Kikwete: Muda wa kampeni ya katiba bado

Kikwete: Muda wa kampeni ya katiba bado

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
3,759
Reaction score
2,209
Habari hii iwafikie UKAWA hasa CHADEMA,wananaharakati,na iliyokuwa tume ya Warioba ambao ni vinara wa kutozingatia sheria kabisa NA KUHESHIMU UTAWALA WA SHERIA.


WAKATI makundi kadhaa yakianza kufanya mikutano na kuendesha midahalo kuhusiana na Katiba Inayopendekezwa, Rais Jakaya Kikwete amesema muda wa kufanya kampeni na kuuelimisha umma juu ya katiba hiyo haujafika na amewataka wananchi kuwa na subira ili kuepusha vurugu.

Akilihutubia taifa kupitia mkutano wake na Wazee wa mkoa wa Dodoma jana mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema sheria ya kura ya maoni ya Katiba mpya inaelekeza muda wa wadau kuuelimisha umma na muda wa kufanya kampeni kabla ya kupigwa kwa kura hiyo.

Alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, zimetengwa siku 60, kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuandaa utaratibu wa wadau kuelimisha umma kuhusu Katiba Inayopendekezwa.

Pia alisema kampeni za kukubali au kukataa katiba hizo zitafanyika siku 30 kabla ya siku ya kura ya maoni.

Ataka subira, asifu kazi ya Warioba "Naomba tuwe na subira, tuzingatie sheria muda wa wadau kuelimisha umma bado haujafika, wana nafasi ya kufanya hivyo na watapewa, lakini tofauti na hivyo ni kuleta vurugu ambazo ndio chanzo cha migogoro," alisema Rais Kikwete.

Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa, Rais Kikwete alisema imejitosheleza kila nyanja na kwamba kazi ya kukusanya maoni iliyofanywa na Tume ya Jaji Joseph Warioba ilikuwa nzuri na ilitumika kama mwongozo kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kupata Katiba Inayopendekezwa.

"Niwashukuru wote waliofanikisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba Inayopendekezwa, wote wamefanya kazi nzuri na sasa uzuri au ubaya wa katiba hiyo sio wa kuambiwa na mtu, waacheni wananchi waisome waione na siku ya kura watachagua," alisisitiza Rais Kikwete.

Alisema wananchi wawe na subira kwani wameagiza nakala nyingi zichapwe za Katiba Inayopendekezwa ili wananchi wengi waipate , waisome na kuielewa kisha wapige kura ya kuamua.

"Wananchi msikubali kuhadaiwa, someni wenyewe Katiba inayopendekezwa, mjue kilichopo na sio kudanganywa na watu maana uhondo wa ngoma lazima uingie ucheze," alisema Rais Kikwete.

Alifafanua kuwa mara baada ya kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Samuel Sitta, alisema kazi yake kama Rais ni kutangaza siku ya kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali.

Kura za maoni

Alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliomba muda zaidi wa kufanya matayarisho ya jinsi ya kuitisha kura hiyo kwa kuwa mfumo mpya utatumika kuandikisha wananchi wote upya wenye lengo la kuziba mianya ya wizi au mtu mmoja kuandikishwa mara mbili.

"Kura ya maoni itaitishwa Aprili 30, mwakani na siku 60, kabla ya kura hiyo kumeandaliwa utaratibu kwa mujibu wa sheria kwa wadau kuelimisha umma," alisema Rais Kikwete na kuongeza ikiwa katiba hiyo itakataliwa, basi kura ya maoni itarudiwa mwezi Juni.

Uchaguzi Serikali za Mitaa

Kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Rais alisema utafanyika Desemba 14, mwaka huu ambapo wananchi kuanzia ngazi ya mitaa, vitongoji na vijiji watachagua viongozi wao na kwamba kazi ya uandikishaji wapigakura itaanza Novemba 27 hadi 30.

Aidha alivikumbusha vyama vya siasa nchini ambavyo vitasimamisha wagombea wake kwenye nafasi hizo kuwasilisha kwa wakati majina ya wagombea wao kwa msimamizi wa kituo cha kupiga kura, ili kuepuka usumbufu.

Hata hivyo alisema kazi ya kunadi wagombea wa vyama vya siasa itaanza Novemba 30 na kumalizika Desemba 13 ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi wenyewe.

Alisisitiza kuwa, ni vyema wananchi wakawa makini na aina ya viongozi wanaowachagua na kwamba wakichagua viongozi wazuri watakuwa wamejenga msingi bora.

"Chagueni wanaopenda utulivu na sio vurugu, kwa maana mkishamchagua mtu ovyo mtajuta… halafu ndio kwanza yuko madarakani itabidi mvumilie kwa miaka yake yote ya uongozi, ila mkichagua kiongozi mzuri mtaendeleza utulivu na maendeleo," alionya Rais Kikwete.

Kuhusu ebola

Akizungumzia ugonjwa wa ebola, Rais Kikwete alisema Watanzania wanapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo, ingawa haijaingia nchini.

Alisema kasi ya kuenea kwake ni kubwa na kwamba unapoingia, unaleta madhara makubwa hivyo hatuna budi kuchukua hatua za kujikinga na kuhakikisha mipaka yote ya nchi na viwanja vya ndege vinakuwa na tahadhari hiyo.

Alishauri wananchi kutoa taarifa endapo wataona mtu au kuwa na dalili za ugonjwa huo, ambazo baadhi yake ni homa kali, kutokwa na damu kwenye matundu mbalimbali ya mwili na kutapika.

Dk Shein aonya wachochezi

Wakati Rais Kikwete akiusihi umma kuachana na michakato ya kampeni za kuelimisha umma juu ya Katiba Inayopendekezwa hadi hapo muda mwafaka utakapofika, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha kutumia vibaya mchakato wa Katiba Inayopendekezwa kwa lengo ya kuwagawa wananchi na kutishia amani na utulivu uliopo nchini.

Lakini pia ameelezea kukerwa na kuchoshwa na matusi yanayojitokeza katika kipindi hiki kutoka kwa baadhi ya viongozi, huku akisema atawachukulia hatua za kisheria na za kinidhamu bila kujali wana nyadhifa gani.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa CCM katika maadhimisho ya miaka minne ya kuwepo madarakani tangu aliposhinda Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

"Nitawachukulia hatua za kisheria na kinidhamu viongozi wanaotumia vibaya mchakato wa kupata Katiba mpya kwa kutoa kauli za chuki na kutukanana katika majukwaa… nitatumia Katiba na Sheria na sio ubabe kwa sababu sio kawaida yangu kufanya hivyo," alisema.

Alisema kumeanza kujitokeza viashiria vya kuanza kuvuruga amani na utulivu iliyopo sasa kwa kisingizio cha mchakato wa rasimu ya Katiba Inayopendekezwa hivi sasa.

Alisema Katiba Inayopendekezwa ni mkombozi kwa wananchi wa Zanzibar kwa sababu imejibu hoja za malalamiko na kero za Muungano ambazo awali zilikuwa zikilalamikiwa na wananchi ikiwemo wanasiasa.

Akifafanua, alisema kwa muda mrefu wananchi wa Zanzibar walikuwa na malalamiko mengi katika Muungano ambayo kwa bahati nzuri katika Katiba Inayopendekezwa yamepatiwa jawabu sahihi.

Kwa mfano alisema si kweli kwamba Muungano uliopo sasa umeimeza Zanzibar na haitambuliwi katika jumuiya za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa.


Chanzo: Habari Leo
 
Mbona yeye anapiga kampeni ya kura ya NDIO wakati sheria inazuia?na amesema kura ya Hapana itarudisha mambo nyuma.
 
Kwa ukawa bado ila kwa CCM tayari. Hii nchi ni nouma. Bora aende zake Marekani maana ni kama hayupo
 
Nani alianza kampeini kabla ya muda. Raisi alifungua pazia la kampeini kabla ya muda alipokuwa mwanza. Yeye kufanya kampeini kabla ya muda ni ruksa lakini kwa wengine iweje iwe haramu.
 
Mbona siku ya kuzima mwenge alitutangazia kuwa itakapokuja katiba pendekezwa tuikubali kwa kura ya ndiyooooooooooo.Acha hizo prof.
 
Habari hii iwafikie UKAWA hasa CHADEMA,wananaharakati,na iliyokuwa tume ya Warioba ambao ni vinara wa kutozingatia sheria kabisa NA KUHESHIMU UTAWALA WA SHERIA.

WARYOBA sasa atulie MIKOCHENI na SIGARA zake.
 
Kwa wengine bado kwake tayari. Siku akimaliza uongozi tutasikia mengi maana watu wanamstahi kwa wakati huu.
Hivi siku hizi keshajua kwa nini Tanzania ni maskini?
 
....huyu mtu pwani ni wa ajabu sana!amegawa nchi,haaminiki,ashauriki,pia inaonekana yeye ni yeye basi....bwana nchi haiongozwia kwa misuli.....elewana na viongozi wenzako wa kisiasa kwanza.wewe hauoni ulivyogawa nchi?
 
CCM tulishawajui kuwa hamana nia njema na Tanzania kwani kuwaelimisha watu kuna muda wake?mbona yeye mwenyewe na chama chake wanaendelea kupiga kampeni kama kawaida.
 
...masikini Profesa kikwete! akina Chenge na Sitta wanamburuza wanavyotaka, wamemfanya awe kituko tena cha ajabuajabu hata anachokisema hakieleweki na yeye mwenyewe sijui kama anakielewa. Utadhani kila anapoenda kwenye mkutano basi asubuhi yake wanashinda wakimkremisha cha kwenda kusema. Mara Hongera tume ya katiba kwa kutuandalia rasimu nzuri, mara rasimu hii ikipita jeshi litapindua serikali, mara bunge hili haliwezi kutupatia katiba nzuri, mara tufanyie marekebisho muhimu katika katiba ya sasa ili kufanya uchaguzi mwakani na baada ya hapo ndipo kura za maoni zipigwe, mara nitawashangaa sana watakaoikataa katiba hii pendekezwa, mara wakati ukifika mtapata katiba muitakayo maana hakuna atakayeweza kuizuia, mara tusianze kampeni kabla ya muda lakini wananchi muipigie kura ya ndiyo katiba pendekezwa.
Hakika wananchi tumsaidie rais wetu. Tuwazuie akina SITTA kumdhalilisha Rais wetu aweze kuondoka madarakani kwa heshima vinginevyo historia hii ikiandikwa vizazi na vizazi vitamdharau sana rais wetu mpendwa kwa uzuzu anaopandikiziwa na akina Sitta, ingawa na yeye pia sijui kwa nini hachanganyi akili zake na mambo ya kuambiwa. Maana BABA WA TAIFA Alishawahi kusema "... mtu mwenye akili akikuambia jambo la kipumbavu na anajua una akili kujua anachokuambia ni cha kipumbavu lakini ukakikubali kama zuzu vile, ANAKUDHARAU" Sijui kama Rais wetu mpendwa anajua kuwa hao akina SITTA na CHENGE wanamdharau kiasi gani.
 
mke wa Kikwete juzijuzi katika mikutano yake alikuwa anawaambia wanawake wenzake waipigie katiba inayopendekezwa kura ya ndio,mbona ameshindwa kumkemea mtu anaye kuwa nae nyumba moja? kwa kweli hila za ccm zimepitwa na miaka wale sio wakati
 
Kama nia yake ni kudhibiti vurugu awachukulie hatua kali kwanza wale waliofanya vurugu kwenye mdahalo wa Waryoba ili liwe fundisho kwao na kwa wengine wanaokusudia kufanya vurugu kama hizo.
 
UKAWA at al hatujaanza kampeni ya katiba bali tuko kwenye mijadala na midahalo kujadili rasimu ya katiba iliyobeba maoni yetu wananchi na kuwasilishwa na Jaji wariba pamoja na Rasimu ya katiba iliyowasilishwa na Chenge chini ya usimamizi wa Sitta.
 
Yah,huyu ndo rais wangu. Nasikia-ga kuna 'BAN' Ila sijui maana yake.
 
Kauli kama hizi ndizo zinazomfanya Kikwete adharaulike na kila mwenye akili. Siku anakabidhiwa alisema anawaomba watanzania waikubali. Akiwa Mwanza akarudia tena, na jana Dodoma tena amerudia hivyo hivyo.

Huyu Rais wetu huwa haelewi anachosema mwenyewe. Akitamka yeye na wahuni wengine wa CCM kama akina Makonda siyo kampeni ila akitamka Warioba, Maalim Seif, Lipumba inakuwa kampeni! Disgusting.
 
...masikini Profesa kikwete! akina Chenge na Sitta wanamburuza wanavyotaka, wamemfanya awe kituko tena cha ajabuajabu hata anachokisema hakieleweki na yeye mwenyewe sijui kama anakielewa. Utadhani kila anapoenda kwenye mkutano basi asubuhi yake wanashinda wakimkremisha cha kwenda kusema. Mara Hongera tume ya katiba kwa kutuandalia rasimu nzuri, mara rasimu hii ikipita jeshi litapindua serikali, mara bunge hili haliwezi kutupatia katiba nzuri, mara tufanyie marekebisho muhimu katika katiba ya sasa ili kufanya uchaguzi mwakani na baada ya hapo ndipo kura za maoni zipigwe, mara nitawashangaa sana watakaoikataa katiba hii pendekezwa, mara wakati ukifika mtapata katiba muitakayo maana hakuna atakayeweza kuizuia, mara tusianze kampeni kabla ya muda lakini wananchi muipigie kura ya ndiyo katiba pendekezwa.
Hakika wananchi tumsaidie rais wetu. Tuwazuie akina SITTA kumdhalilisha Rais wetu aweze kuondoka madarakani kwa heshima vinginevyo historia hii ikiandikwa vizazi na vizazi vitamdharau sana rais wetu mpendwa kwa uzuzu anaopandikiziwa na akina Sitta, ingawa na yeye pia sijui kwa nini hachanganyi akili zake na mambo ya kuambiwa. Maana BABA WA TAIFA Alishawahi kusema "... mtu mwenye akili akikuambia jambo la kipumbavu na anajua una akili kujua anachokuambia ni cha kipumbavu lakini ukakikubali kama zuzu vile, ANAKUDHARAU" Sijui kama Rais wetu mpendwa anajua kuwa hao akina SITTA na CHENGE wanamdharau kiasi gani.


Hawa wajanja wa magamba wanaoutaka URAIS kwa udi na uvumba wanamtayarisha DHAIFU ili awe totally LAME DUCK mpaka wakati wa mchujo wa wagombea asiwe na nguvu hata chembe ili waweze kukisambaratisha chama chao kama kundi lao halitafanikiwa kumpitisha mtu wao!!
 
Back
Top Bottom