Huyu baba anawazimu ooh sorry.Kwanini sheria hii aifanye kwa mbwembwe kulikosheria nyingine?kutakuwa kuna kitu anachofaidika nacho tu.Kama nchi inaongozwa kihivi basi hii litaifa halifai kuwepo duniani,Sheria nyingine zinatiwa sahihi kwa mbwembwe nyingine bila mbwembwe kwanini?
Hilo ni swali muhimu sana, lakini pengine nikukumbushe Gender Sensitive;
1.Huu ndiyo ule muswada wa sheria ambao wabunge waliupinga sana wakisema umechelewa kufikishwa hivyo usuburi hadi uchaguzi mkuu utakapoisha ili kufanya maandalizi ya kutosha. Waliugomea na kutaka uwasilishwe katika bunge lijalo ili hata kama wakiupitisha uje uanze kutumika katika chaguzi zijazo na siyo uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Sababu zao walidai, muda uliosalia ni mfupi kwa sheria hiyo kupitishwa na kuanza kutumika kwa vile inatakiwa kueleweka vizuri kwa wadau wote na hata walifikia hatua ya kuonya kuwa sheria hiyo ikipitishwa, wabunge na baadhi ya watu watafungwa kwa kufanya makosa kutokana na kutoielewa vizuri.
2. Lakini pamoja na kupinga mara kadhaa na kuugomea muswada huu bungeni, hatmae Bunge lilipitisha sheria ya gharama za uchaguzi, Februari 11 mwaka huu ambapo hata hivyo ulizua mjadala mkali kabla ya kupitishwa huku wabunge wakitoa mapendekezo ya kurekebishwa kwa vifungu kadhaa na vingine kuvifanyia marekebisho huku kampeni za chinichini zikielezwa kuanza katika majimbo mbalimbali ya uchaguzi.
Ukiangalia kwa makini sababu za JK kusema atausaini kwa mbwembwe ziko hapa. Wakati wabunge wanaugomea, akiwa katika sherehe za kuadhimisha miaka 33 ya CCM mnazi mmoja JK aliwalaumu wabunge kuwa wanafiki kwa vile wamekuwa wakilalamikia Rushwa lakini baada ya kupelekewa sheria hiyo wamekuwa wa kwanza pia kuipinga.
Kwa vile kupita kwa muswada huu kunatokana na nguvu kubwa ya JK na Pinda ilibainika kuwa kulikuwa na kundi la wabunge ambao walikuwa wakipinga kutokana na kudhania kuwa muswada huo umeandali kwa ajili ya kuwamaliza wao, hivyo kitendo cha kupita ni cha Historia kama alivyokiita yeye kwa vile anaamini huu utakuwa ndiyo Ulimbo wake wa kuwanasa na kuwabwaga wale wote ambao alikuwa akiwahitaji watoke katika mfumo wa ubunge na utawala.
Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa amefurahi kupita kwa muswada huo kwani sasa amewaagiza PCCB na hata Usalama wa Taifa waanze kazi ya kuwafuatilia wanaotoa rushwa. Hapa nadhani lengo lake kuwakamata wale waliokuwa wakimsumbua kwa sababu hiyo ya kisingiizo cha sheria huku akilipiza kisasi.
Hata hivyo siku moja kabla ya mkutano wa 18 wa bunge haujafungwa, muswada huo ulipita baada ya majadiliano makali, hasa katika kipengele cha kuwakirimu wapambe wa mgombea na kufanya marekebisho kadhaa.