Kikwete atembelea Maliasili na kushinikiza ashirikishwe katika maamuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete atembelea Maliasili na kushinikiza ashirikishwe katika maamuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 31, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  RAIS Jakaya Kikwete ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka wazi kama imeshindwa kudhibiti ujangili wa wanyamapori, ili aliagize Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya operesheni maalumu dhidi ya majangili. Aidha ameiagiza wizara hiyo kuandika barua kesho kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kusitisha mara moja hatua za kulifanya eneo la Tao ya Mashariki linaloanzia milima ya Upare mkoani Kilimanjaro, Usambara mkoani Tanga mpaka Uluguru, Morogoro kuwa urithi wa Dunia.

  Akizungumza na watumishi wa wizara hiyo jana katika moja ya ziara zake kukagua utendaji wa wizara mbalimbali, Rais Kikwete aliitaka wizara hiyo kutofanya uamuzi wowote kama huo wa kufanya hifadhi za Taifa kuwa urithi wa dunia bila kumshirikisha yeye kwa kuwa ni sawa na kuuza Uhuru wa Watanzania.

  Kuhusu ulinzi wa wanyamapori, alisema hawezi kuendelea kusikia vifo vya wanyama hao na meno ya tembo yakisafirishwa kila kukicha na kutaka adhabu za wanaokutwa na hatia ya ujangili iongezwe kutoka miaka mitatu na kuwa zaidi ya miaka mitano. “Nina majeshi ya kila aina, muelekeo ulivyo nina mashaka kwamba mmezidiwa kudhibiti ujangili, kama ndivyo mseme, kama mwenendo ni huu kuna vyombo vya ulinzi vingi tu inaweza kufanya kazi hiyo, Jeshi linaweza kufanya operesheni kama ya mwaka 1989,” alisema Rais Kikwete.

  Mwaka 1989 operesheni ilifanyika operesheni maalumu iliyoitwa Operesheni Uhai ya kukabiliana na majangili na kuwezesha hali kuwa shwari kwa muda mrefu na idadi ya tembo iliongezeka. Pia alisema anafikiria kuweka mtambo wa setelite katika Hifadhi ya Selou ambakujangili umekithiri ili kuwashughulikia majangili kwa teknolojia ya kisasa zaidi. Alimtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na idara zake kujichunguza wenyewe kama kuna wasaliti kati yao baada ya waziri huyo kumueleza kuwa wanaimarisha kitengo cha intelijensia kudhibiti hali hiyo. “Mtaimarisha kitengo cha intelijensia lakini bado tembo wataendelea kufa tu…, Doha mlipata tabu kukubalika kwa sababu ulinzi wa wanyama pori bado si mzuri, hatuwezi kuendelea hivi ilivyo, takwimu zenu zinaonesha ujangili umepungua lakini mimi nadhani umeongezeka, yaani faru anapotea kitengo cha intelijensia kipo na baada ya siku tatu anakutwa amekufa! Hii hapana. “Kama mmezidiwa waziri usione haya, kama unashindwa kusema hapa, basi tutafutane, uninong’oneze, lakini hatuwezi kuendelea hivi, sifa yetu isiwe ni kukamata meno ya tembo bali iwe ni kuzuia tembo wasiuawe, hamhitaji msaada kwa wenzenu? Kama mmezidiwa mseme jamani!” Alisisitiza.

  Kuhusu suala la Tao la Mashariki, Rais alisema haiwezekani maeneo yote ya Upareni, Usambara, Uluguru na Udzungwa yenye wakazi wengi yawekwe kizuizini na mashirika ya kimataifa kwa kuwa uhuru wa kufanya shughuli za maendeleo utashindikana mpaka kibali chao. “Hili siwezi kulikubali, kuanzia sasa kibali nitatoa mimi, hamuwezi kukaa waziri na watu wako kupitisha suala hili, hamkunishirikisha,” aling’aka Rais.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mali Kale wa Wizara hiyo, Donatius Kamamba, mkataba wa kuyatambua maeneo na kuyaingiza katika hifadhi au urithi wa dunia kama maeneo maalumu ulifanyika mwaka 1972 na Tanzania iliridhia mwaka 1977. Pia aliitaka Wizara kufanyia kazi taarifa aliyopewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) jana asubuhi iliyoonesha mapato ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) yameshuka kutoka dola za Marekani milioni 20 hadi milioni 4.

  Rais hakufafanua zaidi ila alisema kama kuna ushauri wowote Tanapa imeingia na mwekezaji na kusababisha hasara hiyo, wakafikirie mara mbili kwani ni hasara kubwa kwa Taifa. Katika hatua nyingine aliagiza ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii usiwasahau Waswahili lakini akaonya kuwa Waswahili hao wawezeshwe kuelewa umuhimu wa kumiliki wao na si kuwa mawakala wa wageni.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Maliasili wamefanya makosa na Raisi anaongeza kosa juu ya kosa kama ilivyotokea kwa Dowans.

  Masuala ya uamuzi juu ya ardhi ya Tanzania kuwa hifadhi ya dunia suala linatakiwa lijadiliwe kwenye uwanja mpana wa wawakilishi wa wananchi (bunge). Kwamba rais ashirikishwe na kutolea uamuzi historia itajirudia.
   
 3. m

  matejoo Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Jamani nani anamshauri rais wetu? Nchi zinagombania kupata status ya urithi wa dunia wa UNESCO Tanzania yenyewe ina amrisha kusitisha maombi? Ni kweli swala la ushirikishwaji ni vocabulary katika wizara ya utalii na maliasili lakini kuondoa kabisa hiyo application UNESCO it too much. Naomba rais asitishe huwo uamuzi. Itaharibu sana jina letu katika medani ya uhifadhi. Nawasilisha!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Bado CCM inateswa na mfumo wa utemi badala ya kupeleka suala likajadiliwe na bunge kwa mapana na marefu, eti rais anaagiza kusitisha bila kujadiliwa na wawakilishi wa wananchi
   
Loading...