Kikwete kwa maranyingine tena na serikali tatu.

Kikwete kwa maranyingine tena na serikali tatu.

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete
ameendelea kusisitiza kuwa Tume ya Jaji
Joseph Warioba haina ushahidi kwamba
Watanzania wengi wanataka muundo wa
Muungano wa serikali tatu.
Kauli hiyo aliitoa wiki hii jijini Dar es Salaam
kwenye mahojiano maalumu na Kituo cha
Televisheni cha NTV kilichopo chini ya Nation
Media Group (NMG).

Baadhi ya vyombo vingine vya habari vilivyo
chini ya NMG ni gazeti hili la Mwananchi,
The Citizen na Mwanaspoti kwa upande wa
Tanzania, Daily Monitor kwa upande wa
Uganda na Daily Nation kwa upande wa
Kenya.

Rais Kikwete ambaye moja ya mambo
atakayokumbukwa kwenye uongozi wake ni
kuasisi mchakato wa Katiba, alizungumzia
hoja ya serikali tatu akisema, hakuna
ushahidi kwamba Watanzania wengi
wanataka muundo wa Muungano wa serikali
tatu.

“Hakuna ushahidi kwamba watu wengi katika
nchi hii wanataka serikali tatu, hakuna
ushahidi wa namna hiyo, hata tume yenyewe
haikubaini hicho. Kinachofanywa na vyombo
vya habari ni kuandika habari za wajumbe
wa Bunge la Katiba wanaotaka serikali tatu,
ndiyo kwenye masilahi yao, wanapaza sauti
za wale wanaotaka serikali tatu, hao ndiyo
sauti zao zinasikika. Lakini hawataki kupaza
sauti za wale wanaotaka serikali mbili,”
alifafanua.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuikosoa
ripoti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba. Mara ya
kwanza aliikosoa wakati akizindua Bunge la
Katiba Machi 21 mjini Dodoma.
Rais Kikwete ambaye amewahi kuwa Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa kwa kipindi cha miaka 10, katika
mahojiano hayo alisema katika kuadhimisha
miaka 50 ya Muungano, jambo muhimu na
kubwa ni kuendelea kuwapo kwa Muungano.

“Tunayo mifano ya nchi zilizojaribu
kuungana, lakini zilishindwa, Senegal-
Gambia, Ghana-Guinea, Misri na Libya.

“Muungano umeendelea kuwepo kwa nusu ya
karne ni mafanikio makubwa. Kumekuwepo
na wakati mgumu na changamoto mbalimbali,
lakini tumeweza kukabiliana nazo na
umeendelea kuwa imara zaidi. Siyo kuendelea
kuwepo tu pia umeendelea kuimarika na
mchakato wa mabadiliko ya Katiba
utaimarisha zaidi Muungano na tutakuwa na
Muungano imara baada ya kupata Katiba
Mpya,” alifafanua Rais Kikwete.

Akizungumza kwa kujiamini kutokana na
uzoefu wake wa muda mrefu ndani ya CCM
na Serikali, Rais Kikwete alisema Muungano
ulikotoka ulikuwa imara na umeendelea
kukua katika hali ya uimara wake.
“Kuna mambo ambayo tumefanya yamezidi
kuimarisha Muungano na umeendelea kuwa
na mafanikio makubwa.”
Alisema suala si kuendelea kwa muundo
ulivyo sasa, suala la msingi ni kujadili namna
ya kutengeneza muundo wa Muungano,
kwamba upi ni bora.
 
sasa anaposema tume haikubaini watanzania wanataka s3 je anapinga takwimu za tume aliyoiunda yeye?
 
Nani kakwambia hataki muungano, tunataka kutambulika kwa tanganyika mbn mko na uwoga wa muungano, mara gharama, mara takwimu, mara jeshi full kuhangaika na hoja zisizo na mbele wala katikati
 
sasa anaposema tume haikubaini watanzania wanataka s3 je anapinga takwimu za tume aliyoiunda yeye?
Takwimu za tume zimeokotwa kigoma na manzese siyo za wananchi.
 
"What is evil? - Whatever springs from weakness" - Friedrich Nietzesche
 
Ndo walewale, kikwete hana wazo jipya. Miaka nenda rudi akiwa madarakani, kama mawazo ni chakula basi mawazo yake yalishaharibika kitambo, habadiliki na wakati uliopo.
 
Mr Dhaifu...huyu mtu wa kumuhurumia sijui hata alipokuwa mwanafunzi ufaulu wake ulikuaje!!!
 
Nani kakwambia hataki muungano, tunataka kutambulika kwa tanganyika mbn mko na uwoga wa muungano, mara gharama, mara takwimu, mara jeshi full kuhangaika na hoja zisizo na mbele wala katikati

Ukiitambua Tanganyika nini utanufaika?
 
Huyu jamaa ana tatizo la kisaikolojia na anatangaza vita na wananchi,kwanza na kura zake si harari kama ni harari mbona tume ya uchaguzi haina matokeo ya uraisi 2010? yeye ana uharari gani wa kukubarika kuwa raisi wa Tz?

Poor idiot!
 
Kwa maneno mengine ni kuwa Rasimu ya Katiba inayojadiliwa bungeni ni batili! Na bunge la katiba linalo jadili hiyo rasimu nalo ni batili kwakuwa kila kilichopendekezwa katika rasimu hakina ushahidi!

Lakini pia, tumemsikia mara kadhaa Rais Kikwete akiipongeza Tume ya Jaji Warioba kwa kazi nzuri ya kutukuka, sasa inakuwaje kuwa leo anampongeza (akiwa naye) kesho anamponda? Jk alikuwa ni mtu wa kwanza kukabidhiwa hiyo rasimu, sasa hayo mapungufu na ushahidi uliokosekana si aliuona kwanza? Kwanini aruhusu uwepo wa bunge kwa jambo lisilo na ushahidi?

Kama Jaji Warioba na wenzie wameleta mambo yasiyo na ushahidi, kwanini asishitakiwe mahakamani na alipe gharama zote za tume walizotumia kwa mambo ya kughushi?
 
wafanye wafanyavyo, tunataka tanganyika yetu, na mkuu wa kaya angetuambia idadi ya watu waliompigia kura 2010, je tukifata vigezo vya idadi ya watu, je anastahili kuwepo ikulu?
 
Rais Kikwete ambaye moja ya mambo atakayokumbukwa kwenye uongozi wake ni
kuasisi mchakato wa Katiba, alizungumzia hoja ya serikali tatu akisema, hakuna ushahidi kwamba Watanzania wengi wanataka muundo wa Muungano wa serikali tatu.
Na kweli hapa atakumbukwa sana kwa kuanzisha kitu bila kutafakari kwa undani matokeo yake. Ni kama vile unajifunza kurusha ndege bila kujifunza jinsi ya kutua baada ya kuruka ambapo matokeo yake yanaweza kuharibu kabisa lengo lako zuri kwa kuanguka!
Ni kwamba haya mambo Mwalimu aliamua kuwa 'dikteta' kwa makusudi maana alijua kuwa 80% ya Watanzania uelewa wao ni wa mashaka na sio watu wa kukaa nao mezani mkajadili kitu na kupata mwafaka, jionee mwenyewe kinachoendelea sehemu nyingi nchini ikijumuisha Bunge la katiba lenyewe. Ndio waliokataa hata vyama vingi lakini ukatumika 'udikteta' huo huo kuhalalisha mawazo ya 20% maana ndio waelewa.
Hata mzee Mwinyi na Mkapa waliyaona haya kwa kiasi chao lakini walikaa kimya kwa busara zao. Sasa JK alitegeme anaunda tume inayomjumuisha Jaji Warioba, Jaji Ramadhani, Dk. (wa ukweli) Salim, Dk. Mvungu (RIP) na wengineo makini kuja kutoa 'puppet reports'!?

 
Kimsingi Kikwete anapaswa kushtakiwa kwa kuvunja kwa kutokuchukua hatua alipoona katiba inavunjwa kwa Zanzibar kufanya mabadiliko ya katiba yao ambayo mabadiliko hayo ya kumi ya 2010 ya katiba ya zanzibar ya 1984 ilivunja Muungano kwa wao kujitangaza kuwa ni nchi.Jambo kama hilo lilipotokea mwaka 1984 aliyekua rais wa Zanzibar wakati huo aliwajibishwa kwa kuvuliwa vyeo vyote aliyovyokua navyo. Kikwete yeye alikaa kimya na huo ndiyo msingi wa kupendekezwa serikali tatu kwa kuwa Katiba ya Tanzania ilivunjwa bila waliko madarkani kuchua hatua ya kunusuru jambo hilo. Serikali tatu ni njia pekee ya kuvunika kombe mwanaharamu apite.
 
Back
Top Bottom