Ni kweli. Yeye ni shahidi muhimu sana maana akiwa Waziri wa Mambo ya nje alitetea ununuzi wa nyumba hiyo ya Ubalozi kwamba umefuata taratibu zote pamoja na sheria ya manunuzi. Ninachojiuliza kila siku ni je, endapo alinukuliwa akitetea (bungeni) ununuzi huo, inakuaje anaruhusu Prof kuburuzwa mahakamani na DPP? Nahisi ni kiini macho kingine hiki.
Gazeti la Mwanahalisi haliko mitaani leo! Kila nilipokwenda walisema halijasambazwa! Kumbe pengine ni sababu ya Habari Hii!!!!!!! Makubwa
Alitakiwa tangu siku nyingi walikuwa wakimuonea haya tu sasa kijana Kubenea ameamua kutufumbua macho
Marais wetu wa ngozi nyeusi na unyanyasaji wao chini ya dhana potofu ya 'ABOVE THE LAW', sijui kama atakua wa kwanza kutii sheria na kwenda mahakamani bila kuleta longolongo vile???????????
Raisi Jakaya Kikwete ametajwa kuwa mmoja wa mashahidi muhimu sana wa professa Costa Mahalu na ameitwa mahakami kwa ajili ya kutoa Ushahidi.
Source mwanahalisi ya leo 4/05/2011
Mimi namshangaa sana huyu profesa wa sheria asiyejua au asiyetaka kufuata sheria. Huy bwana alishtakiwa na ushahidi ulipoletwa mahakamani akaonekana ana kesi ya kujibu. Tokea hapo amekuwa akifanya sarakasi za kuhakikisha kwamba hajitetei na kwa bahati nzuri mbinu zake zote zimegonga mwamba katika kila hatua.
Sasa wametengeneza njama za kutaka kuilazimisha serikali kutoa hati ya kufuta mashtaka na mbinu hizi zinaratibiwa kwa karibu sana na Mabere Marando na kiongozi mwandamizi mstaafu aliyehudumu katika awamu ya Rais mwinyi. Walianza na kumdanganya mzee Mkapa kwamba hati ya kiapo atakayoiapa inatakiwa serikalini kwa ajili ya kufuta mashtaka kwa hati maalum (Nolle Prosequi) na kwamba haitakwenda mahakamani, baada ya mawakili wa serikali kukataa wakaitoa gazetini ili kuchafua jina la Mzee Mkapa. Ilisikika kwamba wanapanga kuandika barua kwenda kwa Rais Kikwete ili kuomba atoe ushahidi lakini nia yao ilikuwa ni kufanya hivyo na hatimaye kuipenyeza barua hiyo magazetini ili ionekane Rais anafanya kiini macho uendeshaji wa kesi ya Mahalu na ionekane Mahalu anaonewa au hakuna nia thabiti ya kushughulikia ufisadi. Mambo hayo yanafanywa na wanasheria hao kwa dhamira mbaya na ovu. lakini la kujuiliza hapa ni kwamba Je, Nolle itatolewaje wakati tayari mshitakiwa ameonekana ana kesi ya kujibu, ikiwa na maana kwamba ushahidi uliotolewa ulitosha kutia hatiani kama mshtakiwa hatatoa utetezi? Na sasa hata maamuzi ya Mahakama ya Rufaa yamebainisha wazi mazingira ambayo Nolle inaweza kutolewa na kesi hii haijazingatia mazingira hayo. Walitaka itokee hivyo ili huyo huyo Marando asimame jukwaani akidai kwamba serikali inahadaa watu kuhusu vita vya ufisadi.
Wanajaribu kuunganisha hilo na Hansard inayomnukuu Rais (wakati huo akiwa waziri) akitetea kwamba ununuzi huo ulikuwa halali na uliozingatia sheria ili ionekane kwamba hata yeye alimsafisha. Lakini kilicho wazi ni kwamba Rais aliyatamka hayo kabla ukweli wa skati hili haujabainika na Rais alizingatia nyaraka zilizokuwepo wakati huo. Baadae ilipokuja kupatikana taarifa ya ufisadi na uchunguzi kufanyika ndipo ilipobainika kwamba taarifa za mwanzo hazikubainisha ukweli huo.
Mpango huu wa kupeleka habari hii kwa Mwana Halisi, ulipangwa na unajiuliza kwa nini Marando huyo huyo aliyeandaa barua hiyo aifikishe gazetini kabla hata huko Ikulu haijafikishwa! Hapa kuna siri kubwa na uovu wa hali ya juu.
Labda siku ukionewa wewe ndo utajua utamu wa kuonewa ladha yake nini. Huyu Profesa alipewa POA (Power of Attorney) afanye ununuzi kama alivyoelekezwa ( kuzingatia maslahi ya Taifa, mwenye nyumba alitaka hivyo na kinyume cha hayo angeuza kwingineko) sioni issue ya taaluma yake hapa inahusikaje. Wewe unafikiri wapiganaji wanaouwa maadui vitani hawajui kuua ni haramu? Achenu unafiki. hapa si9gusi ussue za moral na ethic codes.
Mbopo umetumwa?