Kikwete anaogopa kutamka neno "mafisadi"

The Informer

Senior Member
Jun 14, 2010
119
29
Katika hotuba zake zote nilizowahi kusoma na kuzisikia, sijawahi kuona Rais Jakaya Kikwete hata siku moja akitamka neno "mafisadi." Hata neno ufisadi nalo limekuwa ni nadra sana kutamkwa na Kikwete.

Mara zote huzungumzia watoa rushwa, wabadhirifu, watumiaji wabaya wa pesa za umma, etc. Neno "mafisadi" ni marufuku kwake Rais wetu huyu.

Nimekaa na kujiuliza sana pasipo kupata jibu. Katika pita pita zangu nikamuuliza mtu aliye karibu na CCM, kwa nini Kikwete hajawahi kutamka neno "mafisadi" hadharani kwenye hotuba zake?

Akanijibu kuwa Rais Kikwete hawezi kutamka "mafisadi" kwa kuwa watu wanaohusishwa na ufisadi ni marafiki zake wakubwa na ndiyo waliotoa pesa nyingi kuchangia kampeni zake za urais.

Baadhi ya mafisadi hao maarufu walio karibu sana na Kikwete ni pamoja na:

1. Edward Lowassa
2. Rostam Aziz
3. Shubash Patel
4. Tanil Somaiya
5. Yusuf Manji

Hawa mafisadi wanahusika na Richmond/Dowans, Kagoda, ukwepaji kodi, wizi wa fedha za umma, rada, uuzaji wa helikopta mbovu zilizouwa wanajeshi na kadhalika. Kesi zao kamwe hazitafikishwa mahakamani kwa kuwa rafiki yao yuko Ikulu.

"Hutamsikia Rais Kikwete kamwe akitamka neno mafisadi, kwani hiyo itawaudhi marafiki zake wa karibu wanaohusishwa na ufisadi," alisema kada huyo wa CCM.

Naomba wenzangu wa JF mnisaidie. Kuna mtu amewahi kumsikia Kikwete akitamka neno "mafisadi" hadharani?
 
Back
Top Bottom