Kikwete: MZEE NYERERE

Kikwete: MZEE NYERERE

denoo49

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
6,113
Reaction score
6,953
Mwanzo, nilidhani utakua uzushi, ila leo kupitia maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM, ndio nimeamini kupitia matamshi yake. Hv ni kwanini Ndg. Mrisho Kikwete huwa hataki kutamka Jina "Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere"????
Je na zile picha za kumbukumbu zenye Jina la Baba wa Taifa..., ziliandikwa kimakosa??

Nimewahi kusikia kwa mtu kuwa Rais Kikwete huwa hamuiti Mwalimu Nyerere 'baba wa taifa', kama tunavyofanya watanzania wengi. Japo sina uhakika sana na hili, mimi pia nimemsikiliza JK mara kadhaa anapoongea kuhusu Nyerere hamuiti baba wa taifa bali humuita 'mzee Nyerere'.

Kuna sababu yoyote ya maana inayomfanya JK asimuite baba wa taifa? au ameamua mwenyewe tu kumuita hivyo? Kuna tatizo lolote kutokumuita baba wa taifa?
 
Binafsi sijakuelewa mkuu.

mkuu, nauliza ya kwa kwamba ni kwanini Ndugu Mrisho Kikwete, huwa hayuko tayari kumuita Nyerere, "Baba wa Taifa".
Maana leo amezihirisha kabisa kwa kumuita MZEE NYERFRE
 
Inaonekna mzee ni kuonyesha heshima zaidi, kuliko baba wa taifa.
 
Ulidhani Kikwete ampende Nyerere wakati anajua fika angekuwa hai hata huu urais angeusikia maana alimjua alivyo wa hovyo kuliko mtu mwingine? Analipiza kisasi kichini chini. Mara hii mnasahau jinsi Kikwete alivyo bingwa wa kulipiza visasi!
 
Kwani watu wa ccm wanampenda nyerere?sindio walomuua?hua nafaidi hutuba zake kwani hua ni vigongo tu hakuwahi kuisifia ccm hata siku moja.ndiomaana kizaz cha nyerere kinaikimbia ccm now
 
Ulidhani Kikwete ampende Nyerere wakati anajua fika angekuwa hai hata huu urais angeusikia maana alimjua alivyo wa hovyo kuliko mtu mwingine? Analipiza kisasi kichini chini. Mara hii mnasahau jinsi Kikwete alivyo bingwa wa kulipiza visasi!

Maskini Babu Seya!!!!!
 
mkuu, nauliza ya kwa kwamba ni kwanini Ndugu Mrisho Kikwete, huwa hayuko tayari kumuita Nyerere, "Baba wa Taifa".
Maana leo amezihirisha kabisa kwa kumuita MZEE NYERFRE

Mwalimu aliwahi kumtukana sana Kikwete aliposhiriki kuanzisha fagio la chuma lengo likiwa kuwaondoa viongozi aina ya Kawawa Rashidi chamani.....Mwalimu alimtukana sana sana hata matusi ya ajabu kabisa!! kwamba wewe ni nani kwa mtu kama kawawa ktk nchi hii??....lkn alikuwa ameelezwa na Raisi Mwinyi wakati huo ktijibu kitu chochote.

Nihivi, Mwinyi alipotaka kumteua Kikwete uwaziri alimwambia aende kwanza kwa mwalimu akaombe msamaha kwa kuanzisha vuguvugu la kutaka kumng'oa Kawawa CCM......ndiyo yakamkuta hayo ya kutukanwa kama mtoto...kuwa wewe kijana mnafiki sana hata wenzio wanakujua kuwa mnafiki, n.k...

Sasa Kikwete, akichanganya hili, na lile la mwalimu kupeleka barua yake ya unafiki kwa mkuu wa majeshi(rejea jinsi alivyoondoka monduli kwa msukosuko)...bado ana kinyongo sana na Mwalimu!
 
Hili ndio tatizo la watu wanaoanza na jibu halafu wanalitungia swali!!!
 
Mwanzo, nilidhani utakua uzushi, ila leo kupitia maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM, ndio nimeamini kupitia matamshi yake. Hv ni kwanini Ndg. Mrisho Kikwete huwa hataki kutamka Jina "Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere"????
Je na zile picha za kumbukumbu zenye Jina la Baba wa Taifa..., ziliandikwa kimakosa??

Una hakika?
 
Kukosa adabu mtu mzima! Wote tunamwita baba wa taifa, wewe unasema mzee Nyerere. halafu JK unaitwa mtukufu unaitika! Mtukufu ni Mungu tu!
 
Hili ndio tatizo la watu wanaoanza na jibu halafu wanalitungia swali!!!

mkuu yawezekana ukawa unamaana zaidi kupitia maandiko yako haya. Tafadhali nijuze zaidi nipate kuelewa unacho maanisha.
 
Mwalimu aliwahi kumtukana sana Kikwete aliposhiriki kuanzisha fagio la chuma lengo likiwa kuwaondoa viongozi aina ya Kawawa Rashidi chamani.....Mwalimu alimtukana sana sana hata matusi ya ajabu kabisa!! kwamba wewe ni nani kwa mtu kama kawawa ktk nchi hii??....lkn alikuwa ameelezwa na Raisi Mwinyi wakati huo ktijibu kitu chochote.

Nihivi, Mwinyi alipotaka kumteua Kikwete uwaziri alimwambia aende kwanza kwa mwalimu akaombe msamaha kwa kuanzisha vuguvugu la kutaka kumng'oa Kawawa CCM......ndiyo yakamkuta hayo ya kutukanwa kama mtoto...kuwa wewe kijana mnafiki sana hata wenzio wanakujua kuwa mnafiki, n.k...

Sasa Kikwete, akichanganya hili, na lile la mwalimu kupeleka barua yake ya unafiki kwa mkuu wa majeshi(rejea jinsi alivyoondoka monduli kwa msukosuko)...bado ana kinyongo sana na Mwalimu!

mkuu shukrani kwa taarifa hii, yafaa kua sehemu ya historia. Kwa maana hyo historia bado inamuhukumu?
Na ilikuaje viongozi wa DINI walienda mbali zaidi na kutuamisha ya kua jamaa ni chaguo la Mungu, hawakua na hishoria hii au wali fanya dhami ya kupuuzia historia..?????
 
Hivi Nyerere huyu anayetukuzwa kiasi hichi ni Nusu Mungu? Tuache kuabudi watu, hata mimi siuoni huo ubaba wa taifa mnaoutaka utukuzwe kama dini. akiitwa Mzee Nyerere ndio hasa anastahili.
 
kumuita Mzee Nyerere badala ya Baba wa Taifa ni kumpunguzia heshima yake kwa waTz lakini ni kama kuonesha kuwa huyu mkuu bado anaishi na yuko hai!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mkuu, nauliza ya kwa kwamba ni kwanini Ndugu Mrisho Kikwete, huwa hayuko tayari kumuita Nyerere, "Baba wa Taifa".
Maana leo amezihirisha kabisa kwa kumuita MZEE NYERFRE

Na wewe kwanini hutaki kumtambua na kumpa heshima yake kwa kumuita rais. Jakaya kikwete na sio ndugu. Acha roho mbaya isiyo na ustaarabu au wewe sio mtanzania . Unahangaika kutoa heshima kwa marehemu wakati walio hai wanaokutawala huwaheshimu au kwani akimuita mzee nyerere wewe utaongezewa mshahara kibaruani kwako
 
Back
Top Bottom