Serikali imesema itatoa fursa kwa wananchi wote kutoa maoni yao juu ya swala la katiba. Je Wakatoliki si Watanzania? Pia kauli hiyo imetolewa na taasisi ya Kanisa Katoliki haimaanishi kila mkatoliki nchini atakua na mawazo sawa na uongozi wa kanisa lao.
Hakika ukiwa mjinga na ukajikubali na ujinga wako, kamwe hutaziona fursa za kujinasua ktk ujinga wako kwa kuwa umeukumbatia. Hebu angalia hapo nilipokubadilishia rangi kwenye utumbo uliopost hapa, halafu jijibu swali dogo tu:
Shida yako ni kutoa maoni au kuona kuwa yapo mazingira yatakayowezesha maoni yako kufanyiwa kazi?
Kama serikali hii hii imekuwa ikikusanya maoni juu ya mambo mbali mbali na kuyaweka kapuni, leo hii tutakuwaje na imani na maneno tu ambayo siku zote yameahidiwa na yasitekelezwe? Rais aliyeshindwa kuwadhibiti wauza sukari kwa ahadi za kuwachukulia hatua ataweza kuwadhibiti maafisa wake watakapoanza kuipeleka katiba kwa mtindo wa kifisadi?
Mara nyingine tutumie akili zetu na sio kuunga mkono vitu bila kufikiri kwa sababu za woga au kutojiamini. Kama unaona serikali ina nia njema ktk kusaini huu muswada ilhali kuna manung'uniko lukuki, hebu niambie serikali ingepungua wapi kama ingeusoma kwa mara ya kwanza bungeni (kama kanuni inavyosema) na kuacha umma uujadili?
Mtu mwenye akili zake timamu, hawezi kumsikiliza dobi anayejiandaa kutia nguo zake kwenye maji machafu kwa kuwa tu dobi kasema
'usiwe na wasi wasi ndugu mteja, haya maji ni masafi tu na nguo zitatakata' wkt dhahiri unayaona yana tope.
Kaa ukijua kuwa kuna watu wamedhamiria kuhakikisha lengo na kuwa na katiba itakayoweza kuwawajibisha mafisadi halifikiwi. Hata mimi nakubali kuwa uwezekano wa kutoa maoni ni mkubwa, lkn msijitahidi kupotosha maana ya sisi wanaharakati kwa kutumia ukosefu wa elimu wa watu wengi. Hatusemi kuwa maoni hayatatolewa, tunachodai ni mazingira ya uwajibikaji na mgawanyo wa majukumu.
Nasisitiza tena Watanzania wenzangu:
TUTUMIE AKILI ZETU. Hawa wanaoendesha huu mchakato kwa ubabe wa wingi wa viti bungeni wana wanalonufaika na katiba mbovu itakayotungwa, sisi tunaodhulumiwa kila kukicha kwa
EPA, RAD, DOWANS, MEREMETA na mengineyo tusiunge mkono kwa kuambiwa nganjera za amani ambayo kiukweli hatunayo. Wanachofanya ni kuhakikisha hakitungwi kitu kitakachowawajibisha kwa mabaya waliyoifanyia nchi.