Ninaheshimu mawazo yenu wote lakini naomba tu kuwaza tofauti na ninyi kama hivi:
1. hawa jamaa walitumia njia nyingi za halali na haramu kwa zaidi ya Miaka 10 YAANI KABLA YA 1995 kujiandaa kuingia Ikulu,mara ya Kwanza Mwalimu Nyerere akawasambaratisha lakini kwa uzoefu wa kiaskari na suluba walijipa miaka 10 tangu hapo ya kujiandaa.
2.katika maandalizi yao haramu ama halali hawakuuhitaji ule mfumo rasmi uliopo wa kuweza kuingia Ikulu,yaani CCM na hata vyombo vingine.Walichofanya kama VIRUS wa UKIMWI, waliuzubaisha mfumo kias kwamba hawa jamaa walimshangaza hata Mzee wa Lushoto/Sea View/Nanyumbu akakuta hana njia ya kuwazima na mfumo wa kinga za mwili za serikali ukawa umeshaingiliwa kitaalamu wanasema immunity was compromised!
3.kwa kuwa kutawala kwa miaka hii ya sasa ni sayansi utaona kuwa EL alikuwa akifanya kazi ya kuzima moto labda kwa design au kwa kukosa uelewa,au kwa kuwa njia rahisi ya kufanya ufisadi usishtukiwe ni kuwa na majanga ya ajabu ajabu:mvua za kutengenezwa,richmond,madarasa fasta fasta,BARA BARA YA SHEKILANGO NA UPANUZI WA KI-UJIMA WA ALI HASSANI MWINYI ETI GARI MBILI KUELEKEA MJINI ASUBUHI NA MBILI KUELEKEA MWENGE JIONI,ni ishara tosha ya uongozi duni.Zingatieni kuwa mtu wetu EL anasema hata akirudishwa leo atafanya uamuzi richmond-shule za kata type!kura yangu ijapokuwa moja hawezi kupata!Ni kiongozi wa makabila ya ujima huko jirani na kilimanjaro lakini karne ya 21 ndiye siye!
3.Kutoka 2 hapo juu hawa jamaa hawakuwa na mfumo mpya waliotengeneza ama mkakati wa kututoa tulipoachwa na Mkapa.Hawakuwa na hata umoja kikazi kama serikali.Kama Rais anafika sehemu lilipovunjika daraja kabla ya waziri wa miundombinu tafsiri ni nini?japo daraja lile ni maeneo ya nyumbani kwa mtu.unaona ni wazi hakukuwepo na mpango wowote wa kukuza uchumi,kuongeza utoaji wa huduma muhimu wala kuongeza uwekezaji wenye manufaa kwa Watanzania.
4.Nione kwamba hata EL angekuwepo kwa Serikali ingeyumba tu maana msingi wake ni kama ile hadithi ya Biblia ya mtu aliyejenga nyumba yake mchangani ,mvua na mafuriko vilipokuja ilianguka!