Nani anasema CCM Mgombea Urasi wa CCM hana mkono katika hizi meseji.... Ushahidi wa kimazingira huu hapa: Uki-fatilia domain 6telecoms.co.tz, iliyotumika utaona wazi share the name IP ya Kikwete2010co.tz na JK web site yake na nyingine za mafisadi wa papa ziko hosted nao.
Angalia maandishi mekundu!
"
Kikwete2010.co.tz is a domain controlled by two name servers at co.tz. Both are on different IP networks. The name server kikwete2010.co.tz stated in SOA record is not in the list of name servers. Incoming mail for kikwete2010.co.tz is handled by two mail servers also at co.tz. Both are on different IP networks. kikwete2010.co.tz has one IP number (41.77.226.253).
212.233.84.in-addr.arpa, 229.77.41.in-addr.arpa, 228.77.41.in-addr.arpa and 227.77.41.in-addr.arpa share name servers with this domain. 6telecoms.co.tz share mail servers with this domain.
Kikwete kuanza kuzungumzia maneno ya uchochezi ya kumwaga damu siku moja baada ya kusambazwa inaashiria kitu gani? Lini kafanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa si maneno ya kubuni. Je tukisema anahusika na kuyaandaa ili aje kuyatumia kisiasa tutakuwa tunamwonea?
Inaonyesha amemaliza ahadi zote na kuanza kujiingiza kwenye siasa za maji taka kama katibu wake Mkuu. Ndugu wana jamvi mimi nina wasiwasi na Kikwete kuwa ni mmojawapo wa walioandaa maneno hayo kwa jinsi alivyoyachukulia upesi upesi na kuanza kuyatumia majukwaani.
Mkulu kanasa kwenye mtego alioutega
Mungu atunusuru
Hata mimi nimeshangaa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawaonya wafuasi wake kuwa wapinzani wako tayari kumwaga damu. Kama kweli Kikwete ni mcha Mungu basi amwogope sana Mungu wake. Neno damu linatisha masikioni mwa watu. Kadiri anavyolitamkatamka litaanza kukomaa miongoni mwa raia na hatimae watu wakajiandaa kumwaga damu. Dr Slaa usijiingize sana huko kwa kuwa Mungu ni mwema sana kiasi kwamba mawazo ya Kikwete si mawazo ya Mungu. Na vita ya ukombozi wa mwanadamu siyo vita yako Slaa, ni vita ya Mungu mwenyewe kwa kuwa ameona watu wake wanavyozidi kuangamia. Mbinu chafu hazitashinda bali kweli na haki itasimama milele. Mungu tupiganie na taifa lako litasimama.
Pole, usijali yatakwisha haya siku moja.Haitakuwa sahihi na wala haki kulinyamazia hili la JK kudai kusoma taarifa za gazeti fulani(angelitaja walau) kwamba kuna watu wanatishia kumwaga damu. Ningekuwa na uwezo ningewakutanisha wapinzani wote tuandae maandamano ya amani kupinga kauli ya JK na kumtaka kama Raisi ambaye bado yuko madarakani hadi 31 Octoba, kumchukulia hatua huyo ambaye anatishia amani ya taifa hili. Ningefanya hivyo mapema kabla ya uchagui kuhakikisha hali hii tete haitatokea (pre-empty the situation). Lakini uwezo huu maskini sina!
Hizo message anatuma yeye sio anajua zinakotoka, hii sio coincidence, yaani message leo kesho anatamka hayo hayo, kuna walakiniAkihutubia mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea jana, Jumapili, Oktoba 10, 2010, Rais Kikwete amewasuta wanasiasa ambao wamekuwa wanatishia umwagaji wa damu nchi kama hawakufanikiwa kushika nafasi za uongozi wanazozitaka.
"Sisi ni CCM. Sisi ni chama kisichohubiri umwagaji damu. Sisi ni chama cha amani. Umwagaji damu hauna maslahi yoyote na wala tija kwa yoyote isipokuwa kwa wanasiasa wanaotaka kutumia maiti za watu kama ngazi ya kuingilia Ikulu," amesema Rais Kikwete na kuongeza:
"Hawa siyo watu. Hawana maana yoyote. Achaneni nao watu wa namna hii wanaotaka kupata madaraka kwa ngazi ya maiti za wananchi wasiokuwa na hatia."
Amesisitiza Rais Kikwete: "Wanachochea watu wamwage damu na wao wapande ndege kwenda zao Ulaya na kuwaachia nyie mkitoana damu."
My take: Haya ni maneno mazito kutamkwa na kiongozi hasa rais wa nchi. Kikwete kama rais alitakiwa akemee message hizo na wanaozisambaza kwa kuwa zinachonganisha watu badala yake yeye bila kufanya utafiti kama yaliyotamkwa ni ya kweli au la anaanza kuzitumia kama mtaji wa kisiasa. Inawezekana anajua zinakotoka.