VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Rais Kikwete hataachia Uenyekiti wa CCM Taifa. Akiachia, itakuwa aibu kwake hasa kuliko kwa chama. Atatumia kila awezalo ili asiachie. Hata hivyo, vita ya rafiki wake kipenzi ni ngumu. Lowassa ndiye anayetaka Kikwete aachie Uenyekiti kwakuwa 2015 anaweza kuwa kizingiti kwake katika kupitishwa kugombea Urais.
Lowassa hakati tamaa. Anaendelea kupambana hadi mwisho. Kurudishwa kwa Mangula ni dalili nyingine ya kusukumwa kwa Lowassa ili ashindwe. Akina Bashe wanamsingizia bure Membe.Wao wanajua fika kuwa Lowassa ndiye mhusika. Wao wamatumiwa kuwachonganisha Membe na Kikwete makusudi kabisa.
Lowassa anayajua madhaifu ya JK. Ndio maana anaweza 'kumchezea' atakavyo. Lakini mwisho wa siku,Kikwete atabaki kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa. Ingawa uongozi wake umedhoofishwa vya kutosha na kundi la Lowassa, bado anajikongoja. Lakini, JK anatia huruma. Sauti yake, hoja zake na sura yake ni ushahidi hata Mahakamani.