Kifaurongo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 4,288
- 2,438
Katiba ipo kwenye ilani ya Chadema 2010 lakini kwakuwa siyo chadema wanaongoza nchi hii na kwakuwa ccm waliodandia ilani ya chadema, ni vizuri kuachana nao. Hii ni credt kwa chadema kwani hoja ya kuwa ccm haiwezi kuwapa wananchi katiba imeshinda na huu ndio ukweli dhairi. Hivyo ni jukumu la wananchi kuipa chadema furusa 2015 ili ifumuwe mchakato mzima na kutia muhuri katiba ya warioba maana ndio ya wananchi.
Nakubaliana na wewe UKAWA wamenasa. Kwa sababu kiuhalisia hata kama Katiba ingemalizika leo isingetumika katika uchaguzi wa 2015 kwani kulikuwa na kipengele cha kipindi cha mpito. Kwamba rasimu ilitoa muda wa zaidi ya miaka miwili ili kurekebisha sheria ili ziendane na mabadiliko ndipo katiba iliyopitishwa iweze kutumika rasmi. Pili Bunge linaendelea kukamilisha kazi yake kilichoahirishwa ni upigaji kura kwa wananchi kuikubali au kuikataa katiba itakayopendekezwa na bunge. hivyo BMK halija/halitavunjwa. maana yake hatua ya kura ya maoni ikipita salama hapo mwakani tutakuwa tumepata katiba ambayo UKAWA hawakushiriki kuijadili.
Hivyo kinachofanyika sasa kilitegemewa kifanyike hata kama sio kukosa muda.