Mongoiwe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 524
- 263
Nimetoka sasa katika Mkutano mkuu wa Mwanza wa Takukuru ambako Rais Kikwete alikuwa Mgeni rasmi hapa jijini Mwanza.
Kikwete wakati wa kufungua mkutano wa mwaka wa TAKUKURU, emeonyesha furaha yake kwa kupita mswada wa sheria ya fedha za uchaguzi katika bunge la 18 lililomalizika na kusema ni jambo la kihistoria.
Kikwete amesikika akisema kutokana na kupita kwa mswada huo basi zoezi la kutia saini sheria hiyo atalifanya kwa mbwembwe sana tofauti na miswada mingine ya sheria ambayo amekuwa akisaini kimya kimya.
Rais Kikwete mbali na kueleza furaha yake kwa kukupitishwa kwa sheria hiyo ambayo iligomewa na wabunge kupitishwa mara kadhaa, aliwaagiza TAKUKURU kuhakikisha wanaitumia kuwakamata watu ambao alidai kuwa tayari wameaanza kununua uongozi kwa kugawa mipira na kukarabati majengo ya CCM.
Namnukuu akiwaagiza TAKUKURU kuanza na uchaguzi huu wa mwaka huu: "Anzeni sasa kujipanga kuifanya kazi hiyo kwani naambiwa wanunuaji wa uongozi wameshaanza wengine wanapita na kuwagawa mipira na wengine wanakarabati majengo ya ofisi za CCM"
Alisema sheria hiyo iliyopitishwa itsaidia sana kudhibiti rushwa kabla na wakati wa kura za maoni ndani ya vyama vya siasa na wakati wa uchaguzi, na kueleza amefarijika na wenzake serikalini wakati watakapomaliza muda wao wa uongozi, kuacha wamejenga misingi imara ya utawala bora, demokrasia na maadili ya viongozi wa Umma, kwa sheria hiyo kutekelezwa.
Hata hivyo amekiri rusha katika kura za maoni CCM kushamiri, amesema: "Rushwa kubwa kwenye uchaguzi ipo wakati wa kura za maoni katika vyama pengine hata kuliko wakati wa uchaguzi wenyewe".
Ametoa ahahadi: "Mimi niko tayari kufanya kila linalowezekana ili kuiwezesha Takukuru kufanikisha kazi ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi nchini na nawataka muanze sasa na uchaguzi ujao".
Akionekana kugusia suala la Jerry Muro alisema: "Rushwa ipo katika sekta binafsi huko pia kuangalieni, kwani wakurugenzi na watendaji wa sekta binafsi wanafanya hivyo katika ajira, kutafuta masoko na zabuni. Bahati mbaya sana hata waandishi wa habari nao hawako salama katika kadhia hii, tena wanaoandika sana ndiyo nao wamekuwa wakipokea rushwa, rushwa ipo kila mahali ombi langu sote tuhusike na kuhusishwa katika mapambano haya".