Kikwete atunukiwa cheti!

Chuo kikuu cha tiba na sayansi muhimbili kimemtunuku cheti Rais Jakaya Mrisho kikwete kwa kutambua mchango wake katika sekta ya afya!
Ni kweli anamejitahidi kiasi lakini siungi mkono kila mara kumrundikia kiongozi vyeti kila mara!

Huyo ni Raisi anayofanya ni wajibu wake, na anatumia kodi zetu kuboresha sekta ya afya sasa hivyo vyeti vya nini

nchii hii tunakoelekea ni kuja kuwa na Raisi profesa asiye na elimu hiyo!

:biggrin1::biggrin1: mtoa mada umenichekesha sana leo, hivi kwanini wabongo wanatunuki watu kwa sababu ya uzembe, huyu ni yule kiongozi wa nchi aliyesema madaktari wanaweza kuacha kazi mda wowote wakitaka, serikali yake ilimpeleka daktari mwabepande...juzi nilikua muhimbili nikashuhudia wagonjwa wanavyotaabika kwa kulala chini hakuna vitanda magodoro hayatoshi na madaktari hawataki kushuhulikia wagonjwa wakisema hawajalipwa mishahara/mafao yao...sasa huo mchango wake katika sekta ya afya ni upi? hamna hata aibu...nyie ndio wale wale mnaopitisha wanafunzi kwenda kidato cha kwanza hawajui kuandika wala kusoma ndio nyie nyie mnaogawa vyeti ovyo kama hichi
 
Mr. President ametunikiwa Udaktari kwa kufukuza Madaktari au kwa IKULU kumteka Dr. Ulimboka?
 
Back
Top Bottom