Ripoti ya CAG imezimwa kama gazeti la udaku. This is Tanzania Bana, unaiba Leo unaambiwa subiri tutakujadili kikao kijacho cha Bunge

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
873
4,063
Ripoti ya CAG imeshazimwa, kelele zimeisha tunasubiri ripoti ijayo tuone tumeibiwa kiasi gani tena. That's how life goes in Tanzania. Maisha ya vimemo nakujuana.

Lakini haya kwanini yanatokea? Yanatokea Kwa Sababu irregularities nyingi zinatokana na matamko ya viongozi wakuu wa nchi na hivyo likiaribika wao wanashindwa kukwepa lawama.

Sheria inasema hivi then Mawaziri au mabosi zao wanaelekeza hivi na vile, ikitokea tatizo wanaambiwa ninyi ndio mmetufikisha hapa.....ukimya unatawala.

Lakini pia wanaosababisha hoja za billions wote Wana kinga ya kuishtakiwa so Nani anachunguza MTU mwenye kinga?

Mkapa pekee ndiye Rais aliyekubali uchunguzi ukafanyika Bila kuweka mashinikizo dhidi ya utawala wa Jk nakuruhusu kesi ya Costa Mahalu ifike mahakamani na yeye akaenda kutoa ushahidi. Waliobaki wakisikia kuna uchunguzi unawahusu hata kama wanakwenda kuwa mashahidi lazima wazima uchunguzi.

Mwisho WA siku namwona CAG kama mbadhirifu Kwa Sababu anatumia billions kuchunguza na kufanya ukaguzi huku akijua wazi ripoti zake hazina tija kwenye mfumo tuliopo.
Ningekuwa yeye ningeacha kufanya ukaguzi nikaelekeza fedha nilizopewa zikajenge hospitali.
 
Suala la ushoga limekuzwa kuzima wizi wa serikali!!

Watawala wanajua Wadanganyika ni vichwa maji,wapige matukio tu!!

Huku mtaani jirani akipiga kelele za mwizi,tunatoa ushirikiano wa kupiga,kuchoma Moto na saa nyingine kuua ambapo kibaka anaweza kua amekwapua kajisimu ka shs laki tu Ila majizi yanakwiba mabilion,tunawaona mashujaa na tunawatizama tu!!
 
Wakati Abdul Nondo anaandaa Maandamano ya kushinikiza, Mapolisi ya CCM yamemshukia kama Kinyama cha Mwitu.

Sijaona Watanzania wakiongelea na kukemea Serikali kwa uonevu na wizi unaofichwa fichwa huku wale tuliowakabidhi Mamlaka wako bize kukaribishana Futari na kutucheka kuwa wanakula hela ya Wajinga yaani Watanzania.
 
Majizi yanakusanya pesa za kuhonga 2025.
 
Ripoti ya CAG imeshazimwa, kelele zimeisha tunasubiri ripoti ijayo tuone tumeibiwa kiasi gani tena. That's how life goes in Tanzania.
Ripoti ikishasomwa inakabidhiwa bunge.
Bunge linaikabidhi kamati ya hesabu za serikali kuu PAC.
PAC itaita waliotajwa kwa ubadhirifu na pia CAG anaitwa kuclarify changamoto alizopata.
Baada ya kumaliza scrutiny zao ndio wanaandaa mapendekezo na kuyapeleka bungeni.
Ripoti ya CAG Sasa inajadiliwa na wabunge wanapitisha mapendezo ya hatua za kuchukuliwa.

So utaratibu ndio huwa upo hivo miaka yote. Tatizo huwa tu mapendekezo yanakua legelege sababu PAC kwa Sasa ipo chini ya CCM so tusitegemee hatua kali kuchukuliwa. Otherwise kikanuni bunge liko sahihi kujadili ripoti ya CAG kwenye bunge lijalo. Labda Cha kushauri ni kwamba ripoti isiwe inatolewa mpaka muda wa kujadili kufika kuliko hii ya Sasa ripoti inatoka Mapema wakati kisheria muda wa kuijadili Bado.

Cc Kalamu
 
Asante sana kwa ufafanuzi huu mujarab! U must be one of them!
 
Ripoti itajadiliwaje na bunge kabla ya kamati ya PAC?
Tuliona haya hata wakati kamati hii ikiongozwa na Mwami Zitto.
Waacheni wenyeviti wa kamati hizi toka genge la Covid 19 Mdee na Kaboyonga wafanye yao.
Ikitokea Covid 19 wamefutwa ubunge itakuwa sababu isijadiliwe mwaka huu.
 
Suala la ushoga limekuzwa kuzima wizi wa serikali!!

Watawala wanajua Wadanganyika ni vichwa maji,wapige matukio tu!!

Huku mtaani jirani akipiga kelele za mwizi,tunatoa ushirikiano wa kupiga,kuchoma Moto na saa nyingine kuua ambapo kibaka anaweza kua amekwapua kajisimu ka shs laki tu Ila majizi yanakwiba mabilion,tunawaona mashujaa na tunawatizama tu!!
Tuko buzzy kupinga ushoga, maendeleo sio kipaumbelee chetu.
Lala Land.
 
Ripoti ikishasomwa inakabidhiwa bunge.
Bunge linaikabidhi kamati ya hesabu za serikali kuu PAC.
PAC itaita waliotajwa kwa ubadhirifu na pia CAG anaitwa kuclarify changamoto alizopata.
Baada ya kumaliza scrutiny zao ndio wanaandaa mapendekezo na kuyapeleka bungeni.
Ripoti ya CAG Sasa inajadiliwa na wabunge wanapitisha mapendezo ya hatua za kuchukuliwa.

So utaratibu ndio huwa upo hivo miaka yote. Tatizo huwa tu mapendekezo yanakua legelege sababu PAC kwa Sasa ipo chini ya CCM so tusitegemee hatua kali kuchukuliwa. Otherwise kikanuni bunge liko sahihi kujadili ripoti ya CAG kwenye bunge lijalo. Labda Cha kushauri ni kwamba ripoti isiwe inatolewa mpaka muda wa kujadili kufika kuliko hii ya Sasa ripoti inatoka Mapema wakati kisheria muda wa kuijadili Bado.

Cc Kalamu
Kwahiyo mijizi inaendelea kuwepo ofisini.
 
Imezimwa kwa kutumia "sheria na taratibu" zetu tulizojiwekea, ndio hata kama ni "sheria na taratibu" za hovyo zinazotoa nafasi kwa wezi kujipenyeza kwa wakubwa kutafuta msamaha ndio maana kila siku wanalindana.
 
Mmekuwa gaslighted na idara ya "propaganda" ya taifa kuhusu mashoga ,mkapotea kwenye reli..imeisha hiyo
 
Ripoti ya CAG imeshazimwa, kelele zimeisha tunasubiri ripoti ijayo tuone tumeibiwa kiasi gani tena. That's how life goes in Tanzania. Maisha ya vimemo nakujuana.

Lakini haya kwanini yanatokea? Yanatokea Kwa Sababu irregularities nyingi zinatokana na matamko ya viongozi wakuu wa nchi na hivyo likiaribika wao wanashindwa kukwepa lawama.

Sheria inasema hivi then Mawaziri au mabosi zao wanaelekeza hivi na vile, ikitokea tatizo wanaambiwa ninyi ndio mmetufikisha hapa.....ukimya unatawala.

Lakini pia wanaosababisha hoja za billions wote Wana kinga ya kuishtakiwa so Nani anachunguza MTU mwenye kinga?

Mkapa pekee ndiye Rais aliyekubali uchunguzi ukafanyika Bila kuweka mashinikizo dhidi ya utawala wa Jk nakuruhusu kesi ya Costa Mahalu ifike mahakamani na yeye akaenda kutoa ushahidi. Waliobaki wakisikia kuna uchunguzi unawahusu hata kama wanakwenda kuwa mashahidi lazima wazima uchunguzi.

Mwisho WA siku namwona CAG kama mbadhirifu Kwa Sababu anatumia billions kuchunguza na kufanya ukaguzi huku akijua wazi ripoti zake hazina tija kwenye mfumo tuliopo.
Ningekuwa yeye ningeacha kufanya ukaguzi nikaelekeza fedha nilizopewa zikajenge hospitali.
Tatizo ni katiba, kiongoz wa Nchi ana mamlaka yote ya kuamua nn kiwe despite sheria. Hili tatizo la kinga kwa Rais halaf kibaya zaid mzalendo na mtetea rasilimali za nchi akaja akawaongezea kinga wengine zaid 😪😪😪!! Hii Nchi inahitaji reshuffling kubwa san!!
 
Kwahiyo mijizi inaendelea kuwepo ofisini.
Ndio kanuni zenu hizo za CCM tokea 2009, hata kipindi Cha JPM ilikua hivo hivo ripoti inatoka alafu mapendekezo yanasubiri bunge la baada ya bajeti hukoo in fact zamani ilikua bunge la January kabisa. Nashangaa watu mapovu ilihali miaka yote ipo hivi, lazima watuhumiwa wajitetee mbele ya kamati na ndio inayokula muda maana kesi Moja Moja mpka ziishe siku 90 plus
 
Imezimwa kwa kutumia "sheria na taratibu" zetu tulizojiwekea, ndio hata kama ni "sheria na taratibu" za hovyo zinazotoa nafasi kwa wezi kujipenyeza kwa wakubwa kutafuta msamaha ndio maana kila siku wanalindana.
La kwanza, ripoti ni ya 2021/22 Ina maana huu ufisadi wote ni mpaka June 2022 Ina maana tayari mwaka umeshapita tokea ufisadi ufanyike so ni Yale Yale tu if muda ndio issue.

La pili, Miaka yote utaratibu upo hivo mkuu, ripoti ya CAG haiingii floor ya bunge mpaka ipitie PAC Ili wasikilize pande zote then ndio wapeleke mapendekezo ya adhabu bungeni.

Sikiliza hiyo video utaona hapo Mawaziri mpaka wanang'olewa (Kina Msutapha Mkullo) ilikua baada ya PAC kumaliza kusikiliza hoja za CAG na hao watuhumiwa ndio wakaja na masharti ya waziri mkuu ajiuzulu au mawaziri waondolewe.

Tofauti ni kwamba tu PAC na bunge la enzi za JK sio sawa na la Sasa lililojaa machawa na chama kimoja pekee.
 
Ripoti ikishasomwa inakabidhiwa bunge.
Bunge linaikabidhi kamati ya hesabu za serikali kuu PAC.
PAC itaita waliotajwa kwa ubadhirifu na pia CAG anaitwa kuclarify changamoto alizopata.
Baada ya kumaliza scrutiny zao ndio wanaandaa mapendekezo na kuyapeleka bungeni.
Ripoti ya CAG Sasa inajadiliwa na wabunge wanapitisha mapendezo ya hatua za kuchukuliwa.

So utaratibu ndio huwa upo hivo miaka yote. Tatizo huwa tu mapendekezo yanakua legelege sababu PAC kwa Sasa ipo chini ya CCM so tusitegemee hatua kali kuchukuliwa. Otherwise kikanuni bunge liko sahihi kujadili ripoti ya CAG kwenye bunge lijalo. Labda Cha kushauri ni kwamba ripoti isiwe inatolewa mpaka muda wa kujadili kufika kuliko hii ya Sasa ripoti inatoka Mapema wakati kisheria muda wa kuijadili Bado.

Cc Kalamu
Uzuri wako mkuu 'zitto junior', huwa hupendi kubabaisha na kuzungumzia usichokifahamu vizuri (mara nyingi). Hapa umetoa somo sahihi kabisa.

Nami ninakubaliana na huo mstari wako wa mwisho, kwamba haina maana yoyote kwa waTanzania kuelezwa madudu/mapungufu yote yale siku CAG anapotoa ripoti yake. Ni kuumiza tu nyoyo za watu na kuamsha hasira nyingi za watu.
Na kwa siku hizi ni kama hatua hiyo ni kichocheo/darasa kwa baadhi ya watu kutamani na wao wapate mahali pa kukwapua. Huu ni utamaduni unaojengeka na hatmaye itakuwa kama ndiyo tabia ya nchi yetu ya kutamani kupata fursa ya kukwapua mali za wengine.

Na inakuwa mbaya sana inapoonekana wanaodaiwa kukwapua hata hawachukuliwi hatua yoyote, na baadaye hakuna maelezo yoyote yanayofuatia hatua hiyo ya madai ya kukwapua.

Napendekeza, pawepo na utaratibu, hiyo ripoti ya CAG ikishapitia hatua zote, na kama kuna waliobainika kuhusika na ukwapuzi, basi iwepo pia hatua ya kuwasilisha kwa wananchi matokeo ya uchambuzi wa ripoti ya CAG, hatua kwa hatua.
Wananchi wanayo haki ya kujua usalama wa mali zao, na wanaovuruga usalama huo wote washughulikiwe kisheria bila kuoneana aibu.

Tanzania tunaelekea kubaya sana kuhusu ufujaji huu wa mali za wananchi. Kuna umuhimu wa kuiga baadhi ya nchi wasiofanya mchezo na tabia ya namna hii.
Unajua, waChina ni wezi sana, kama unavyowaona baadhi yao wanapokuja huku. Kule kwao wanajua mchezo huo hauvumiliki, na hawathubutu kukwapua hovyo hovyo.. Kuna umuhimu na sisi tujifunze jinsi ya kushughulikia tatizo hili.
 
Wakati Abdul Nondo anaandaa Maandamano ya kushinikiza, Mapolisi ya CCM yamemshukia kama Kinyama cha Mwitu.

Sijaona Watanzania wakiongelea na kukemea Serikali kwa uonevu na wizi unaofichwa fichwa huku wale tuliowakabidhi Mamlaka wako bize kukaribishana Futari na kutucheka kuwa wanakula hela ya Wajinga yaani Watanzania.
Umenena mkuu,watanzania ni wa kulalama tu hasa humu JF, Ile push back hawana ila ni wabobezi wa kujadili yanayotokea Sudan, Uganda, it's craze mkuu
 
Unajua, waChina ni wezi sana, kama unavyowaona baadhi yao wanapokuja huku. Kule kwao wanajua mchezo huo hauvumiliki, na hawathubutu kukwapua hovyo hovyo.. Kuna umuhimu na sisi tujifunze jinsi ya kushughulikia tatizo hili
Ni kweli sema tatizo huku tuna ushabiki wa kisiasa. Unakumbuka issue ya Makinikia lawama zikawa kwa Lissu mara msaliti mara anatumika yaani kesi nzima ya Trillion 400 ikawa kama vile Lissu ndio alisign mikataba!!

Ikaja kesi ya uhujumu uchumi, ona wote waliokamatwa ni wale tu waliokosana na utawala ila wale waliokua mafisadi ila yapo ndani ya mfumo kesi haikuwahusu eg wezi wa Escrow, mafisadi ya Makinikia, wezi wa mabilioni ya NIDA, wezi wa mabilioni ya electronic passport!!

Ikaja issue ya madawa ya kulevya, nikashangaa wanaotajwa ni Mbowe sijui Gwajima yaani watu ambao ni anti government. Same to issue ya kutelekeza watoto akatajwa Lowassa na Msigwa!!

So hata hiyo issue ya kunyonga mafisadi ikija usishangae wanaonyongwa ni Mbowe na Lissu kwa kile kitakachoitwa wizi wa ruzuku ya chama!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom