Elections 2010 Kikwete atuambie, Kauli zake zimekwenda wapi

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,763
Mwaka 2005 alikuja na kauli mbiu tamu sana, eti maisha bora kwa kila mtanzania. Nimeona sehemu nyingi, picha nyingi pamoja na maelezo ya watu wengi kuwa mambo sia kama walivyotaka iwe.

Mwaka huu wameizika kabisa kauli ile na hata hawatamani kuisikia tena. Bado wanang'ang'ana na ANGUKA zaidi (Ari zaidi, Nguvu zaidi Kasi zaidi). Wapi yale maisha bora yilohubiriwa? Wapi ile nchi ya asali na maziwa tuliyoahidiwa waana wa nchi?

leo hii wanakuja na kauli mbiu iliyopakwa ikakasi zaidi. Waana wa nchi wanazidi kudanganywa huko mikoani kuwa wataletewa meli, watu wa morogoro watajengewa nyumba ( wale wahanga wa mafuriko). Mbona ahadi hizi zinasubiri wakati wa kampeni? Wanaahidiwa barabara, miji yao itajengwa na kuwa kama ya ulaya. Huyo ni mgombea wa urais ambaye anawaasa wagombeaji wenzake wa udiwani na ubunge kuwa wawajibu wananchi kwa ufasaha na kuwapa ahadi kemkem.

Kuna sababu ani ya kutoamini haya wakati tuliwapa miaka mitano ya kutekeleza ahadi za awali na wakashindwa? Ninachoamini ni kuwa pale watu wanapokupa ridhaa ya awali inabidi ufanye jambo ambalo litakuwa reference ya baadae kwako na kwa wahusika. Inakuwaje haya hayakutekelezeka katika awamu ya kwanza yaje kutekelezeka katika awamu ya pili?

Waana wa nchi, hili ni changa la macho tu. hakuna jipya. CCM wakitaka twende sawa wafufue ile kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania na watueleze kwa kinaga ubaga maisha yameborekaje? Au ndio wingi wa magari njiani, tena Dar peke yake. mwaka 2010 HATUDANGANYIKI!
 
Back
Top Bottom