Kikwete "ashitaki" bunge kwa mawakili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete "ashitaki" bunge kwa mawakili!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fataki, Nov 3, 2008.

 1. F

  Fataki Senior Member

  #1
  Nov 3, 2008
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika hotuba yake kwa mawakili wa Tanganyika Law Society kwenye hafla ya kuchangia fedha za kuanzisha Kituo cha Msaada wa Kisheria (Legal Aid), hafla iliyofanyika Ijumaa usiku tarehe 31 Oktoba, 2008 kwenye viwanja vya Karimjee, Rais Kikwete alitahadharisha uwezekano wa mhimili moja kuvuka mipaka yake na kuingilia shughuli za mihimili mingine ili "kujipendekeza kwa wananchi ama kwa sababu ya ubinafsi, ama kwa kisingizio kuwa mihimili mingine haifanyi kazi yao vizuri". Akataka Watanzania wakatae hali hiyo!

  Mawakili wote waliokuwepo kwenye hafla hiyo walielewa maana ya kauli hiyo ya Kikwete: ilimlenga Sitta na Bunge lake la "viwango na kasi", ambalo hivi karibuni limekuwa mbele kuisukuma Serikali kuchukua hatua kuhusiana na EPA, Richmond, Twin Towers na uozo mwingine. Inaonesha kuwa Kikwete alikerwa sana na hatua ya Sitta "kumshauri" kuwa mkali kidogo katika kushughulikia mafisadi baada ya Kikwete kutoa hotuba ambayo wengi waliita ya "mdebwedo" Bungeni.

  Maoni yangu:
  (1) Bunge chini ya Sitta linatimiza wajibu wake vizuri. Hivyo Rais na yeye atimize wajibu wake sawasawa! Asipofanya hivyo, ni halali kwa Sitta na wabunge wengine kumsukuma atimize wajibu wake!

  (2) Kama ni suala la kuingilia madaraka ya mihimili mingine, Rais Kikwete na wasaidizi wake wamevunja rekodi. Uamuzi wa kuwabagua watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA kati ya kundi la kushitakiwa na kundi la kuendelea kutesa na fedha za wizi, ni kuingilia wajibu wa kikatiba wa mhimili wa mahakama!
   
 2. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  shukurani kwa taarifa.
  itakuwa vyema kama utatuwekea nakala ya
  hiyo hotuba ili nasi tuweze isoma kwa kina.
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  From the given (and the singularity knows how reliable such counsel often proves to be!), Kikwete is not only not leading, but it is clear that he is becoming paranoid.From the "mnamzomea nani?" incident in Tabora, his bar keeps stooping lower and lower to some despicably unpresidential low point.

  More than that, by defending himself, presumably preemptively, he is making his opponent's case more than he is defending himself, given the mood of the population.

  It is as if Kikwete has decided to be the anti-people president.
   
  Last edited: Nov 3, 2008
 4. F

  Fataki Senior Member

  #4
  Nov 3, 2008
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ahsante mkuu. Nimewaomba members wa TLS wanipe copy ya hotuba ya mkuu, nikiipata nitaimwaga hapa. In the meantime naomba usome nakala ya Tanzania Daima ya Jumapili, Novemba 2, 2008 ukurasa wa 2. Hotuba ya Rais iko well reported kwenye story yenye kichwa kisemacho: MATANGAZO YAMKERA JK.
   
 5. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Its just a matter of time folks. Be hold brethrens! Salvation is coming. We just have to trust our opposition parties. The more opposition MPs we have in the parliament, the more chances we have of changing this country.
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Watanzania tuna safari ndefu all over suddenly Sitta kawa mtendandaji mzuri kwa kuwa tu kamwambia Rais awe mkali kidogo.

  Hivi sio Sitta huyu huyu aliepitisha kibabe azimio la kumfungia Zitto? sio huyu aliemwambia Dr Slaa kaokota kwenye internet sakata la Benki kuu na kumnyamazisha? sio huyu huyu aliemnyamazisha Marehemu Wangwe? sio huyu anaewanyamazisha wapinzani kila uchao? Leo kawa mzuri kwa kauli hii tu

  Haya bwana naona umejiunga maalum kwa hili
   
 7. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Masatau,

  Ni lazima tuangalie vitu kwa depth na at a multi dimensional level.

  Ni kweli Sitta ana mambo yake, lakini ukweli kwamba Sitta ana mambo yake yamepinda hauzuii watu kuunga mkono issues za Sitta ambazo zitakuwa zimekaa sawa, hapa hapendwi mtu, si Sitta wala Kikwete wala Slaa, ni hoja tu.

  Na katika hoja hii, kama ilivyokuwa presented hapa, Sitta kambana rais panapofaa kwa njia ya checks and balances.Kwa hiyo anahitaji kuungwa mkono kwa sababu swala linawahusu wananchi kwa sana tu, na muungwana kachemsha kwa sana tu.

  Sasa kama kuna issue nyingine ya Sitta kutumia issues kufanya self promotion weka issues watu tuichambue self promotion yake, lakini hatuwezi kukataa kuiunga mkono critique valid ya Sitta eti kwa sababu Sitta is this or that.

  After all kila mtu ana makosa yake, kwa hiyo let's discuss issues, not people.
   
 8. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tanzania watu tuna attention span ya takriban dakika 5 na kumbukumbu isiyozidi siku kama saba hivi.

  Huyu Sitta alikuwa pilloried kwa kujinunulisha madawa ya pharmacy ya mamillioni. Leo nani anakumbuka hayo?

  Alitaka kufanya ufundi ufundi wakati panga la Lowassa linakuja Bungeni, mpaka akasema Anna Makinda hawezi kusimamia Bunge yeye asipokuwepo. Sema tu panga lenyewe la Mwakyembe likawa limewazidi vipimo, ikabidi wakubali.

  Leo kawa hero!!!
   
 9. M

  Mama JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Ndio hivyo tena wepesi kusahau, subiria hiyo 2010 sijui 2011 siku Kikwete anaapishwa tena ndio utachoka zaidi.
   
 10. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Our president needs to be strong,sasa afocus mbele,na arekebishe yote ya nyuma,Jamani,kuwa president unashikilia maisha ya watu,ni zaidi ya Pilot wakati akiwa angani.anyway tutafika ila itachukua muda,watu wasigive up.
   
 11. F

  Fataki Senior Member

  #11
  Nov 4, 2008
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, nani kasema Sitta ni hero? Nani kasema Sitta hana dosari zake? Hayo ya Pharmacy ambayo yalithibitika kuwa porojo na uongo wa mafisadi kutaka kumkomoa Mnyamwezi huyo, yanahusiana nini na hoja hii? Pundit ametoa hoja nzito sana na yenye mantiki alipokuwa anamjibu Masatu. I wish we could all think the same na kuweza kutenganisha pumba na mchele kila tunapojadili suala!
   
 12. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Matangazo yamkera Kikwete
  na Mwandishi Maalumu  WABIA wa maendeleo wa Tanzania wameshauriwa kuangalia uwezekano wa kufadhili vikundi dhaifu zaidi katika jamii kuweza kupata ushauri wa kisheria badala ya kutumia mamilioni ya fedha kufadhili matangazo ghali ya kukejeli juhudi za maendeleo za serikali ama wafadhili wenyewe.

  Rais Jakaya Kikwete pia aliwataka Watanzania kukataa uwezekano wa mhimili mmoja wa dola kujipa madaraka makubwa kupita yale yanayoruhusiwa chini ya mgawanyo wa madaraka kuingilia shughuli za mihili mingine.

  Rais pia alitaka Watanzania kujiepusha na tabia ya kujinyakulia sheria mkononi na kufanya vitendo kinyume cha sheria.

  Rais Kikwete alitoa rai hiyo wakati alipozunguza kama mgeni rasmi katika shughuli ya kuchangia fedha kwa ajili ya Chama cha Sheria cha Tanganyika (TLS), kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, juzi usiku.

  Shughuli hiyo ililenga kuchangia fedha za kuiwezesha TLS kuanzisha rasmi Mpango wa Msaada wa Kisheria na Kituo cha Utetezi wa Kisheria kwa wananchi wa kawaida, ambao hawana uwezo wa kugharimia huduma za kisheria ambazo katika Tanzania ni ghali mno kwa wananchi wa kawaida.

  Jumla ya sh 250,150,000 zilipatikana katika shughuli hiyo ya uchangishaji zikiwamo sh milioni 7.9 taslimu.

  “Napenda kutambua juhudi mbali mbali zinazofanywa na vikundi mbali mbali vya hiari katika kutoa misaada ya kisheria. Vinafanya kazi nzuri sana katika jamii yetu, na ninavitia moyo kuendelea na juhudi hizo,” alisema na kuongeza:

  “Wenzetu wengi katika jamii yetu – wajane, yatima, walemavu, na makundi mengine mengi wamekuwa wanategemea misaada ya namna hiyo katika kupata misaada ya kisheria. Ninaelewa fika kuwa kazi hiyo imekuwa siyo rahisi kwa sababu vingi vya vikundi hivyo vya hiari vinakosa fedha na huduma za kutosha kuzifanya kazi hizo.

  “Ni matumaini yangu kuwa wabia wetu wa maendeleo wataliangalia jambo hili, na jinsi ya kuvisaidia vikundi hivi kutekeleza juhudi hizi muhimu, badala ya kutoa fedha kwa taasisi ambazo zinatumia fedha hizo kulipa matangazo ghali kwenye televisheni ambayo yanalenga kukejeli juhudi za maendeleo za serikali na za wafadhili wenyewe.”

  Rais pia alisisitiza kuwa utawala wa sheria pengine ni jambo kubwa zaidi la mafanikio ya jamii ambalo Watanzania wanaweza kuwarithisha watoto wao na wajukuu wao.

  “Ni kinga na ngome kuu dhidi ya watu kujitwalia sheria mkononi na uwezekano wa watu kurubuniwa kufanya vitendo vya kujifurahisha tu. Ni utawala wa sheria unaotutawala, unaomlinda kila mmoja wetu wakati tunapopambana na wale wasiokubaliana nasi, ama wanaotofautiana nasi kwa sababu yoyote ile,” alisema.

  Kuhusu mihimili mbali mbali ya dola, Rais Kikwete alisema: “Moja ya nguzo kuu za utawala wa sheria ni mgawanyo wa madaraka ya dola. Ni lazima tuwe waangalifu na wenye wasiwasi mkubwa wakati mmoja wa mihimili hiyo inavuka mipaka ya utendaji wake kwa sababu za kutaka kujipendekeza kwa wananchi ama kwa sababu ya ubinafsi – ama kwa kisingizio kuwa mihimili mingine haifanyi kazi yao vizuri. Ni lazima tukatae jambo hili.”

  Kaaazi kwelikweli
   
 13. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwamba Sitta alikuwa na ka scandle ka kununua madawa ya mamilioni ni porojo na uongo?

  "Ni kweli kuwa mwezi uliopita, Spika Sitta alilipwa shilingi milioni mbili katika kipindi cha wiki moja kwa ajili ya kununulia dawa katika duka la dawa la Oysterbay,"
  Damian Foka, Katibu wa Bunge, akiliambia TanzaniaDAIMA, 28 Machi 2008.

  Mara nyingi najua ninachokiongea, Fataki, na kama sijui najaribu kuhakiki facts zangu kabla ya kubandika madudu ya dataz hapa.

  Yani tumeshasahau kwamba Wabunge walitaka independent inquiry against shutuma lukuki za Sitta ? Matokea yake huyu huyu clerk, Foka, ambae ni subordinate wa Spika akaenda kumchunguza Spika ?

  Tusiwasafishe na kuwageuze mashujaa hawa kina Sitta kwa vile tu waliharibu zaidi ya siku 7 zilizopita.
   
 14. H

  Huduma Member

  #14
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wabunge wetu wanachotaka ni kula, kunywa, kulala na kustarehe. Masikini hawa hawakutaka ubunge ili kusaidia kubadili maisha ya Mtanzania hata kwa ioa. Sasa wanashtakiwa kwanini?

  Kuna wenye nyumba mara kwa mara utawasikia wanalalamika kwamba kuna wanaokaa kwake ambao kazi yao ni kujaza choo tu!

  Hivi huyu mwenye nyumba Mtanzania anasemaje kuhusu wategemezi hawa wa bunge wanaoishi katika nyumba yake?
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135


  Wakati mwingine najiuliza hivi huyu ndugu yetu Jk huwa huko kichwani kuko shwali?

  Inakuwaje kila mara anasema kile asicho kimaanisha?
  Hivi yeye anapo ingilia sheria za nchi kuamua mwizi yupi ashitakiwe na kuwasemehe (EPA) wengine kabla hawajafikishwa mbele ya sheria na kuhukumiwa yeye haoni kwamba anaingilia muhimili mwingine????

  Jk toa kwanza kibanzi ndani ya jicho lako kabla hujaangalia boriti kwa jicho la mwenzio!
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wananchi ndio WAAJIRI wa mihimili yote mitatu. Mihimili hiyo sio tu inatakiwa ijipendekeze kwa mwajiri wao, bali pia IWAJIBIKE kikamilifu kwa WANANCHI kwa maneno na vitendo vyao kila siku.
   
 17. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  ![/QUOTE]

  Unampigia mbuzi gitaaa???!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...