Kikwete na Davos, Kagame na LA Times! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete na Davos, Kagame na LA Times!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 2, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Johnson Mbwambo

  SIKU hizi nina muda wa kutosha kufuatilia majadiliano mbalimbali katika tovuti kadhaa kubwa duniani zinazozungumzia masuala ya Afrika na watawala wetu.

  Baadhi ya mijadala hiyo ya mitandaoni iliyonivutia, hivi karibuni, ni ile iliyomhusu Rais wetu, Jakaya Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda.


  Mjadala kuhusu Kikwete ulihusu kile alichokizungumza kwenye mkutano wa hivi karibuni wa uchumi uliofanyika huko Davos, Uswisi na ule wa Kagame ulihusu habari zilizoandikwa kwenye gazeti la
  Los Angeles Times la huko Marekani kuhusu Rwanda.


  Kwenye mjadala kuhusu alichokisema Kikwete huko Davos, wachangiaji wengi walimlaumu kwa mchango wake ‘mwepesi’ kuhusu nini hasa kinacholitatiza bara la Afrika lishindwe kuendelea, na hivyo kuendelea kutegemea misaada ya nchi tajiri duniani.


  Katika mkutano huo wa Davos, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, aliwaomba marais wa Afrika waliohudhuria mkutano huo kuueleza mkutano ni kwa nini hali hiyo inaendelea kulikumba bara lao.

  Walitangulia kujieleza Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Raila Odinga wa Kenya, na ndipo Rais wetu Jakaya Kikwete alipopewa fursa kuzungumza.

  Kwa mujibu wa wachangiaji wengi kwenye mitandao hiyo, Zuma na Raila walijitahidi kujieleza vizuri; lakini Rais wetu, Jakaya Kikwete, ‘aliboronga’, na kwamba aliishia tu kujenga dhana kwamba nchi za Afrika haziwezi kuendelea bila ya misaada ya mataifa tajiri!

  Baadhi ya wachangiaji kwenye mtandao waliwalaumu wasaidizi wa Rais Kikwete kwamba hawakumuandalia kitu kizito cha kuzungumza

  kwenye mkutano huo, na hivyo kumwachia azungumze mwenyewe kutoka kichwani mwake.

  Hicho alichokisema Kikwete huko Davos nacho kimewekwa (neno kwa neno) kwenye mitandao na mwananchi mmoja.
  Mtazamo huo wa Kikwete huko Davos kwamba Afrika haiwezi kuendelea bila misaada ya mataifa tajiri ndio uliomuudhi Mwingereza

  mmoja ambaye alimshutumu rais wetu gazetini; huku akitumia lugha ambayo haipendezi – lugha ambayo unaweza kusema ni sawa na kupiga chini ya mkanda.


  Huyo Mwingereza alidai alifanya kazi UNDP hapa Tanzania na anaijua vizuri nchi yetu. Kwa mtazamo wake, Kikwete ni rais dhaifu kiutendaji kuliko wengine wote tuliopata kuwanao.


  Alichokisema bwana huyo dhidi ya Kikwete kiliwekwa hata kwenye mtandao wa hapa nchini wa
  Jamiiforum, na watu wamekuwa wakisambaziana habari hiyo hapa nchini kwa njia ya intaneti.

  Labda niweke wazi mapema kabisa kwamba nami naungana na wale wote wanaotofautiana na Rais Kikwete kuhusu kile alichokizungumza kule Davos.

  Si kweli kwamba Afrika haiwezi kuendelea bila kusaidiwa na mataifa tajiri, na si kweli kwamba Afrika haiwezi kulitupilia mbali bakuli la ombaomba ambalo imekuwa ikilitembeza Ulaya na Marekani kwa zaidi ya miaka 50 sasa.


  Lakini nisemi pia kwamba sikushangazwa na kauli hiyo ya Kikwete huko Davos; kwani miaka sita au saba hivi ya uongozi wake, imetuthibitishia sote kuwa si muumini wa dhana ya kujitegemea.


  Na ndiyo maana alikwenda Davos na kulalamika ili tuonewe huruma na Wazungu kwa kutamka kwamba Waafrika tunaishi maisha ya shida mno
  (hand to mouth) na tunahitaji kusaidiwa!


  Najua jambo hili kwamba hatuwezi kuendelea bila misaada ya Wazungu linakera baadhi yetu, na ndio maana mimi binafsi sichoki kumtolea mfano Rais Kagame wa Rwanda kama mmoja wa marais Afrika anayethibitisha kwamba nchi inaweza kupata mafanikio katika vita yake dhidi ya umasikini bila misaada ya Wazungu.


  Mwezi uliopita niliandika katika safu hii kuhusu mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Rwanda imeyapata katika kampeni yake ya kutokomeza nyumba za udongo katika nchi hiyo, na kuwaomba watawala wetu wakajifunze Rwanda kwa Kagame.

  Makala hiyo ilipokelewa vyema na wasomaji wangu wengi, lakini wako wachache waliotofautiana nami; huku wengine wakinipinga kwa

  kutumia lugha chafu ikiwa ni pamoja na wanaoishi Ughaibuni waliosema eti mimi ni Mtutsi. Mpare na Mtutsi wapi kwa wapi jamani?!

  Ni kwa sababu ya hao walionipinga kuhusu Kagame nilifuatilia kwa hamasa kubwa huu mjadala mwingine mitandaoni juu ya kile

  kilichoandikwa na gazeti la
  Los Angeles Times la Marekani kuhusu Kagame.

  Serikali ya Rwanda ilitangaza, hivi karibuni, kwamba imefanikiwa kupunguza umasikini kwa asilimia 12 katika kipindi cha miaka sita iliyopita; yaani imeushusha umasikini kutoka asilimia 57 hadi asilimia 45.

  Mafanikio hayo yamechukuliwa kuwa ni ya aina yake duniani; huku gazeti hilo likiyaita
  ; one of the most stunning poverty drops in the world.


  Ni kwa sababu hiyo
  , Los Angeles Times lilimtafuta mmoja wa wachumi wanaoheshimika duniani anayeitwa Paul Collier ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Uchumi wa Dunia katika Chuo Kikuu cha Oxford na kumuomba ufafanuzi wake juu ya mafanikio hayo ya haraka ya Rwanda.


  Matokeo ya mazungumzo hayo ni kuchapishwa kwa habari hiyo kwenye
  Los Angeles Times iliyobeba kichwa kinachosomeka hivi: How did Rwanda cut its poverty so much? Habari hiyo iliwekwa katika mitandao kadhaa na ikawa ndio chanzo cha majadiliano hayo mitandaoni.


  Kimsingi, mchumi huyo wa Oxford University anataja sababu mbili kubwa zilizoiwezesha Rwanda kupata mafanikio hayo makubwa ndani ya miaka sita.


  Sababu ya kwanza aliyoitaja ni bei nzuri ya kahawa katika soko la dunia, na kwamba Rwanda iliitumia vizuri fursa hiyo.

  Paul Collier anaeleza kwamba Serikali ya Rwanda ilielekeza mapesa iliyoyapata kutoka katika mauzo yake ya nje ya kahawa kwenye miradi ya maendeleo vijijini.

  Kama hivyo ndivyo, Mtanzania unashindwa kujizuia kujiuliza; sisi Tanzania tulikuwa wapi tusifaidike na bei hiyo nzuri ya kahawa katika soko la dunia?


  Lakini si vigumu kulipata jibu la swali hilo hasa katika mazingira ambayo tunaambiwa kuwa kahawa yetu mkoani Kagera inavushwa kila mwaka kuingizwa nchini Uganda, na kwamba ni Uganda ndio inayoiuza nje kwenye soko la dunia!

  Lakini sababu ya pili iliyotajwa na Paul Collier ni kwamba Rwanda ina rais mwadilifu na mchapakazi kweli kweli. Kwa maneno yake mwenyewe Collier alitamka hivi: The President (Kagame) runs a tight ship within government built on performance rather than patronage”.

  Msomi huyo wa Oxford University pia alimsifu Kagame kwa kujenga utamaduni wa uchapaji kazi nchini Rwanda, na kwa kuwapangia mawaziri wake viwango wanavyopaswa kuvifikia kila mwaka, na wasiovifikia huwajibishwa.


  Si hivyo tu, msomi huyo alisema kwamba Rwanda ndio nchi pekee katika bara la Afrika inayokaribia, japo kidogo, njia iliyofikiwa na nchi za Mashariki ya Mbali kupata maendeleo ya haraka. Alisema hivi:


  “Basically, President Kagame built a culture of performance at the top of the civil service –minister well paid but given targets. Rwanda is the nearest that Africa gets to an East Asian-style developmental state.”


  Hivyo ndivyo mkurugenzi huyo wa Oxford University anavyomwona Kagame na Rwanda yake, na sisi tuliobahatika kuitembelea Rwanda ndivyo pia tunavyomwona Kagame.


  Nirudie kusema tena kwamba Kagame ni mfano hai unaothibitisha kwamba Afrika inaweza kuendelea bila ya kutegemea misaada ya Wazungu; kitu ambacho Rais wetu, Jakaya Kikwete, hakiamini; kama alivyotuthibitisha tena kwa kauli yake ile tata kule Davos.


  Kwa hiyo, tunachohitaji Afrika ni kuwa na marais wa aina ya Paul Kagame, na si wa aina ya Jakaya Kikwete na wenzake.

  Hawa (kina Kikwete na marais wenzake Afrika) ndio wale waliofurahia na kuchekelea, hivi karibuni, kule Addis Ababa, Ethiopia wakati wa uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) lililojengwa na Serikali ya China kama ‘msaada’ kwa Waafrika.

  Kina Kikwete na wenzake hawakuona kuwa ni aibu kubwa kwa AU kujengewa hata ofisi zake na China wakati umoja huo umekuwepo kwa miaka zaidi ya 40!

  Kama katika historia ya miaka zaidi ya 40 ya umoja huo, wameshindwa hata kujijengea ofisi tu, watamudu nini?
  Na wala marais wale wa Afrika hawakutambua hata kuwa kujengewa jengo hilo na Wachina ni aina fulani ya “rushwa”!

  Wangelijua kwamba ni aibu na ni ‘rushwa’ ya aina fulani inayotolewa na nchi hiyo inayosomba na kunufaika na maliasili za Afrika; achilia mbali kubwaga bidhaa zake dhaifu kwenye bara hilo, wasingechekelea walivyochekelea wakati wa uzinduzi ule!

  Ni rais mmoja tu barani Afrika ambaye hakuchekelea. Yeye aliiona hiyo kuwa ni aibu kubwa kwa bara letu la Afrika na alitamka hivyo.

  Rais huyo ni Paul Kagame wa Rwanda, na ndiyo maana sikushangaa
  Los Angeles Times likimmwagia sifa kemkem.

  Hii ndio simulizi yangu ya leo kuhusu ya Jakaya Kikwete huko Davos na ya Paul Kagame huko Los Angeles (LA), lakini nihitimishe hivi:

  Kwa miaka 50 tumekuwa tukipokea misaada kutoka kwa Wazungu lakini tumeshindwa kuitumia kujiletea maendeleo na pia imetufanya tushindwe kujitegemea.


  Utegemezi huo umetubwetesha kiasi kwamba (kwa mfano) tukipewa msaada wa boti ya uvuvi, mathalan na Sweden, tutataka pia fedha za kununulia mafuta ya boti hiyo zitoke pia Sweden! Hicho ndicho kiwango cha utegemezi tulichokifikia.


  Ndugu zangu, tumebweteshwa mno na misaada ya Wazungu. Ole wetu siku Wazungu watakapoanza kutuchoka. Na siku hizo hazipo mbali; maana tumeshaanza kuziona dalili.

  Tafakari.
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ntarudi baadae ni ndufu sana
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Acha uvivu wa kusoma soma kwanza kisha uweke hoja yako.
   
 4. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Yaani niache kujipodoa nikae chini kusoma insha. Babu usituchoshe eeh. Kama vipi jaribu kuifupisha hiyo habari yako vinginevyo hupati mchango wangu ng'oooo......
   
 5. m

  mwikumwiku Senior Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu! Nimeisoma tafakuri hii makini kwa maumivu makali sana! Ee Mwenyezi mungu tuhurumie na utuokoe ss wanao! Tuanafedheheshwa sana na viongozi hawa dhalimu!
   
 6. T

  Taso JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Heri yetu, sio ole wetu, Wazungu watakapotuchoka. Umesema mwenyewe misaada ndio inatuponza.
   
 7. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa (nataka twende poin by point) si kweli kuwa Tanzania inapokea misaada mingi zaidi ya Rwanda.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Bibie,
  Ngoja nikufupishie. Anasema inatia aibu kwamba miaka hamsini baada ya kupigania uhuru wetu tuna kiongozi ambaye anafikiria kuwa wale waliotupokonya uhuru wetu wakati mmoja ndio hao hao watakaotukomboa kiuchumi. Ni aibu na Kikwete ni janga la taifa.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  It does not matter. Leo hatuna moyo au ubunifu wa kujitegemea. Hata kilimo tumeshajisalimisha kwa makampuni makubwa ya kibiashara ya nchi za nje.
   
 10. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  We mvivu sana kama presidaa
   
 11. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa namjibu Mzizimkavu.
  Utakaa mtandaoni kulaumu, hiyo haitasaidia. Nia yangu ni kujaribu kutafakari jinsi Rwanda na Tanzania zinavyopata misaada kutoka nje. Rwanda asilimia ya misaada inayopata (as a percentage of GDP) ni zaidi kidogo ya Tanzania.

  Sasa kwanini Kagame azungumziwe humu kama ni rais asiyependa misaada wakati kibakuli anatembeza kama hana akili nzuri?
   
 12. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Walewale mnaorudisha nyuma maendeleo ya Tz
   
 13. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Umetumwa na Jk nini?
   
 14. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Lete data.... siyo kejeli.
   
 15. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli namkumbuka Mwalimu J.K Nyerere.. Alifanya dhana ya maendeleo kwa vitendo pamoja na kuangushwa na watendaji wake... Tuliheshimika na kuombwa ushauri juu ya masuala ya Afrika..na mjumbe wa mkutano alikuwa anasubiri mwakilishi wa Tz ahutubie ndio ajipe udhuru wa kwenda kuvuta sigara... lakini kama livyosema mwenye we JKN kwamba .. siku hizi..kwenye mikutano ya kimataifa mtu akitaka kutoka nje ya ukuimbi wa mkutano kuvuta sigara husubiri zamu ya msemaji wa Tz ili atoke ...
   
 16. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Nilipata kuona yale majadiliano ya DR.JK & DAVOS mtandaoni. Duu kaaz kweli kweli. Sijajua per capital income ya rwanda ni kiasi gan?
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Tukitegemea Misaada kila siku itabidi tukubali Masharti ya misaada ya Akina David Cameron kuruhusu Ushoga na ndoa za jinsia moja je mkuu utakubali misaada ya masharti hayo?
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Sitakubali. That is not an issue here.
  Umeleta hoja kuwa Rwanda haitegemei misaada kama Tanzania.
  Naomba ulete data hapa. According to WB, Tanzania ina Poverty head count ratio of 34% right now.
  Na Rwanda ina 44.9%.
  Misaada kwa tanzania tangu 2007 ni asilimia 13.7 ya total GDP.
  Misaada kwa Rwanda ni asilimia 17.9 ya total GDP.
   
 19. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Tukishamaliza hilo, tuanze kuchambua historia ya Rwanda kama Coltan exporter kuanzia mwaka 2000 mpaka 2011.
  Kwanini haijauza hata kilo moja tangu April 2011?
  Wakati iliuza kilo 115,000 za Coltan in like 2months prior to that?...
   
 20. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180

  Matatizo ya shule za kata! Yaani walichoandika L.A Times unaona hakina maana zaidi ya wewe kujipodoa na uchafu wa China? Mnatia aibu nyie watoto wa sasa.
  Face the challenge so that you can rectify your faulty lines.
   
Loading...