MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Mjerumani aitwaye Otto von Bismarck aliwahi kusema ‘’Politics is the art of the possible''.
Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye kwa sasa anatembelewa na watu/viongozi (wa ngazi za juu za kitaifa).
Alianza Rais Magufuli kumtembelea, hakuamini kama anaweza kutembelewa na Rais Magufuli.
Baada ya Rais Magufuli, kwa sasa ameibuka Waziri Mkuu, Majaliwa.
Baada ya Waziri Mkuu, Majaliwa, kwa sasa ameibuka Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.
Ama kweli, usitukane mamba kabla hujavuka mto!
Naweza pia kusema, usitukane wakunga...
Viongozi wetu wameonyesha ukomavu mkubwa wa kifikra katika mitazamo ya kisiasa!
============================================================

Dar es Salaam. Rais mstaafu, Jakaya Kikwete akiambatana na mkewe Salma, jana walimtembelea Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Muhimbili.
Kikwete ambaye alifika hospitalini hapo saa 11 jioni, alianza kuwasalimia baadhi ya wagonjwa waliolazwa na baadaye kuingia wodi aliyolazwa Sumaye.
Baada ya kuingia katika chumba hicho, Kikwete alikaa kwenye kochi pamoja na Sumaye kisha kumpa pole na kumtania Sumaye aliyekuwa na mkewe Esther kuwa amenenepa japokuwa anaumwa.
Sumaye alisema ana siku ya tano hospitalini hapo na kuelezea furaha yake kwa ujio huo wa Kikwete.
“Japokuwa nilikuwa katika hali mbaya ila sasa hivi naendelea vizuri. Pia, nakupongeza mheshimiwa (Kikwete) kwa kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar,” alisema Sumaye. Mbali na Kikwete, Waziri Mkuu, Kassim majaliwa na mkewe nao walimtembelea kiongozi huyo jana.
Kaimu Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema kila siku hali ya Sumaye inaimarika.
Juzi, Rais Magufuli alimtembelea Sumaye na kumpa pole huku akimuombea apone haraka.
Chanzo: Mwananchi
Last edited: