Kikwete: Kimatendo unaishi kwa tundu lissu, kwa maneno unampinga, why? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Kimatendo unaishi kwa tundu lissu, kwa maneno unampinga, why?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Nov 25, 2011.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimetoka Uwanja wa Taifa kuangalia mpira, bahati mbaya nimeshuhudia kituko kikubwa. Ulipigwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar, Bendera yao ikiwa imepandishwa. Kesho Timu ya Kilimanjaro Star nao wanacheza. Je watatumia wimbo gani na Bendera gani?. Timu ya Zanzibar ina kocha wao, Timu ya Kilimanjaro Stars ambayo kimsingi ndiyo ya Tanganyika ina kocha wao. Na Timu ya Taifa unapochanganya timu zote Zina kocha mmoja. Kilimanjaro Stars kesho hawatatumia gari iliyotolewa na NMB, iliyoandikwa Taifa Stars, maana yake ni kuwa hiyo ni gari ya Timu ya Taifa ya Tanzania, hivyo hairuhusiwi kutumiwa na Timu ya Tanganyika. Kama kwa maisha ya kawaida kimichezo mnakubali serikali tatu, nini kinawafanya CCM chini ya Mwenyekiti Kikwete kumtukana Msemaji wa kambi ya Upinzani kwa masuala ya Sheria na Katiba anapotaja Serikali Tatu? . Kama Kesho bendera ya Taifa itatumika, maana yake hakuna bendera ya Tanganyika. Kama wimbo utakaopigwa ni wa Taifa, maana yake Tanganyika haina wimbo wa Taifa. Imepitwa na Zanzibar ina bendera yake, wimbo wake, na Taifa linalojitegemea katika Muungano wenye kasoro. CCM Mnakataa serikali tatu kisiasa kwa kuwa mnanufaika kwa ubinafsi ila SIMAMENI SEMENI NINI MAANA YA HUU MKANGANYIKO-Wana JF nipeni mawazo
   
Loading...