Kikwete azungumzia sheria ya fedha za uchaguzi


Mongoiwe

Mongoiwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
523
Likes
106
Points
60
Mongoiwe

Mongoiwe

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
523 106 60
Nimetoka sasa katika Mkutano mkuu wa Mwanza wa Takukuru ambako Rais Kikwete alikuwa Mgeni rasmi hapa jijini Mwanza.

Kikwete wakati wa kufungua mkutano wa mwaka wa TAKUKURU, emeonyesha furaha yake kwa kupita mswada wa sheria ya fedha za uchaguzi katika bunge la 18 lililomalizika na kusema ni jambo la kihistoria.

Kikwete amesikika akisema kutokana na kupita kwa mswada huo basi zoezi la kutia saini sheria hiyo atalifanya kwa mbwembwe sana tofauti na miswada mingine ya sheria ambayo amekuwa akisaini kimya kimya.

Rais Kikwete mbali na kueleza furaha yake kwa kukupitishwa kwa sheria hiyo ambayo iligomewa na wabunge kupitishwa mara kadhaa, aliwaagiza TAKUKURU kuhakikisha wanaitumia kuwakamata watu ambao alidai kuwa tayari wameaanza kununua uongozi kwa kugawa mipira na kukarabati majengo ya CCM.

Namnukuu akiwaagiza TAKUKURU kuanza na uchaguzi huu wa mwaka huu: "Anzeni sasa kujipanga kuifanya kazi hiyo kwani naambiwa wanunuaji wa uongozi wameshaanza wengine wanapita na kuwagawa mipira na wengine wanakarabati majengo ya ofisi za CCM"

Alisema sheria hiyo iliyopitishwa itsaidia sana kudhibiti rushwa kabla na wakati wa kura za maoni ndani ya vyama vya siasa na wakati wa uchaguzi, na kueleza amefarijika na wenzake serikalini wakati watakapomaliza muda wao wa uongozi, kuacha wamejenga misingi imara ya utawala bora, demokrasia na maadili ya viongozi wa Umma, kwa sheria hiyo kutekelezwa.

Hata hivyo amekiri rusha katika kura za maoni CCM kushamiri, amesema: "Rushwa kubwa kwenye uchaguzi ipo wakati wa kura za maoni katika vyama pengine hata kuliko wakati wa uchaguzi wenyewe".

Ametoa ahahadi: "Mimi niko tayari kufanya kila linalowezekana ili kuiwezesha Takukuru kufanikisha kazi ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi nchini na nawataka muanze sasa na uchaguzi ujao".

Akionekana kugusia suala la Jerry Muro alisema: "Rushwa ipo katika sekta binafsi huko pia kuangalieni, kwani wakurugenzi na watendaji wa sekta binafsi wanafanya hivyo katika ajira, kutafuta masoko na zabuni. Bahati mbaya sana hata waandishi wa habari nao hawako salama katika kadhia hii, tena wanaoandika sana ndiyo nao wamekuwa wakipokea rushwa, rushwa ipo kila mahali ombi langu sote tuhusike na kuhusishwa katika mapambano haya".
 
Shadow

Shadow

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2008
Messages
2,906
Likes
72
Points
145
Shadow

Shadow

JF-Expert Member
Joined May 19, 2008
2,906 72 145
Tatizo sheria yenyewe inamatundu kibao asa ukisoma kifungu cha 21.3 cha hiyo EET
 
N-handsome

N-handsome

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,340
Likes
143
Points
160
N-handsome

N-handsome

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,340 143 160
Hilo nalo neno, problem yawezekana kabisaa ni PROPAGANDA hapo chacha!
 
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,373
Likes
1,632
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,373 1,632 280
Kama kweli anataka TAKUKURU wafanye kazi yao vizuri, kwanini anang'ang'ania hao TAKUKURU wawe chini ya ofisi yake na wasiwe INDEPENDENT wakiwajibika kwa BUNGE? Anafanya siasa watu watakaokamatwa ni wale mtandao wake usiowataka ama sivyo Sophia Simba angekuwa wa kwanza kukamatwa kwa rushwa wakati wa uchaguzi wa kina mama wa CCM!! Wanajanvi mmesahau Lowassa alivyowafanyizia wale wabunge wa Arusha walitaka kugombea NEC [ Mollel] na uenyekiti wa CCm mkoa halafu TAKUKURU ikawakamata kwa kisingizio cha kutoa rushwa? Baada ya uchaguzi kesi ikafutwa!!
 
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Likes
3
Points
35
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 3 35
Hata iweje, tusitegemee lolote jipya katka sheria hiyo zaidi ya kuwapamba hao TAKUKURU kwa kazi wasiyoifanya!Nchi hii siasa zitatumaliza.
 
Eric Cartman

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Messages
6,818
Likes
1,678
Points
280
Eric Cartman

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined May 21, 2009
6,818 1,678 280
safi sana tusubiri hiyo saini ipigwe na hiwe marufuku kutoa zawadi wakati wa campaign hawa akina Juma inabidi waanze kusikiliza sera sasa na si kusubiri punje kutoka kwa mh kadhaa.
 
W

Watanzania

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2009
Messages
727
Likes
3
Points
0
W

Watanzania

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2009
727 3 0
Kikwete amesikika akisema kutokana na kupita kwa mswada huo basi zoezi la kutia saini sheria hiyo atalifanya kwa mbwembwe sana tofauti na miswada mingine ya sheria ambayo amekuwa akisaini kimya kimya
Kwa kuwa CCM wameshanunua magari zaidi ya 200 kwa kukwepa ushuru na wanazuia vyama vingine kupata vitendea kazi kama hivyo.


Ametoa ahahadi: "Mimi niko tayari kufanya kila linalowezekana ili kuiwezesha Takukuru kufanikisha kazi ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi nchini na nawataka muanze sasa na uchaguzi ujao"
Du! kuanzia 2005 mpaka sasa bado ni ahadi tu, utekelezaji itakuwa lini?
Bahati mbaya sana hata waandishi wa habari nao hawako salama katika kadhia hii, tena wanaoandika sana ndiyo nao wamekuwa wakipokea rushwa, rushwa ipo kila mahali ombi langu sote tuhusike na kuhusishwa katika mapambano haya”.
Kwa hiyo ni uthibitisho kuwa waliomwandika sana 2005 wakati wa kampeni walipewa rushwa?
 
Msongoru

Msongoru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2008
Messages
306
Likes
5
Points
35
Msongoru

Msongoru

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2008
306 5 35
Ngoja tuamini na kusubiria alichosema mkuu!
 
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2007
Messages
6,446
Likes
396
Points
180
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2007
6,446 396 180
Huyo ndo kikwete wa matumaini mapya.

Anayoyasema na anayoyadhamiria ni vitu viwili tofauti.

Bisha!
 
D

Deo

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2008
Messages
1,216
Likes
119
Points
160
D

Deo

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2008
1,216 119 160
Ninamashaka sana na utekelezaji wake. Kumbukeni kuwa wakati wa uchaguzi ndani ya CCM TAKUKURU nao walipewa kazi, na walifanya kama walivyoagizwa yaani wasiopendwa walizuiwa na wengine walibabikizwa na kukamata. Na wenye kutoa maagizo walizidi kupeta na kuweka wapenzi wao ambao leo hii wanaosumbua kwa kutetea mafisadina kufanya makundi ndani ya chama. Dhamiri ya kweli ipo au ni kama vita vingine vya rushwa tuvionavyo sasa
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Huyu baba anawazimu ooh sorry.Kwanini sheria hii aifanye kwa mbwembwe kulikosheria nyingine?kutakuwa kuna kitu anachofaidika nacho tu.Kama nchi inaongozwa kihivi basi hii litaifa halifai kuwepo duniani,Sheria nyingine zinatiwa sahihi kwa mbwembwe nyingine bila mbwembwe kwanini?
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Sasa kama bosi wake anatuhumiwa kwa ufisadi usafi hapa upo wapi??
 
Mongoiwe

Mongoiwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
523
Likes
106
Points
60
Mongoiwe

Mongoiwe

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
523 106 60
Huyu baba anawazimu ooh sorry.Kwanini sheria hii aifanye kwa mbwembwe kulikosheria nyingine?kutakuwa kuna kitu anachofaidika nacho tu.Kama nchi inaongozwa kihivi basi hii litaifa halifai kuwepo duniani,Sheria nyingine zinatiwa sahihi kwa mbwembwe nyingine bila mbwembwe kwanini?
Hilo ni swali muhimu sana, lakini pengine nikukumbushe Gender Sensitive;
1.Huu ndiyo ule muswada wa sheria ambao wabunge waliupinga sana wakisema umechelewa kufikishwa hivyo usuburi hadi uchaguzi mkuu utakapoisha ili kufanya maandalizi ya kutosha. Waliugomea na kutaka uwasilishwe katika bunge lijalo ili hata kama wakiupitisha uje uanze kutumika katika chaguzi zijazo na siyo uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Sababu zao walidai, muda uliosalia ni mfupi kwa sheria hiyo kupitishwa na kuanza kutumika kwa vile inatakiwa kueleweka vizuri kwa wadau wote na hata walifikia hatua ya kuonya kuwa sheria hiyo ikipitishwa, wabunge na baadhi ya watu watafungwa kwa kufanya makosa kutokana na kutoielewa vizuri.


2. Lakini pamoja na kupinga mara kadhaa na kuugomea muswada huu bungeni, hatmae Bunge lilipitisha sheria ya gharama za uchaguzi, Februari 11 mwaka huu ambapo hata hivyo ulizua mjadala mkali kabla ya kupitishwa huku wabunge wakitoa mapendekezo ya kurekebishwa kwa vifungu kadhaa na vingine kuvifanyia marekebisho huku kampeni za chinichini zikielezwa kuanza katika majimbo mbalimbali ya uchaguzi.
Ukiangalia kwa makini sababu za JK kusema atausaini kwa mbwembwe ziko hapa. Wakati wabunge wanaugomea, akiwa katika sherehe za kuadhimisha miaka 33 ya CCM mnazi mmoja JK aliwalaumu wabunge kuwa wanafiki kwa vile wamekuwa wakilalamikia Rushwa lakini baada ya kupelekewa sheria hiyo wamekuwa wa kwanza pia kuipinga.


Kwa vile kupita kwa muswada huu kunatokana na nguvu kubwa ya JK na Pinda ilibainika kuwa kulikuwa na kundi la wabunge ambao walikuwa wakipinga kutokana na kudhania kuwa muswada huo umeandali kwa ajili ya kuwamaliza wao, hivyo kitendo cha kupita ni cha Historia kama alivyokiita yeye kwa vile anaamini huu utakuwa ndiyo Ulimbo wake wa kuwanasa na kuwabwaga wale wote ambao alikuwa akiwahitaji watoke katika mfumo wa ubunge na utawala.


Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa amefurahi kupita kwa muswada huo kwani sasa amewaagiza PCCB na hata Usalama wa Taifa waanze kazi ya kuwafuatilia wanaotoa rushwa. Hapa nadhani lengo lake kuwakamata wale waliokuwa wakimsumbua kwa sababu hiyo ya kisingiizo cha sheria huku akilipiza kisasi.Hata hivyo siku moja kabla ya mkutano wa 18 wa bunge haujafungwa, muswada huo ulipita baada ya majadiliano makali, hasa katika kipengele cha kuwakirimu wapambe wa mgombea na kufanya marekebisho kadhaa.
 
R

Rwiai

Member
Joined
Jul 17, 2009
Messages
45
Likes
0
Points
13
R

Rwiai

Member
Joined Jul 17, 2009
45 0 13
Asante kwa kueleza ukweli, kama umepata soft copy ya muswada huo uapload ktk jamii forum ili wadau wa mapambano dhidi ya rushwa waanze kuupitia
 

Forum statistics

Threads 1,251,743
Members 481,857
Posts 29,783,065