Nilitaka tu kuuliza ni lini amegundua haya?
"Nchi za Ulaya zinatoa ruzuku ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 365 kwa mwaka kwa wakulima wao. Wakulima wetu hawawezi kushindana na wakulima ambao wanapewa ruzuku ya namna hii. Ndiyo maana tunasema kuwa mfumo na taratibu kwenye ngazi ya kimataifa lazima zibadilike, ili kutoa nafasi kwetu kuendelea,"alisema.
Sio kila kitu ni kupinga tu, ni kweli mfumo wa uchumi wa kimataifa unainyonya Afrika, na hili hawezi kuliondoa Kikwete mwenyewe bali muungano wa Afrika (AU) pamoja na zile "Regional blocks" kama Afrika Mashariki (EAC), COMESA, SADC nk hazitajiweka sawa. Hili la ruzuku ni baya mno, nchi tajiri zinapotoa ruzuku, ina maana bei ya mazao yaliyozalishwa na hawa waliopewa ruzuku huwezi kuifananisha na bei za mazao toka Afrika. Kumbuka ugomvi wa Ethiopia na Starbucks
Kuna mashirika kama IFM, World Bank nk, haya hutoa misaada kwa masharti. Wanaweza kukwambia kabla ya kukupa msaada badili mtaala wa Elimu, punguza wafanyakazi nk. Na masharti mengi huumiza hizi nchi zetu masikini. Burundi wana matatizo, waliweza kuunganisha majeshi yao, kutoka vikundi vya uasi, wakati nchi inatulia na kundi la mwisho la uasi linataka kuingia serikalini, wanaambiwa wapunguze jeshi, wakati hata hawa waasi wapya sharti mojawapo la kusimamisha vita ni wanajeshi wao waingizwe kwa jeshi la Taifa. Sasa unawaingiza waasi, na hapo hapo una sharti toka kwa haya mashirika ya kimataifa upunguze jeshi. Hii ni kuwatafutia ugomvi mpya, kupunguza wanajeshi kuna wakati ni hatari hasa katika nchi iliyotoka vitani, manake unaweza zalisha waasi wapya. Kama haya mashirika ya kimataifa yangetupenda yangesema wapunguze kuajiri wanajeshi kwa kipindi fulani.
Angalia Zimbabwe, baada ya kutofautiana na hao watu wa Magharibi, uchumi wao uko wapi?. Hivyo tusilaumu tu bila kuangalia ukweli. Kikwete kasema kweli kuwa uchumi wa kimataifa unainyonya Afrika, hawataki tuendelee ili kila kitu tutegemee toka kwao. ILA MUHIMU NI VIONGOZI WA AFRIKA KUJITAHIDI KUJIWEKEA MAZINGIRA YA KUWEZA KUFANYA BIASHARA WAO KWA WAO NA KUONGEZA NGUVU KTK UMOJA.
........aende zake huko..........asituletee za kuleta hapa........mtu unataka kutoa statement kubwa....lakini hutaki kuonyesha juhudi ya kuyazima hayo maovu nyumbani kwako........sit down and keep quite......
Na wewe usipotupa matokeo ya investigation yako ya Dk. Masau then you need to sit down and be quite....Lol
Sio kwamba tunapinga; ila tunachouliza ni "what is he doing about it?"
Akikutana na waheshimiwa wa nchi hizo za magharibi wanazungumza nini?
We do not have to re- invent the wheel, tulikuwa na kiongozi anaitwa Julius Nyerere. Aliwahi kuyasema haya haya na yeye hakuishia kusema tu. He confronted these western leaders about this inequality. Sasa hawa viongozi waliofuata wanaona aibu ku-identify with Julius Nyerere in international issues, kwa hiyo wakisema wanachosema tunaona ni geresha tu. Ni kama tu wamegundua sudenly kuwa the world is round.
......wee......naona unamuogopa.......Kuhani......eehh.........kwi kwi kwi kwi
Aaah huyo jamaa (naogopa hata kumtaja) moto wake si mchezo bana...
Wewe najua uko sleki mayai na moto wako ninauwezo wa kuumudu....
........aende zake huko..........asituletee za kuleta hapa........mtu unataka kutoa statement kubwa....lakini hutaki kuonyesha juhudi ya kuyazima hayo maovu nyumbani kwako........sit down and keep quite......
Sio kila kitu ni kupinga tu, ni kweli mfumo wa uchumi wa kimataifa unainyonya Afrika, na hili hawezi kuliondoa Kikwete mwenyewe bali muungano wa Afrika (AU) pamoja na zile "Regional blocks" kama Afrika Mashariki (EAC), COMESA, SADC nk hazitajiweka sawa. Hili la ruzuku ni baya mno, nchi tajiri zinapotoa ruzuku, ina maana bei ya mazao yaliyozalishwa na hawa waliopewa ruzuku huwezi kuifananisha na bei za mazao toka Afrika. Kumbuka ugomvi wa Ethiopia na Starbucks
Kuna mashirika kama IFM, World Bank nk, haya hutoa misaada kwa masharti. Wanaweza kukwambia kabla ya kukupa msaada badili mtaala wa Elimu, punguza wafanyakazi nk. Na masharti mengi huumiza hizi nchi zetu masikini. Burundi wana matatizo, waliweza kuunganisha majeshi yao, kutoka vikundi vya uasi, wakati nchi inatulia na kundi la mwisho la uasi linataka kuingia serikalini, wanaambiwa wapunguze jeshi, wakati hata hawa waasi wapya sharti mojawapo la kusimamisha vita ni wanajeshi wao waingizwe kwa jeshi la Taifa. Sasa unawaingiza waasi, na hapo hapo una sharti toka kwa haya mashirika ya kimataifa upunguze jeshi. Hii ni kuwatafutia ugomvi mpya, kupunguza wanajeshi kuna wakati ni hatari hasa katika nchi iliyotoka vitani, manake unaweza zalisha waasi wapya. Kama haya mashirika ya kimataifa yangetupenda yangesema wapunguze kuajiri wanajeshi kwa kipindi fulani.
Angalia Zimbabwe, baada ya kutofautiana na hao watu wa Magharibi, uchumi wao uko wapi?. Hivyo tusilaumu tu bila kuangalia ukweli. Kikwete kasema kweli kuwa uchumi wa kimataifa unainyonya Afrika, hawataki tuendelee ili kila kitu tutegemee toka kwao. ILA MUHIMU NI VIONGOZI WA AFRIKA KUJITAHIDI KUJIWEKEA MAZINGIRA YA KUWEZA KUFANYA BIASHARA WAO KWA WAO NA KUONGEZA NGUVU KTK UMOJA.
Ndiyo, kulikuwa na unafuu. Wafaransa walianzisha Paris club kuwapunguzia mzigo wa madeni nchi zinazoendelea. Hata haya madeni tuliyosamehewa ya EPA yalitokana na juhudi zake Nyerere. Ilikuwa wajibu wa viongozi waliofuataBaada ya Nyerere kuwaambia kulikuwa na unafuu, ama haya yanaendelea hadi leo. Hawa jamaa wa Magharibi unadhani hawalijui hili, wanasubiri waambiwe ama kelele?. Suala ni Viongozi wetu wa Afrika kuwa wamoja, kama nilivyoeleza ktk "post" yangu, ndio tutaondoa huu mnyanyaso. "dont mourn, organize".