Kikwete anataka kuwaambia nini wanawake?

Kikwete anataka kuwaambia nini wanawake?

Mheshimiwa Mwl Steve

Senior Member
Joined
Nov 3, 2012
Posts
139
Reaction score
40
Kwenye mkutano mkuu wa nane wa chama cha mapinduzi,mwenyekiti amekuwa akitumia kauli tata akiita CCM kuwa chama ''dume'' na jana akaongeza kuwa chama dume tena dume la mbegu.Mi nadhani kwa nafasi yake ya urais na ile ya uenyekiti wa chama si sahihi hata kidogo kutumia maneno hayo kwa sababu CCM si chama cha wanaume peke yao.Hivi wanawake wanaojitambua wanapoambiwa kwamba wako kwenye chama dume wao wanajisikiaje? Na akitokea mtu akaita ccm kuwa chama JIKE? Najua watachukia.Inakuwaje rais wa nchi anakuwa gender biased? Wanawake kwa kauli hii wamedhalilishwa. I stand firm on my feet to be corrected!
 
yaani magamba ni dume la mbegu kama yeye mwenyekiti alivyo kidume kwa wake za watu!
 
Jinsi ya kiume inatumika kuonyesha uimara wa jambo au chombo . Katika hali ya kawaida huwezi kutumia jinsia ya kike kusifia
 
Ni mambo ya wanasiasa, hamna kitu serious hapo. CUF nao wanajiita chama dume hata kabla ya CCM.
 
mtu akikwambia una mambo ya kike utafurahi? ukipata jibu jua umejijibu tayari
 
Alitawaliwa na hisia tu huyo,mahaba kwa chama chake yameyazidi mapenzi so amekuwa mpofu.....!!!!
 
Jinsi ya kiume inatumika kuonyesha uimara wa jambo au chombo . Katika hali ya kawaida huwezi kutumia jinsia ya kike kusifia

Jibu zuri.......sasa je mtoa mada ni mwanaume!!!!

Maana sisi wanaume hapa hakuna hoja ya kujadiliwa......au ndo umagharibi umemkolea mtoa mada
 
Neno DUME hutumika zaidi kwa wanyama na majini. Huwezi kumuita binadamu mwenzio DUME yeye huwa ni MWANAUME. Pia DUME la mbegu humaanisha ng'ombe, mbuzi, kuku, majini nk. Kumwita mwanao DUME la mbegu ni kudhihaki.

CCM itakuwa ni mnyama au jini.
 
Ni maneno yasiyo na staha ambayo hayakutakiwa kutoka kinywani mwa Raisi wa nchi. Ni nini maana yake kujiita hivyo? kama si udhalilishaji? wa wanawake na wa vyama vingine? CCM wanatuambia nini kumpigia kura kwa zaidi ya asilimia 97% mtu kama huyu asiyechunga ulimi wake?
 
hapa unanikumbusha wakati watu wanaiambia kafu kuwa imeolewa na sisiem.

kiongoz mmoja/mwanachama wa kafu kule arusha akawa anajidai kuwa kafu ndo imeioa sisiem.(so kafu inailala sisiem)
 
Back
Top Bottom