Kikwete awapongeza Karume, Seif | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awapongeza Karume, Seif

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Nov 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete amepongeza hatua iliyochukuliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Amani Abeid Karume, na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad, kukutana na kufanya mazungumzo kwa faida ya Wazanzibari.
  Rais Kikwete ametoa kauli hiyo wakati akikamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Misri kwa kutembelea shamba la kisasa la binafsi lililoko kaskazini mwa mji wa Cairo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo asubuhi jijini, Rais Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake na uamuzi wa CUF kuitambua rasmi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na kumtambua Karume kama Rais wake.

  Rais Kikwete amewahakikishia ushirikiano wake binafsi na ule wa Serikali ya Muungano na Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Taarifa hiyo ilisema: “Hiyo ni hatua kubwa na muhimu sana katika juhudi za kuleta umoja, amani na utulivu katika Visiwa vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.”


  Amewataka Wazanzibari na wananchi wote wa Tanzania kwa ujumla na jumuiya ya Kimataifa, kuwapongeza, kuwaunga mkono na kushirikiana na Rais Karume na Maalim Seif Sharif Hamad kwa uamuzi wao wa busara na moyo wao wa ujasiri.

  Rais Kikwete alisema kuwa katika kipindi hiki, viongozi hao wanahitaji kutiwa moyo ili waendeleze kwa kasi zaidi jitihada zao hadi kufikia ile haima njema inayotarajiwa, yaani Zanzibar na Tanzania ambayo watu wake wanaishi kwa amani, umoja, upendo mshikamano na ushirikiano kwa maslahi yao wote na nchi yao.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3521494&&Cat=1
   
 2. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona kachelewa mpaka waanze wenzie? huyu mh vipi?au alikuwa anasubiri kutayarishiwa (hata shukurani) - alitakiwa awe wa kwanza kuwapongeza seif/karume.
  mh .kumbuka wewe ni rais wa wote sisi wapemba na waunguja pamoja na watanganyika.
   
Loading...