Kikwete atunukiwa cheti!

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,600
1,195
Chuo kikuu cha tiba na sayansi muhimbili kimemtunuku cheti Rais Jakaya Mrisho kikwete kwa kutambua mchango wake katika sekta ya afya!
Ni kweli anamejitahidi kiasi lakini siungi mkono kila mara kumrundikia kiongozi vyeti kila mara!

Huyo ni Raisi anayofanya ni wajibu wake, na anatumia kodi zetu kuboresha sekta ya afya sasa hivyo vyeti vya nini

nchii hii tunakoelekea ni kuja kuwa na Raisi profesa asiye na elimu hiyo!
 
Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,174
2,000
Rais wetu ukimsifia tu tayari anakupa unachotaka na ndiyo maana wanafanya hivyo ili awaangalie ktk chochote
 
2c2

Member
Nov 5, 2009
98
0
Dongee kimewaumaaa haloooo
sizani kama ni donge ila Watanzania hawa ambao ni ma-great thinkers wanajaribu kufikiria mbali zaidi ambapo wajinga na wasio na upeo kama wewe hawawezi kufikiri, ulijaribu kujiuliza kwa nini Mwl hakuitwa Dkt na alibakia kuitwa Mwl. Mpaka wakati huu waleo japo ni marehemu.
 
Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,600
1,195
Ni nchi pekee duniani hospitali kuu ya taifa wagonjwa wanalala chini! Alafu leo wanampa cheti!
 
MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,474
2,000
Wanajipendekeza ili waongezewe mishahara na posho.
Njaa mbaya sana! Yuda alimdalalia Yesu!! Madaktari wakamtoa kafara ULIMBOKA!! sasa wanamuona Dhaifu ni bora na mwema kwao. SHAME ON THEM.
 
Mgaya D.W

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
966
250
Na atakapokuwa anaachia madaraka tutampa LEAVING CERTIFICATE akaonyeshe wajukuu na vitukuu vyake huko.
 
Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,600
1,195
Mwalimu Nyerere alichelewesha uhuru wetu ili nchi nyingine zijikombolewe, alijenga chuo kikuu cha dar salaam, amejenga mashule mengi sana,hivi mbona hakupewa hata cheti!

Ilikuwa ni wajibu wake
haiwezekani kila kitu kumpongeza wakati ni wajibu wake aliokabidhiwa na wananchi.

Nelsoni mandela mbona siyo dkt,
Kwame Mkuruma,
Jomo Kenyata,
Gadaff, clintoni,
Tufike mahali tuache haya mambo ya kipuuzi.

Haijawahi kutokea wananchi kuwa na hali ngumu kama kipindi cha jk leo mnampa tuzo.
 
Myakubanga

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,837

Point of correction:Mwalimu Nyerere alipokea udaktari wa heshima mara nyingi zaidi ya kiongozi yoyote hapa Tanzania,lakini hakutaka kuitwa Dr.
Kwa kweli alistahili.
 
Kibagata

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
771
225
waliompa hicho Chet ni Madaktari au hospital. Siamini masikio yangu. Watanzania tuwe makini na matendo yetu katika macho ya Ulimwengu. Haingii akilini mwezi April mnagombana na Serikali kwa Maslahi duni mwezi November mnatoa cheti kwa kiongozi kwa lipi alilofanya. mishahara imepanda? T scan imepona au imenunuliwa mpya? ? NYIE NI MADAKTARI AU WAGANGA WA KIENYEJI?
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,701
2,000
Hao walitoa hicho cheti waache kujikomba!hata miezi 6 bado tangu mgomo mkubwa vile leo mnamtuni cheti kwa lipi?kufanya anayofanya kwa mapungufu ni wajibu wake na alitakiwa afanye na zaidi.....
 
tetere

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
963
225
Raisi anajua siku moja ataulizwa alifanya nini akiwa rais. Sasa lazima awe na ushahidi wa vyeti/ Degrees etc. sijui ni kwa nini washauri wake wanaona kuwa hii ni njia nzuri ya kujenga trust/profile ya Rais. Au wanampa ile kitu ambayo roho yake inapendaa????????? Hawezi kataa?????? Au kama hamna zawadi nyingine anadai angalau chetiii??? Mr President, kweli???
 
muhogomtamu

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
412
195
Chuo kikuu cha tiba na sayansi muhimbili kimemtunuku cheti Rais Jakaya Mrisho kikwete kwa kutambua mchango wake katika sekta ya afya!
Ni kweli anamejitahidi kiasi lakini siungi mkono kila mara kumrundikia kiongozi vyeti kila mara!

Huyo ni Raisi anayofanya ni wajibu wake, na anatumia kodi zetu kuboresha sekta ya afya sasa hivyo vyeti vya nini

nchii hii tunakoelekea ni kuja kuwa na Raisi profesa asiye na elimu hiyo!
Si bora ya kuwa hivyo kuliko Maprofesa halisi ambao hatuoni hata uprofes wao unaisaidia vipi nchi hii

"Tumefika hapa tulipo kwa sababu tumeruhusu akili ndogo itawale akili kubwa" (Msigwa, 2012)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom