Kikwete asema mfumo wa uchumi kimataifa unainyonya Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete asema mfumo wa uchumi kimataifa unainyonya Afrika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 26, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Date::2/25/2009
  Kikwete asema mfumo wa uchumi kimataifa unainyonya Afrika
  Na Mwandishi Wetu
  Mwananchi

  RAIS Jakaya Kikwete amesema mfumo na taratibu kwenye ngazi ya kimataifa lazima zibadilike, ili kutoa nafasi kwa wakulima wa mataifa masikini waweze kushindana na wakulima ambao wanapewa ruzuku wa nchi tajiri na kwa namna hiyo kutoa nafasi ya kuendelea kwa Afrika na Tanzania kwa ujumla.

  Hayo aliyasema na kunukuliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, alipokuwa akijibu swali kutoka kwa mwanafunzi mmoja ambaye alitaka kujua kwa nini Bara la Afrika limebaki nyuma kwa maendeleo, na kwa nini kasi yake ya kuendelea ni ndogo.

  “Nchi za Ulaya zinatoa ruzuku ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 365 kwa mwaka kwa wakulima wao. Wakulima wetu hawawezi kushindana na wakulima ambao wanapewa ruzuku ya namna hii. Ndiyo maana tunasema kuwa mfumo na taratibu kwenye ngazi ya kimataifa lazima zibadilike, ili kutoa nafasi kwetu kuendelea,”alisema.

  Rais Kikwete alisema kuwa sababu hiyo pamoja na mfumo wa sasa wa kimataifa usiokuwa wa haki wa uchumi na biashara, wenye kuzipendelea nchi tajiri, zimechangia kwa kiasi kikubwa kudumaza maendeleo ya Afrika.

  “Mataifa yote duniani, wakati mmoja ama mwingine wa historia, yalikuwa masikini. Kuna sababu nyingi za hali ya sasa ya Afrika kubakia nyuma na moja ya sababu hizo ni ukoloni ambao uligeuza Bara hili kuwa chimbuko la malighafi na soko la bidhaa kwa ajili ya nchi tajiri zilizotutawala,”alisema.

  Alisema maendeleo ni mchakato na kwamba , hayawezi kuja ghafla kama ndoto, na kufafnua kwamba Afrika iko nyuma siyo kwa sababu uongozi mbovu bali nimfumo.

  “Haiwezekani kuwa uongozi wa nchi zote 54 za Afrika hauna uwezo. Unahitaji mfumo wa uchumi wa kimataifa wa haki na hili ndilo jambo tumelizungumza miaka mingi tangu wakati wa mazungumzo ya Uruguay na sasa tuko Doha.

  Tunasema kuwa wakulima wote hawawezi kutoka kwenye umasikini wakati wanazuiliwa kuuza mazao yao kwa bei nzuri na za haki duniani kwa sababu ya nchi tajiri kulinda masoko yao kwa kutoa ruzuku kwa wakulima wao,” alisema Rais na kuongeza.

  “Maendeleo ni mchakato, tena mgumu. Huwezi kuamka asubuhi moja na kujikuta tayari ,” Rais Kikwete aliliambia kundi la wanafunzi kutoka Tanzania na Ujerumani wakati alipokutana na kuzungumza na wanafunzi hao jana, Ikulu, Dar es Salaam.

  Kundi hilo la wanafunzi 25 kutoka nchi za Tanzania, Ujerumani, Kenya, Ethiopia, Mauritius, Uganda na Rwanda linashiriki katika mpango wa kubadilisha uzoefu kati ya wanafunzi wa Afrika na Ujerumani wa “Go Africa, Go Germany” unaodhaminiwa na Rais wa Ujerumani, Horst Kohler.

  Katika mazungumzo hayo na wanafunzi hao, Rais pia alijadili kuhusu uundwaji wa Serikali ya Afrika, mchakato wa kuunganisha uchumi wa nchi za Afrika Mashariki chini ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), nafasi ya suala zima la ardhi katika ushirikiano wa EAC, na mikopo ya kugharimia elimu ya juu nchini.

  Alipoulizwa na mwanafunzi kutoka Ujerumani kuhusu ni nini anadhani ni changamoto kuu kuliko zote ambayo inaikabili Tanzania kwa sasa, Rais Kikwete bila kusita alijibu, “umasikini,” na kuendelea kufafanua umuhimu wa kuongeza uzalishaji katika kilimo kama njia kuu ya kuwatoa wananchi walio wengi katika umasikini kwa haraka zaidi.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kusema kweli jamaa anatia huruma.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa Afrika nao wamechangia sana katika kunyonywa kwa nchi za Afrika. Kwa mfano serikali yetu imesaini mikataba ya uchimbaji dhahabu ambayo 'wachukuaji' wanachukua 97% ya mapato na kutuachia sisi 3% ya mapato huu ni unyonyaji wa hali ya juu na hakuna nchi yoyote duniani itapata maendeleo ya kweli kwa kusaini mikataba mibovu kama hii. Pamoja na Kikwete kuahidi kuipitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini wakati wa kampeni zake, huu ni mwaka wa nne sasa tangu aingie madarakani hajafanya lolote ili kutimiza ahadi yake ya kuipitia mikataba hiyo na kuhakikisha ina maslahi kwa Watanzania. Hapa wa kumlaumu si mfumo wa uchumi wa dunia bali ni viongozi ambao watasema chochote ili wachaguliwe halafu ahadi zao wanaziweka pembeni.

  Kuhusu changamoto linaloikabibili Tanzania kwa sasa, sikubaliani kwamba umaskini ndiyo tatizo letu kubwa, bali tatizo kubwa la Tanzania ni viongozi mafisadi, wanafiki, waoga, walioweka mbele maslahi yao binafsi na ya chama chao badala ya Watanzania hili ndilo tatizo letu kubwa sana.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nilitaka tu kuuliza ni lini amegundua haya?
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mfumo huo unaionyonya Afrika.

  Lakini ni viongozi wa CCM na serikali yake ndiyo walifungua milango mizito ya chuma pale BOT na kupakia Maburungutu ya noti za dolali zaidi ya Tani 50 na kugawana kama peremendi na kuliingiza taifa katika songombingo la kiuchumi.

  Ni nani aliyewatuma kuiba fedha BOT mchana kweupe? Ni wakuu wa mfumo wa uchumi duniani au ni Ukenge wa akili zaviongozi wa CCM?
  Mfumo wa uchumi duniani unajipenyeza kunyonya Afrika kupitia ufinyu wa akili za viongozi wetu wenyewe, wanaojiingiza na kujikita madaraka kwa kutumia fedha za chanjo za watoto na dawa za vidonda aidha chakula cha wagonjwa pale Mwaisela.

  Ni kweli mfumo wa uchumi duniani unainyonya Afrika pia ni ukweli kwamba viongozi wa nchi zote za Afrika wakiwemo akina Kikwete nao pia wanatukuza mfumo wa kijambazi unaodhurumu na kujuhujumu juhudi zote za maendeleo ya Afrika kwa kutumia vibaya dhamana waliyo nayo kwa wananchi.
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ........aende zake huko..........asituletee za kuleta hapa........mtu unataka kutoa statement kubwa....lakini hutaki kuonyesha juhudi ya kuyazima hayo maovu nyumbani kwako........sit down and keep quite......
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ..........umesahahu siku ile aliposema hajui kwanini Tanzania ni MASKINI.........labda ndio sasa amegundua.........yaani aisee.......
   
 8. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vizuri amegundua moja ya matatizo mengi yanayotufanya tuwe maskini lakini tuanze na kurekebisha kwetu kabla kuanza kulaumu.
  Tuache vita za wenyewe kwa wenyewe,
  tuunde umoja strong wa waafrica,
  tuache kung'ang'ania madaraka,
  tuache kutoa na kupokea rushwa,
  tuache kujiibia wenyewe kwa kusaini mukataba tata,
  tuwache kusapport watu kama Mugabe,
  tuwe wakweli na kadhalika. THINK TWICE


  SAHIBA.
   
 9. T

  Tom JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JK ni limbukeni, maneno mazito lakini matendo sifuri.

  Hizo hadithi zimesikika toka tunapata uhuru, inasikitisha kuwa mpaka leo hajui kuwa ni jukumu la serikali zetu kujipangia na kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa nchi zetu kwa kufanya kazi na si kwa maneno matupu majukwaani. Sio lazima kuleta maendeleo kwa kupitia kilimo kwanza, tunaweza kabisa kuanzia na madini na viwanda, muhimu ni kujua kipi tuna advantage kubwa. Kama hatujui advantages zetu basi hata nchi zilizoendelea zifute ruzuku kwa wakulima wao, kwetu haitasaidia kitu, watakaolima na kuuza mazao ya kutosha watakua haohao wa Ulaya/US.

  Kwanza kilimo Afrika kipo ila si cha kibiashara, kwa mfano TZ tuna ng'ombe wengi sana lakini economic impact yake ndogo, si kweli kwamba nyama na maziwa hayana soko la kimataifa bali kwa kuwa serikali yetu haijajua mpaka leo kwamba huo ni uchumi tosha wa kuweza kutukomboa - ni advantage yetu. Ng'ombe si lazima wawe kwenye farms km Ulaya/US. Ukweli ni kwamba JK amepoteza sababu halisi ya AFRIKA KUA NYUMA katika kutapatapa katika uwanja mkubwa mno kutafuta jibu wakati anahitaji jibu dogo tu.

  Kwa mfano, China walijifungia na wameitumia vema nafasi 'advantage' yao ya opening up na wameitumia cheap labor yao, uwezo wao wa kupanga mambo yao vizuri na kucontrol watu wao ili kuwavuta, kuwazalishia na kuwatajirisha Wazungu kwa kuwazalishia bidhaa za viwandani katika viwanda vinavyojengwa/wekezwa na wazungu wenyewe. Sisi tuna uwezo kabisa wa kutumia advantage yetu ya madini, gasi, bahari, ng'ombe, nk.

  Je tunazijua advantages zetu nafauti kwa mfano na za Kenya. Nchi zote Afrika haiwezekani kujikwamua ati kwa kua tu Ulaya/US wameondoa RUZUKU kwa wakulima wao. TZ lazima kwanza tufanye chenye advantage kubwa kwetu tofauti na kile wenzetu Kenya, Uganda, Sudan, nk wanafanya ili kufyonza utajiri toka huko uliko. Kila nchi ya Afrika ifanye kwa 'advantage' iliyonayo, sio kufuata tu mkumbo, km JK anavyofikiri.
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sio kila kitu ni kupinga tu, ni kweli mfumo wa uchumi wa kimataifa unainyonya Afrika, na hili hawezi kuliondoa Kikwete mwenyewe bali muungano wa Afrika (AU) pamoja na zile "Regional blocks" kama Afrika Mashariki (EAC), COMESA, SADC nk hazitajiweka sawa. Hili la ruzuku ni baya mno, nchi tajiri zinapotoa ruzuku, ina maana bei ya mazao yaliyozalishwa na hawa waliopewa ruzuku huwezi kuifananisha na bei za mazao toka Afrika. Kumbuka ugomvi wa Ethiopia na Starbucks

  Kuna mashirika kama IFM, World Bank nk, haya hutoa misaada kwa masharti. Wanaweza kukwambia kabla ya kukupa msaada badili mtaala wa Elimu, punguza wafanyakazi nk. Na masharti mengi huumiza hizi nchi zetu masikini. Burundi wana matatizo, waliweza kuunganisha majeshi yao, kutoka vikundi vya uasi, wakati nchi inatulia na kundi la mwisho la uasi linataka kuingia serikalini, wanaambiwa wapunguze jeshi, wakati hata hawa waasi wapya sharti mojawapo la kusimamisha vita ni wanajeshi wao waingizwe kwa jeshi la Taifa. Sasa unawaingiza waasi, na hapo hapo una sharti toka kwa haya mashirika ya kimataifa upunguze jeshi. Hii ni kuwatafutia ugomvi mpya, kupunguza wanajeshi kuna wakati ni hatari hasa katika nchi iliyotoka vitani, manake unaweza zalisha waasi wapya. Kama haya mashirika ya kimataifa yangetupenda yangesema wapunguze kuajiri wanajeshi kwa kipindi fulani.

  Angalia Zimbabwe, baada ya kutofautiana na hao watu wa Magharibi, uchumi wao uko wapi?. Hivyo tusilaumu tu bila kuangalia ukweli. Kikwete kasema kweli kuwa uchumi wa kimataifa unainyonya Afrika, hawataki tuendelee ili kila kitu tutegemee toka kwao. ILA MUHIMU NI VIONGOZI WA AFRIKA KUJITAHIDI KUJIWEKEA MAZINGIRA YA KUWEZA KUFANYA BIASHARA WAO KWA WAO NA KUONGEZA NGUVU KTK UMOJA.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sio kwamba tunapinga; ila tunachouliza ni "what is he doing about it?"
  Akikutana na waheshimiwa wa nchi hizo za magharibi wanazungumza nini?
  We do not have to re- invent the wheel, tulikuwa na kiongozi anaitwa Julius Nyerere. Aliwahi kuyasema haya haya na yeye hakuishia kusema tu. He confronted these western leaders about this inequality. Sasa hawa viongozi waliofuata wanaona aibu ku-identify with Julius Nyerere in international issues, kwa hiyo wakisema wanachosema tunaona ni geresha tu. Ni kama tu wamegundua sudenly kuwa the world is round.
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Feb 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Na wewe usipotupa matokeo ya investigation yako ya Dk. Masau then you need to sit down and be quite....Lol
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ......wee......naona unamuogopa.......Kuhani......eehh.........kwi kwi kwi kwi
   
 14. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Baada ya Nyerere kuwaambia kulikuwa na unafuu, ama haya yanaendelea hadi leo. Hawa jamaa wa Magharibi unadhani hawalijui hili, wanasubiri waambiwe ama kelele?. Suala ni Viongozi wetu wa Afrika kuwa wamoja, kama nilivyoeleza ktk "post" yangu, ndio tutaondoa huu mnyanyaso. "dont mourn, organize".
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Feb 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Aaah huyo jamaa (naogopa hata kumtaja) moto wake si mchezo bana...

  Wewe najua uko sleki mayai na moto wako ninauwezo wa kuumudu....
   
 16. O

  Ogah JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .......the real "true substance of life" coming..........watch me!
   
 17. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  .........Sit doown and keep quite...!!! Mwinyi kept quite for 10 years, JK 10 years, 20 years of keeping quite!
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Mfumwa, nakubaliana kabisa na wewe lakini wakati huo huo na Viongozi wa nchi mbali mbali za Afrika wanachangia kuendeleza unyonyaji huo wa Mataifa yetu ya Afrika. Mfano ni huo wa mikataba ya uchimbaji wa dhahabu. Siyo siri kwamba mikataba iliyosainiwa na viongozi wetu haikujali kabisa maslahi ya Watanzania kwa kuwaachia wachukuaji wachukue 97% na sisi wenye mali kubaki na 3%. Kikwete analijua hilo kwamba mikataba hiyo haina maslahi na ndiyo maana akaahidi kwamba ataingalia upya ili kuifanyia marekebisho na kuhakikisha mikataba hiyo ina maslahi kwa Watanzania.

  Yuko madarakani mwaka wa nne sasa, hajafanya lolote la kuipitia mikataba hiyo na mwingine ule wa Buzwagi ulisainiwa akiwa madarakani nao pia hauna maslahi yoyote kwa Watanzania. Je, hapa wa kulaumiwa ni mfumo wa uchumi wa dunia au viongozi wabovu tuliokuwa nao wasiojali maslahi ya nchi zao? Jingine la kwenda kununua mashangingi 1,000 ambayo moja linagharimu kati ya shilingi 100 mpaka 150. Hizi pesa zingeelekezwa kwenye mambo muhumi ya Taifa zingesaidia sana katika kutatua baadhi ya matatizo yetu na kuleta maendeleo. Tunachukua kidogo tulichonacho na kuwapelekea Japan ambao wenzetu wako mbali sana kimaendeleo. Je, hapa wa kulaumiwa katika ununuzi wa mashangingi ni mfumo wa uchumi wa dunia?
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ndiyo, kulikuwa na unafuu. Wafaransa walianzisha Paris club kuwapunguzia mzigo wa madeni nchi zinazoendelea. Hata haya madeni tuliyosamehewa ya EPA yalitokana na juhudi zake Nyerere. Ilikuwa wajibu wa viongozi waliofuata
  kuendeleza hizo kelele lakini wameamua kukaa kimya kwa sababu zao wenyewe.
  Sasa mtu akikurupuka kana kwamba ndiyo amegundua mfumo wa uchumi wa kimataifa unanyonya nchi za Kiafrika tuna haki ya kujiuliza huyu alikuwa wapi?
   
 20. O

  Orkesumet Member

  #20
  Feb 27, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  tatizo tumekuwa watumwa wa misaada na kufubaza akili zetu. kila kitu tumekuwa tukiwatupia lawama nchi tajiri eti wanatoa ruzuku, misaada ya masharti magumu nk. wimbo umekuwa tangu nchi zetu zilivyopata uhuru hadi sasa. Hivi utawezaje kupiga hatua ya kimaendeleo kwa kutegemea misaada? kutegemea favors kutoka kwa nchi zilizoendelea? Kulikwamua bara la afrika katika hali hii ni kubadilisha mtazamo na kufanya vitu kwa kutumia models zetu, kusisitiza kuongeza thamani ya bidhaa kwenye nchi zetu kabla ya kuziuza nje ya bara letu nk. hii itapunguza utegemezi na hata itafika siku serikali zetu zitatoa ruzuku kwa wakulima wetu!
   
Loading...