Kikwete aongoza jopo teule la umoja wa mataifa kukabiliana na majanga ya afya duniani

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,812
1,824
1.JPG


Wakati Magufuli akiiwakilisha Tanzania vyema kitaifa, Kikwete anaiwakilisha vyema Kimataifa.

Kwenye picha akiendesha kikao cha jopo teule la umoja wa mataifa katika kupendekeza namna nzuri ya kukabiliana na majanga ya afya duniani huko jijini New York.

3.JPG
Wajumbe wa Jopo katika Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Sekretariati ya Jopo.

Jopo la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa la Kupendekeza Namna Bora ya Dunia Kukabiliana na Majanga ya Afya limekamilisha kazi yake wiki iliyopita jijini New York.

Jopo hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete lilikabidhiwa jukumu hilo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon tarehe 2 Aprili, 2015 na kupewa muda wa kuanzia Mei hadi Desemba 2015 kukamilisha kazi yake.

Jopo limefanya mikutano minne na kukutana na wadau mbalimbali wa afya zikiwemo taasisi za Umoja wa Mataifa, wadau wa maendeleo, wataalam mbalimbali na kupokea maoni na uzoefu kutoka kwa nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola.

Watu mashuhuri wanaounda Jopo hilo ni Mheshimiwa Michelin Calm-Roy aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Uswisi; Mheshimiwa Marty Natelagawa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia; Mheshimiwa Joy Phumaphi, aliyekuwa Waziri wa Afya wa Botswana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Mheshimiwa Celso Amorim aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil na Rajiv Shah aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID).

Jopo hilo linatarajia kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi January, 2016 na baadae kuwasilishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kwa hisani ya mpekuzi
 
Bila shaka zitakuwa za hao waliompa hiyo kazi. sidhani kama ni kodi zetu (correction allowed)
 
Dadake si kazikwa jana jamani?. Au Kwenye msiba nako Kuna washawasha? Ama kweli kikwete ni. Sikio la kufa
 
safari ya tano nje ya nchi tangu astaafu urais.

keshaenda Ethiopia,Uingereza,Afrika ya kusini,Comoro na Marekani.
 
Kuna story naskia anautafta ukatibu mkuu wa umoja wa taifa baada ya ban ki moon
 
Duh........... hakika haya sasa ni mapepo yanayomsumbua huyu jamaa!
Itabidi watumishi wa Mungu waanze maombi ya mfululizo na wafunge ili waweze kumwombea huyu jamaa wa Msoga ili 'mapepo' wake wa kusafiri nje ya nchi waweze kumtoka huyu jamaa.
 
Majanga ya Kiafya wakati Tz kipindupindu hadi Msoga... kila mkoa kipindu pindu, tena bado akiwa Rais...

Hapo ni per diem tu anatafuta na U vasco da gama anauendeleza kama kawa...!!!
Huyu jamaa bomu kweli...😨
 
safari ya tano nje ya nchi tangu astaafu urais.

keshaenda Ethiopia,Uingereza,Afrika ya kusini,Comoro na Marekani.

Mkuu unampunja! Ya 6 hiyo (kumbuka Ethiopia kaenda Mara 2). Magufuli naye hii sasa ni double standard, kwa nini atuzuie sisi hata kama safari zimelipiwa lakini huyu wanamwachia tu? Huyu jamaa ni kunguru hafugiki, juzi tu kamzika dadake yeye tayari kesharuka sasa tunaokuja kumhani tutakaa na nani? Mwishowe tumkute Salma peke yake atubambikizie kesi!! Kama hii safari ina kibali cha Magufuli tunamwomba Gerson Msigwa atuwekee hapa tujiridhishe!!
 
Wivu kwa watoto wa kiume ni jambo la hatari sana, jitu liko nyabitaka linataka kujilinganisha na Jk!
 
Kumfuatilia kikwete mtapata viharusi,mwacheni afanye kazi alizotumwa na UN
 
Back
Top Bottom