Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Mojawapo ya hofu nilizonazo ni kuwa Kikwete hatimaye anaweza kuwa Gorbachev wetu. Yawezekana akaja na mawazo ya Perestroika anapotaka kugombea mara ya pili na watu wakakubali na matokeo yake itakuwa ni kuvunjika kwa Muungano wetu.
Kama Gorbachev sidhani kama atakuwa na ujasiri wa kutumia nguvu kuzuia kumeguka kwa muungano au kama ana ujuzi wa kisiasa kuimarisha Muungano. Hadi hivi sasa ni wazi kuwa suala al Muungano analiona ni gumu mno kiasi cha kushindwa hata kujaribu kulirekebisha na matokeo yake yeye na CCM wanaamua kutafuta "the path of least resistance" a.k.a referendum.
Kuna watu hata hivyo wanamuona Gorbachev shujaa na wanamshukuru kwa maamuzi yake; na kuna watu (kama kina Putin) ambao wamesimama na kurudisha ukutufu wa yule "Dubu" wa Ulaya Mashariki.
Hili swali bado natafuta jibu lake kwani pande zote mbili naweza kuziona kinadharia.

Muungano haulazimishwi na JK pekee, na si jambo la kumuangalia mtu moja moja na kutoa hukumu..muungano ni majumuisho ya historia, faida/hasara, wananchi, na wakati wake
Kama muungano utavujika ni wakati wake umefika wala halitakuwa kosa la gorbachov wala JK, wanaolilia muungano watuambie kinagaubaga wanataka muungano kwasababu zipi? na wanapata faida zipi kwa kuangalia historia yake nk. please "msilete habari za alinacha eti nyerere kasema" this is an old crying song hatutaki kusikia..tuambiwe sasa hivi (wakati huu) muungano unatusaidia nini? na uwe muungano wa aina gani? kwa manufaa zaidi?
Wanaokataa muugano vilevile watuambia hawataki kwasababu gani wanapata hasara gani na wanataka muugano wa aina gani?
Hoja ziwekwe wazi..hii mambo imefichwa sana utafikiri karume na nyerere walikuwa malaika ni ujinga kwa nchi yenye wasomi kama nchi yangu
JK wetu asipoisimamia na kuilinda KATIBA yetu ya JMT atakuwa Gorbachev wetu. Zanzibar sasa hivi wanatoa matamshi yao kama vile katiba hii haipo, haiwahusu. JK amewekwa pale kwa mujibu wa katiba hii lakini anakuwa kama anaionea haya vile!
Muungano haulazimishwi na JK pekee, na si jambo la kumuangalia mtu moja moja na kutoa hukumu..muungano ni majumuisho ya historia, faida/hasara, wananchi, na wakati wake
Kama muungano utavujika ni wakati wake umefika wala halitakuwa kosa la gorbachov wala JK, wanaolilia muungano watuambie kinagaubaga wanataka muungano kwasababu zipi? na wanapata faida zipi kwa kuangalia historia yake nk. please "msilete habari za alinacha eti nyerere kasema" this is an old crying song hatutaki kusikia..tuambiwe sasa hivi (wakati huu) muungano unatusaidia nini? na uwe muungano wa aina gani? kwa manufaa zaidi?
Wanaokataa muugano vilevile watuambia hawataki kwasababu gani wanapata hasara gani na wanataka muugano wa aina gani?
Hoja ziwekwe wazi..hii mambo imefichwa sana utafikiri karume na nyerere walikuwa malaika ni ujinga kwa nchi yenye wasomi kama nchi yangu
Lakini, Ikulu au rais (kama taasisi) nimoja ya mihimili muhimu ya Muungano. Mtu anayeongoza taasisihiyo anapaswa kutoa uongozi utakaotyoa mwelekeo wa mambo muhimu kama nchi na kwa sisi, Muungano ni moja ya mambo muhimu kabisa. Kwa hiyo, JK hatoweza kukwepa lawama au sifa iwapo lolote litatokea kuuhusu Muungano wakati wa kipindi cha yeye kuongoza taasisi hiyoMuungano haulazimishwi na JK pekee, na si jambo la kumuangalia mtu moja moja na kutoa hukumu...
Natumai na wewe ni msomi mbona hueleweki where did u stand on? and why? TOA MTIZAMO WAKO.
Wazanzibari wanataka kuitumia katiba yao bila kuona kama inagongana na katiba ya JMT ambayo kimsingi ndio iliyo juu ya katiba zote nchi hii.
katiba JMT inawaamulia rais wa Zanzibar?
Then, wanatakiwa wawe wameshavunja huu muungano siku nyingi, kwakuwa ni Ukoloni
Umuhimu wa muungano ni nini?Lakini, Ikulu au rais (kama taasisi) nimoja ya mihimili muhimu ya Muungano. Mtu anayeongoza taasisihiyo anapaswa kutoa uongozi utakaotyoa mwelekeo wa mambo muhimu kama nchi na kwa sisi, Muungano ni moja ya mambo muhimu kabisa. Kwa hiyo, JK hatoweza kukwepa lawama au sifa iwapo lolote litatokea kuuhusu Muungano wakati wa kipindi cha yeye kuongoza taasisi hiyo
Kusigina katiba kuanzia kwenye SMZ kutaka Bendera yao, then Ukaja kupigwa kwa wimbo wao wa taifa kwenye baraza la wawakilishi, ikaja kodi , mafuta na hivi karibuni wabara wataambiwa kuanza kutumia pasi za kusafiria kuingia huko visiwani. Hadithi ya Mwarabu na Ngamia inakaribia kutimia. Nadharia yangu ni kwamba ata kama URT itavunjika then kuna hatari ya kuwa na serikali ya Pemba na Zanzibar { Makubaliano ya Maalimu na Karume nyuma ya Pazia}. Kikwete inaonekana ameridhia kufa kwa URT.
Muungano ulipigiwa kura na Bunge la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar. Pande zote mbili zilijadili (najua wengi hawajui historia hiyo). Nyerere alileta hoja Bungeni na kuwaelewa wabunge wetu kwanini mataifa mawili haya yataungana. Wabunge wakaridhia na ni baada ya hapo ndio Muungano ukafanyika.
Hivyo ni Muungano halali na ni jukumu la kila Mtanzania kuulinda. Katika kuulinda huko ni jukumu letu kuwapinga pasipo kuwapepesea macho wale wote wanaotaka Muungano uvunjike kwa sababu hawataki kufanya maamuzi magumu au kuzungumzia mambo yanayoleta utata katika Muungano. Wapo watu wa bara ambao kwa kawaida hatupendi sana migongano, tunapenda vitu lelemama kiasi kwamba tumekuwa kama tumedekezwa hivi!
Serikali ikisema "hawa wanaleta mgawanyiko katika jamii" basi kama watoto tunakubali na kuwakimbia wenzetu kwa sababu "serikali imesema"; Serikali ikija na kusema wapinzani wanataka kuligawa taifa basi tunakimbia kama watoto huku tumenyanyua mikono tubebwe huku tunaonesha vidole "yule anataka kuligawa taifa mama!".
Hatutaki kugonganisha mawazo na matokeo yake hata kwenye vikao vya kazi tumekuwa hivi hivi tu. Mtu anayebisha sana anaonekana "mbishi tu"; mtu anayetaka maelezo zaidi anaonekana kama anataka kujipendekeza. Tunataka mambo ya upole upole na taratibu.
Ndio maana utaona watu wengi wa bara wanaotaka Muungano uvunjike wanafanya hivyo kwa sababu utaondoa "migongano" na kubishana bishana. Tunataka "utulivu, amani, na mshikamano" wa uongo. Ndio maana watu wa bara wanaona kama Zanzibar ni wakorofi kweli kumbe kule Zanzibar wao wameshazoea zile siasa za kujibizana, kubishana na serikali, na kutunishiana misuli.
Ninaamini athari kubwa sana ya ukoloni katika psyche ya watu wa bara ni unchecked docility ya ajabu sana. Na watawala wetu wanatumia sana hii kuwatuliza watu wa bara.
Muungano tutaulinda na tutaudumisha na kuuboresha. Tutawapinga watu wa bara wanaotaka kuuvunja kwa sababu hawataki kubishana na kulumbana na kugongana kifikra na tutawapinga watu wa visiwani wanaotaka kuuvunja kwa sababu wanaogopa kukubali ukweli wa umuhimu wa muungano.
Tutawaunga mkono wale wote majasiri ambao watasimama na kutoa hoja za jinsi ya kuudumisha, watakaokuwa tayari kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuuboresha na wale watakaonesha uongozi wa kuboresha muungano wetu kwa uwazi na ukweli na ujasiri usio kikomo.
Natumaini hatutawafumbia macho wala kuwaonea haya kuwashughulikia pasipo kuwabembeleza watu wanaofanya njama za kuuvunja muungano wetu.
Muungano daima!