame alijua kwa nini Rwanda ilikuwa masikini na akachukua hatua kulikabili tatizo. Lakini kwa upande wa Tz sio rais wala waziri wake mkuu anayejua kwa nini Tz ni masikini. Na mara nyingi wamekuwa wanakiri pasipo aibu tena kwa confidence kubwa tu. Tz kuna raslimali za asili ukilinganisha na nchi yeyote hapa East Afrika lakini tatizo ni viongozi hawa wasio wazalendo ndiyo wanao ifisidi hadi tumefikia hali tuliyonayo sasa. Ili tuweze kujinasibu walau tuamue kwa nia moja kuiondoa huu mfumo wa uongozi uliofikia uko wa kufikiri na tuupachike mfumo wenye mawazo mapya. Eidha kwa kupitia sanduku la kura au nguvu ya umma kama ilivyo na inavyotokea sasa kule mashari ya kati.
