Kikwete: I can turn Tanzania into heaven if I get a billion dollars a month

Rais wetu kajitahidi kujenga hoja.. ila Revenue ya $1Bn. a month naona iko over-ambitious unless tuongeze na kupanua tax base...

Kwani BUDGET ya sasa ni ngapi? sio 12trilion? Je hii ni Billioni ngapi? nadhani ni more than 0.75 bil.
Kafanya nin jk, Kutwa safari.
 
Hata kama JK ni tajiri wa mali, namna yake ya kuwaza ni ya kimaskini!

Ni haramu kwa mtengeneza majeneza kulalamika kwamba watu wanakufa sana, ni vipi sie tulalamike jirani ana njaa ilihali njaa yake ni fursa kwetu?
 
Well, $1bn@Month=$12bn. In TZs that is around 19.2trillion per year. Our budget now is around TZs 13.5trillion, just 5.7trillion short of Kikwete's wishes. According to JK he just need 5.7trillion TZs to turn our country into 'heaven'. Ridiculous! Tax exemptions 1.2trn. Embezzlements 4.5trillion.

He simply doesn't get it. How the hell did we get JK as president? He is a disgrace to our country.
 
Well, $1bn@Month=$12bn. In TZs that is around 19.2trillion per year. Our budget now is around TZs 13.5trillion, just 5.7trillion short of Kikwete's wishes. According to JK he just need 5.7trillion TZs to turn our country into 'heaven'. Ridiculous! Tax exemptions 1.2trn. Embezzlements 4.5trillion.

He simply doesn't get it. How the hell did we get JK as president? He is a disgrace to our country.

Mkuu! this guy is a real joker! he has got no clue!! mmhh wait! i am told that he is an economist??
 
Kamakabuzi,

..U read my mind.

..lakini ukiendelea kumsoma u will come to a conclusion kwamba he doesnt get it.

..JK anaona uhaba wa chakula Kenya ni tatizo kwetu wa-Tanzania, badala ya kuona kuwa ni opportunity[market] ya sisi kuweza kuwauzia chakula na kupata faida.
JokaKuu hapo nadhani hujampata JK, Kakubali ana challenge katika paragraph ulomuelewa hivo, ila kaongeza the below... Kueleza as much as ni challenge pia ni opportunity na akaongeza kua ita create an impressive number of vacancies.... Issue sio what Kikwete has said in the Speech, He usually is good sababu the guy anajua kujipanga kwa speech za kukosha.

Tatizo ni kwamba hayo ambayo yapo ndani ya uwezo wake anafanikiwa to what extent? Hii nilomqoute EMT, Inatoa an overview ya mawazo ya JK kwa wananchi wake.... Na ni nzuri... Ila shida ni kuwa ni maneno tu. Ikwapi "Kilimo Kwanza"?

Kwa maelezo na utambuzi alo nao juu ya umuhimu wa Kilimo.... we ask ourselves why the failure? Then we ask an hypothetical question basing on his hypothetical billions.... Does he think only money is the answer to sector ya kilimo kuweza simama Tanzania?

Mr. Kikwete sees in this challenge an opportunity. He has instructed the Ministry of Agriculture to increase production of food, particularly corn and rice, to have enough to feed Tanzanians, as well as export. His government set up the Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania in a part of the country that gets the most rain and has ideal soil and climate conditions. If all goes according to plan, the corridor will create 420,000 jobs and produce an annual income of $1.2 billion. "If we can succeed, we will lift millions and millions of people out of poverty very quickly," Mr. Kikwete said..
 
Kwani lazima kuongea kila tunapokuwa mbele ya kadamnasi? Haisaiidi mtu kama unaongea bila kujielewa...misamaha ya kodi mwaka uliopita mpaka ilikuwa inatisha. Halafu we dream of collecting US$ 1 billion a month....sasa hawa marafiki zetu ambao kwa kweli ni wafanyabiashara uchwara watafanyaje biashara?
 
Rais wetu kajitahidi kujenga hoja.. ila Revenue ya $1Bn. a month naona iko over-ambitious unless tuongeze na kupanua tax base...

Mkuu kabla ya kuiweka hiyo article hapa niliisoma mara tatu lakini sikuona hoja ya Rais. Wataalamu wanasema kuwa asilimia 80 ya matatizo yanasababishwa na mfumo wa uongozi. Kwa maana ya kuwa yanatengenezwa na mfumo uliopo, ambapo asilimia 20 hutokana na sababu nyingine.

Kwa hiyo basi hata kama akipewa hizo dola bilioni moja kila mwezi, sidhani kama ataifanya Tanzania kama mbingu. Tatizo la Tanzania sio pesa. Pesa zipo, resources tunazo kibao tuu. Tatizo kubwa tulilo nalo ni mfumo wa uongozi. Pesa bila mfumo mzuri wa uongozi Tanzania haitaweza kuwa kama paradiso.
 
Huyu rais ana maajabu kweli, hata kuzalisha chakula ndani ya nchi yako unaenda kuomba msaada kwa wazungu wakutatulie tatizo la njaa?? Hajui tu kuwa wazungu wanamcheka sana kwa ardhi yenye rutuba aliyonayo na rasilimali zilizopo ni mtaji tosha wa kumaliza njaa. Uvivu wa kufikiri na ufisadi wao ndani ya ccm ndio chanzo cha njaa.
Unashangaa hilo? Unasahau alihongwa suti? Ule wakati wa kujisifia na kujivunia kuwa "Mimi ni Mtanzania" umepita.
 
Kweli ni aibu kuwa mwafrika sasa mbona viongozi wetu wanatudharirisha hivi. Kweli msafara wa watu 16 unaweza kumshauri baadhi ya haya mambo, aibu kwa tanzania kuomba msaada kwa ajiri ya kupigana na njaa kilimo kwanza wakulima wanapelekewa mbolea ya kupandia na mbegu wakati wa kuparizi mahindi, sisi tunaitaji watalamu wa kilimo ambao watasimamia kilimo sio fedha kwa mfano kapunga rice baada ya serikali kukabizi ule mradi umekufa wale wajapan wakija kuona ule mradi hawataamini pili kilimo uyole kipindi wapo wazungu kulikuwa na ng'ombe, nguruwe na kuku wa mayai na nyama lakini baada ya kuondoka hakuna kitu tena. Rais aombe wataalamu wa kilimo sio fedha.
 
JokaKuu hapo nadhani hujampata JK, Kakubali ana challenge katika paragraph ulomuelewa hivo, ila kaongeza the below... Kueleza as much as ni challenge pia ni opportunity na akaongeza kua ita create an impressive number of vacancies.... Issue sio what Kikwete has said in the Speech, He usually is good sababu the guy anajua kujipanga kwa speech za kukosha.

Tatizo ni kwamba hayo ambayo yapo ndani ya uwezo wake anafanikiwa to what extent? Hii nilomqoute EMT, Inatoa an overview ya mawazo ya JK kwa wananchi wake.... Na ni nzuri... Ila shida ni kuwa ni maneno tu. Ikwapi "Kilimo Kwanza"?

Kwa maelezo na utambuzi alo nao juu ya umuhimu wa Kilimo.... we ask ourselves why the failure? Then we ask an hypothetical question basing on his hypothetical billions.... Does he think only money is the answer to sector ya kilimo kuweza simama Tanzania?

"Pesa sii msingi wa maendeleo"maneno ya nyerere. huyu jamaa bogus kabisa

Kuna article moja niliisoma kwenye gazeti la Raia Mwema kwa jina "Nini kitatatua matatizo yetu" ilibidi nikaitafute. Article yenyewe inasema:

"Hatukuwahi kujadili falsafa nyingi kama taifa kwa sababu tulikuwa katikati ya vuguvugu la kutaka kujitambua, kujitawala na kuondoa ujinga, maradhi na ufukara. Kwa mfano, tulihubiri kama kasuku; "pesa si msingi wa maendeleo bali ni rasilimali watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora". Kwa kuwa hatukuelewa mantiki ya dhana hiyo, leo hii tunaamini kama dini kuwa pesa ni msingi wa maendeleo. Bila pesa hakuna kinachowezekana.

Waliotutangulia walijua athari ya kutegemea pesa kama msingi wa maendeleo hasa kwa sababu hatuna udhibiti na pesa wala sera zake, bali tuna rasilimali zetu. Je, tufanyeje ili ziweze kukidhi mahitaji, matakwa na matarajio yetu? Utamaduni wa mfumo pesa ni kuhakikisha kila kitu kinauzwa kwa faida, na kama huna uwezo wa pesa itabidi ukakope, ulipe kwa riba na mfumko wa bei utakua ni jambo la kudumu kwa sababu kila anayeuza bidhaa au huduma lazima apate faida. Kwa maana hiyo iwe ni nchi au mtu binafsi daima utakua na nakisi katika bajeti yako na utakuwa mtumwa wa pesa.

Katika uchumi uliojikita katika fedha hakuna haki wala kuaminiana. Eti mwenye duka la mikate akwambie yeye hauzi mikate mizuri kisha akushauri ukanunue kwa jirani yake ndie mwenye mikate mizuri. Uadilifu wa kiwango hiki haupatikani katika mfumo fedha unaolenga faida, na ni vyema uache kabisa biashara!

Kwa hiyo ushindani unazalisha mila na desturi kama vile ufisadi, unyonyaji, udhalilishaji na hata watawala wachache wenye nguvu ya pesa. Kwa hiyo, mfanyakazi akifukuzwa kazi kwa vile tu kuna mashine ambayo inaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kwa gharama za chini hiyo si tabia ya kifisadi.

Ni sawa tu kwa mfanyakazi huyu mwenye familia akahangaike, baadae awe mhalifu atupwe jela, na familia yake ivuruguke. Au wananchi wafukuzwe kwenye ardhi yao kwa sababu wataalamu wamegundua kuna dhahabu, kwa hiyo wenye mamlaka na madaraka wananunua vitalu ili kesho waingie ubia na wawekezaji. Kwa nini wananchi katika kijiji hicho wasiwe ndio wabia na huyo mwekezaji? Kwa falsafa za Azimio la Arusha hiyo ni tabia ya kifisadi kwa kuwa haizingatii haki, usawa, utu na huruma ni unyamaunyama tu.

Siasa katika mfumo wa pesa pia inazaa utamaduni mwingine kwenye demokrasia, kwani katika masuala ya uchaguzi lazima pesa itumike kwa ajili ya matangazo na kadhalika. Katika hali hiyo inakua ni udikteta wa wachache wenye fedha au wenye wafadhili. Ile imani kuwa ukichagua viongozi wenye maadili basi uko salama ni adimu katika mfumo wa pesa ni msingi wa maendeleo. Kwa hiyo haijalishi chama gani kitaendesha serikali, kinachotokea ni kubadilisha watawala kama ilivyo Marekani, unachagua ama simba au nyoka.

Miaka 25 baada ya Azimio wengi tumejifunza mengi na bado tuko katika mshituko kwa kuwa hatuelewi kinachoendelea. Kila mtu na hasa viongozi na watendaji tuliowapa dhamana wamebadilika kwa mawazo, maneno na matendo. Lugha yetu imebadilika kwani siku hizi hapendwi mtu ni pesa, cheza na mwili wangu lakini sio pesa zangu, wawekezaji si makabaila, wabia katika maendeleo sio mabeberu, mpango wa kupunguza umasikini sio mpango wa matumizi bora ya rasilimali kuondoa ufukara. Kwa kifupi Watanzania wengi wanamfadhaiko, wamechanganyikiwa, wananyanyasika na kukata tamaa. Je, nini kitatatua matatizo yetu ni siasa, dini, ubunifu au pesa?

Dalili zote zinaashiria hali haitabadilika kama Watanzania na Waafrika kwa jumla tutaendelea kukataa kuwa hatujachanganyikiwa na kwa hiyo tutafute kiini cha tatizo. Hatuwezi kula pesa iwapo hatutazalisha chakula cha kutosha au wenye chakula wakikataa kutuuzia. Tutasaga meno pale watakaposema pesa zimefutwa sasa tunatumia dhahabu, au almasi wakati tumebakiwa na mashimo tu. Wanasiasa hawawezi kutatua matatizo yetu kwa vile ni wapiga debe, hawana muda wa kutafakari, hawana weledi na wataalamu ambao wangewasaidia wamegeuka wanasiasa, wengine hawana weledi na wanafukuzia pesa.

Chanzo: Raia Mwema - Nini kitatatua matatizo yetu?
 
Back
Top Bottom