Kimsingi Mh Rais Kikwete hakujiita Dr kihihivi bali ni udaktari wa heshima( Honorary doctorate) aliotunukiwa ktk chuo kikuu cha Nairobi baada ya kazi kubwa ya upatanishi wa mgogoro ule kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu wa kenya wa 2007 na kufanikiwa kuwapatanisha mahasimu Raila Odinga na Kibaki dakika za mwisho.. Lazima ukumbuke kwamba mgogoro huu uliwashinda kabisa wapatanishi Koffi Annan, Benjamin Mkapa, Graca Machel,Mwenyekiti wa AU wakati ule Rais John Kuffor wa Ghana na Mwenyekiti wa EAC wakati huo Rais Museven wa Uganda..Kutokana na juhudi kubwa za Rais Kikwete maafikiano yakapatikana na ndipo jopo la maprofesa Nairobi University lilipomtunuku Udktari huo wa heshima..Pia kihistoria inaonesha kuwa Kikwete ndo Rais wa kwanza barani Africa kupewa udaktari wa heshima na chuo kikuu hicho cha Nairobi..Watanzania tuache upotoshaji juu ya udaktari wa mh kikwete, tuwe wakweli.