Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hutaki Unaacha, Dec 30, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Hutaki Unaacha

  Hutaki Unaacha Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mr President,

  Ningekuwa na muda ningekueleza mengi sana. Muda wangu ni kidogo sana ndiyo maana nashindwa hata kupost mambo mengi kuhusu taifa hili hapa JF. Ninatuma post hii si kwa lengo la kukutisha. Lengo ni kukukumbusha uwe makini ili usijefanya uamuzi wa hovyo na kuliingiza taifa katika machafuko na kuharibu timetable za watanzania. Machafuko ndiyo tunayoyakwepa lakini si wewe (I have to tell you the truth because you are not my breadwinner at all).

  Mtandao

  Ninachozungumzia hapa ni kundi kubwa na hatari linaloaminika kuongozwa na Edward, Rostam, Othman, Apson, Karume na Shein na Mkapa. Ninakufahamu vizuri sana na ungekuwa uwezo wako, hawa wote ungeweza kufanya uwezalo ili kumweka madarakani mtu unayemtaka kwa maana ya Asha au Nahodha. Huu ni mtandao unaofanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana. Ukitaka kuamini, jiulize swali la kipuuzi sana kuwa kwanini kila plans unazofanya (zisizo na faida) kwa kundi hili zote zimefail?

  1. Shein ni nani?

  Nataka nikukumbushe ''issue'' ya Omar Juma. Huyu alikuwa threat kubwa kwa kundi lenu kwa ajili ya 2005. Mtandao wake ukibebwa na Mkapa ulikuwa ni hatari sana. The only way ilikuwa ni ''kumwondoa'' na hilo liliwezekana. Siku nikiwa na muda nitaeleza mchezo wote ulivyofanyika. Wakati jina limeletwa tukiwa hotel moja maarufu hapa Dar, nakumbuka hukuweza kumfahamu Shein wala kulitamka jina lake vizuri. Ulikosea mara tatu kulitamka. Tukacheka wote. Hatimaye Shein akawa makamu wa rais.

  Baada ya wenzako kukuweka madarakani (mgombea ndani ya CCM), kosa ambalo Shein hataweza kukusamehe katika maisha yake (Mimi sio Mungu, kwani anaweza kukusamehe vilevile) ni pale ulipo-attempt kumfanya Zakhia kuwa makamu wa rais. Asingekuwa Edward, Rostam, Mkapa na Karume, leo hii Shein angekuwa mwenyekiti wa TPDC au TANAPA!. Kitendo cha Shein kuletwa na kundi hili, kutetewa na kundi hili achilia mbali kushawishiwa na kundi hili agombee urais wa Zanzibar ili kummaliza nguvu Nahodha chaguo lako kinamfanya awe mtiifu kwao kuliko hata kwa Mwanamwema!. Unafahamu vizuri Shein alivyoshinda urais Zanzibar, rafiki zako walikuchezea akili wakikuambia kuwa wamemleta Shein ili kupunguza kura za Bilal na ulipomkubali Shein wao wakaenda kumpigia Bilal kampeni wakijua kazi ya kumweka Shein imekamilika. Baada ya hapo uliendelea kumng'ang'ania Zakhia kuwa makamu. Mkapa akishirikiana na Rostam (ambaye alikuwa akim-install Bilal kuwa makamu huku yeye akiwa South Africa kuangalia World Cup) walimweka Bilal hapo alipo.

  Shein hakushinda uchaguzi Zanzibar. Kilichofanyika ni Mkapa, Rostam, Karume kumhonga pesa za kutosha sana Maalim kupitia kwa kijana wao hatari sana Jussa (kumbuka huyu aliletwa na Rosatm ili umteue awe mbunge). Today, umeshindwa kumweka mtu wako Zanzibar na makamu wa rais Muungano. Walichoweza kufanikisha ni kuiteka Zanzibar yote (Bilal na Shein). Nakukumbusha ya kwamba, ili uwe mgombea kupitia CCM, unahitaji Zanzibar na 'Lake Zone'. Kule 'Lake Zone' wamekushinda. Hilo unalifahamu vizuri. Hii ndiyo maana Wanzanzibar wamekutesa sana ndani ya CC iliyopita. Ili kukuonyesha kwamba hufai, Shein kampa udaktari wa heshima ''Baba yake'' mdogo Karume. Ninafahamu jinsi unavyojikosha kwa Anne kwa kumpa nishani ili kusiwe na vote of no confidence mwakani hasa kwa sakata la Richmond na Twiga. Napenda kumhakikishia Anne ya kwamba that's a strategy anayoitumia Mugabe ya kuwamaliza watu. JK ameiiga huko. Naomba Anne uwe makini sana. Waweza kufa kwa ''presha'' usipoangalia.

  2. Karume ni nani?

  Huyu alipigiwa kampeni kubwa sana na Edward na Rostam mwaka 2000 licha ya CCM Zanzibar kumkata jina lake. Kwa hili Karume hawezi kuwasahau hawa jamaa mpaka anakufa. Karume alikupinga Butiama. Yeye, Edward na Rostam wakaenda ku-design ''mwafaka'' wao wanaoujua ambao leo hii unafanya kazi Zanzibar. Nataka nikukumbushe mara ya pili kuwa Jussa aliletwa kwako na Rostam ili umpe ubunge. Think twice! Karume ndiye rais aliyeleta maendeleo makubwa Zanzibar. Shein will do more than what Karume did. Usishangae ukisikia Karume kuwa makamu wa Lowassa 2015!. Karume ana msimamo. Hayumbi na bahati mbaya sana hakuogopi.


  NITAENDELA SIKU NYINGINE WAPENDWA WANA JF
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nitapita baadaye hii yataka mda kidogo
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu unatisha'hii ni kweli?itafutwa sasa hivi ngoja ni save haraka
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huna Address ya Magogoni? Kikwete huwa hachungulii huku akipita anaweza kufa kwa presha za humu JF.
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu wewe ni nani'mwakembe au lowasa?hii naipeleka mbali kwa watanzania wote ndio kazi yangu
   
 6. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mungu wangu hii siri imevuja haponi mtu
   
 7. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Huu mzunguko mbona nimeshindwa kuuelewa? Aliyesoma akaelewa ajaribu kunisaidia ili na mimi nisiachwe nyuma. Nini chimbuko la waraka huu?

  Tiba
   
 8. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu hizi habari inaelekea unamjua vilivyo huyu Kikwete na mtandao wote, mwaga mboga mkuu sisi tutakula hata kama umemwaga kwenye michanga.

  Hii ni balaa mkuu mboga imeshaisha ongeza nyingine
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  "Hadithi" ni nyingi NCHI hii! JMK na Karume ni watu wa karibu sana tangu mwaka 2000. Walikuwa na adui yao mmoja wakati huo akiitwa Komandoo Salmin Amour ambaye alimfanyia kitu mbaya JMK kwenye Urais wa mwaka 1995. Haya mengine mapya tena. Yanaweza kuwa kweli kwa kuwa kwenye siasa za bongo hakuna rafiki wala adui wa kudumu.
   
 10. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  UPUPU wa kutaka kumchafua Lowassa na Rostam.

  Hata mkifanyaje tunawajua wala hatushikiki. Good story telling though.
   
 11. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wildcard

  Angalia watoto wanavyoshabikia hadithi hadithi.. LOL kumbe na wewe umemshtukia? ahahahahahah kila akiandika jina Lowassa linakua mdomoni.
   
 12. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,784
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  kama Jason bourne vile, ngoja nitafakari.
   
 13. s

  sarawati Senior Member

  #13
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  utaendelea lini mkuu..????imenichanganya sana hii habari.....
   
 14. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawa watu wa ajabu sana kila siku kujipanga kugombea madaraka kitu maendeleo kwa wananchi hakitamkwi tumechoka na thread hizi za watu wa mitandao na wenye uroho wa madaraka wakati umaskini unashambilia nchi na wanachi utafikiri kirus cha kompyuta au hiv
   
 15. condorezaraisi

  condorezaraisi JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona unawasaliti wenzio mnajadiri pamoja huko mafichoni ,wewe umeamua kuvunja ukimya ,asante hii ni very useful post :A S-coffee:
   
 16. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 867
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  mmh..asee..kama mafia nation.
   
 17. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mzee malizia na waliobaki ili tupate picha nzima na tuweze ku-connect the dots....... Otherwise TUMETHUBUTU, TUMESHINDWA NA TUSIPOANGALIA TUTAZIDI KUSHINDWA TUNAVYOSONGA.
   
 18. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #18
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Watanzania,

  Hivi kweli mnapenda story za udaku namna hii?.

  Kila siku huwa nasema na kusisitiza anzeni kufikiri kwa kutumia ubongo wenu acheni magazeti na mitandao kuwafikiria.

  Ndio maana mnalialia kila kukicha maisha magumu, hayawezi kuwa raisi kama mnaamini story ya kutunga kama hiyo hapo juu.
   
 19. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #19
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hutaki Unaacha, lini hiyo Part two inatoka? utuambie mkuu
   
 20. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Titans!

  Mambo ni mazito humu jamvini halafu kuna kila aina ya VEMPA humu!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...