Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Fairplay hata udaku ni habari !
Mimi naisubiri sana Part 2 maana Jamaa anaonekana kama ni mtu wa system ndio maana anasema jina la Shein Jk alishindwa kulitaja mara 2 wakacheka ! Story tamu sana mpaka nasisimkaaa !
 
wana bodi naomba msione nimerukwa akili,kwa uwezo huu wa kufikiri wa Rostam,napendekeza tumpe nchi yeye mwenyewe!
Mtazamo, tumpe mara ngapi?. Yeye ndiye "The King Maker" aliyemuweka JK kwa zile fedha za Kagoda na sasa ndiye anayemweka EL mwaka 2015!. There is nothing we can do!.

Msiomkubali Lowassa, nawashauri bora mkubalini tuu vinginevyo!.
 
Weee Pasco mhuni sana yaani... uwe karibu unukie manukato au sio?.. unajua kusema kweli una point nzuri sana maana maisha ya leo na umaskini huu unapopiga kelele za mlangoni au kunadi salaa alfajiri ambyo kwao ni usiku wa manane unawachosha waliolala.. Kubakia peke yako inakupa wakati mgumu sana pengine kweli inabidi watu tujipange nyuma ya Lowassa maana kufa maskini nako kazi!!!! Haaa! haaa! haa!
 
Kwa mfumo wa TISS na utawala wa nchi ulivyo JK anajua kila kitu kinachoendelea kila siku. JK anaweza kuwa sehemu ya mtandao huo ama la. Kama rais mwenye busara ameamua kutojionesha yupo kundi/mtandao gani. Hii itamsaidia akae aangalie upepo kama alivyofanya mzee Mkapa pale 2005 jioni kabisa aliposema tuchague rais kijana (akimlenga JK).
 
kwa style hii ya hadithi za siasa na uraisi kila kukicha MAENDELEO na Maisha BORA kwa watanzania ni NDOTO!
 

You are very very wrong !
 
Mtoa thread hii anajua mambo mengi sana na ambayo yako very useful kwa sisi wavimba macho na kwa MH.RAIS mwenye, ila kwa mtazamo wangu bado ana hofu ya nini kinaweza kumtokea kama atamwaga mboga yote anahofia kulala njaa. Ndio maana ukisoma kama thread inakosa muunganiko hivi but nafikiri tumtie moyo ili atupe maneno zaidi.

Nafungua macho na masikio rasmi.............
 
Kwa kweli JF naiogopa sasa!

Kumbe wakubwa wa nji hii mumo ndani humu!! Nakushukuru sana mkuu this is very interesting at least na sisi pangu pakavu tunaambulia tusiri twa nchi yetu!
 

Nahodha sidhani kama ataonekana kwenye medani za kisiasa baada ya 2015, ila Dr Mwinyi zamu yake itafika! na nadhani ataanzia Zanzibar baada ya hapo ndio atakuja bara !
 
kwa style hii ya hadithi za siasa na uraisi kila kukicha MAENDELEO na Maisha BORA kwa watanzania ni NDOTO!
Wakishaingia tu madarakani, shughuli ya kwanza ni kujitayarisha kwa uchaguzi unaofuata, ndo maniac cycle ya banana republic hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…